Ukiona mwanamke anaikataa ndoa jua yamemfika hapa!

Amina Lizarazu
Huyo mwachie Mungu tuu
Huyo achukui round niamini mimi, lazima atakuja anatembelea magoti kutaka muyasululishe hili apate hata ile amani ya moyo tu.

Halafu wanaume huwa hatujuagi tu, hakuna mwanamke aliye timamu anaweza akakuamini na kuwa na mahusiano serious na wewe, pale atakapojua kwamba umetelekeza familia yako wala hauijali na badala yake una mjali yeye. Hayupo nasema!! sana sana atakuwa na wewe kimikakati hili aweze kutimiza mipango yake ya kiuchumi kwa sjri halafu baada ya hapo anakumwaga na wewe utabaki kama reference kwake kila mara atakapokuwa anawaongelea wanaume wa ovyo.

Huyo ex-mume siku sio nyingi hao mahawara watamuona hana maana na watamkimbia maana naamini hana kisima cha hela zitaisha tu.. kwanza ataanza kuku miss,kumiss watoto,atakumbuka zile good moments zote mlizokuwa mna spend together halafu ataanza kuwatumia watu wako wa karibu kukulainisha hili mkae meza moja atubu.
 
Habari za muda huu wakuu

Nimejiskia kushare historia yangu ya safari ya ndoa KWA UFUPI SANA wakuu ukiona mwanamke kachoka kavumilia mengi

Mimi ni mwanamke mwenye watoto3 niliolewa miaka14 iliyopita nkajaliwa watoto wa3.

Nimeishi kwenye ndoa ya mateso kwa miaka 12 hadi nilipoona inatoshaa na kuamua kukaa pembeni kujiepusha na malumbano.

Kwa kifupi tulipoingia kwenye ndoa na aliyekua mume wangu nikiwa naanza kazi wakati huo yeye alishafanya kazi sehemu tofautitofauti kwani hata kwa umri ni mkubwa kwangu amenipita miaka karibu 10

Tulipoana mwenzangu alikua anafanya kazi mbali na mimi (mikoa tofauti) na wakati huo mimi nilikua nafanya kazi ya mkataba mfupi. Tulikubaliana nisiache kazi hadi hapo nitakapopata kazi kule alipo.

Mungu mkubwa miezi miwili baada ya ndoa niliconcive nikaendelea na kazi hadi nilipojifungua.

Wakati nikiwa mjamzito nilianza kuhisi mwenzangu hajui majukumu yake kwani alikua anajua nilikua nalipwa kidogo sana tena nalipwa kwa wiki lakini hakuwahi kunisupport chochote kama mke iwe kodi, mavazi, au pesa ya kula.

Ikitokea amenipa pesa basi ujue labda laki1 au moja na nusu kwa miezi 6 tena baada ya kuomba sana na kulalamikiwa sana.

Mtoto wangu akiwa na miezi5 kazi yangu iliisha tukaamua niungane mwenzangu anakofanyia kazi. Tuliishi kwa amani, mwenzangu akiwa anaenda kazini Mimi nabaki nyumbani pia aliahidi kunitafutia kazi.

Basi wakati huo nikiwa mama wa nyumbani mtoto anaweza akawa anaumwa mwenzangu anaenda pharmacy ananunua dawa ananiambia nimpe yeye anaenda kazini.

Nilikuwa nabaki nyumbani nina chakula tuu ila senti tano sina. Kuna kipindi nilibaki na mtoto akazidiwa sina hata vocha ya kupiga sim.

Nilihisi kumpoteza mwanangu nikaomba wasamaria wema msaada mwanangu akatibiwa nikiahidi nitawalipa pesa zao. Jioni aliporudi mwenzaàngu nilimwambia alinyamaza nikampa namba za walionisaidia na kiasi walichonipa.

Hakuonyesha Kujali ila baada ya siku 2 aliwatafuta na kuwapa pesa yao. HAPO KENGELE ZA HOFU ZILIANZA KULIA KICHWANI NIKAONA ILI NIISHI MIMI NA MWANANGU LAZIMA NIFANYE KAZI.

Kama mwanamke yoyote nilimweshim sana mume wangu sikutaka kabisa kumuudhi nilikua naongea nae kwa busara kuhusu maisha na majukumu yetu kama wazazi ila hakuwahi kunipa majibu ya wasiwasi niliokua nao wala kuonyesha njia ya kupata suluhu. Niliumia na kuogopa sana na moyoni nilijua lazima nifanye kazi sana.

Basi nikampigia kaka yangu aliyekua ananitaftia vibarua, nikamwambia kaka huku sina kazi mwaka sasa,nikamwomba anitumie msg kuna kazi (japo haikuwepo) ili niweze kuomba nauli na kurudi sehemu ambayo ni kama nyumbani na ni rahisi hata kupata msaada

Nilirudi nikatafuta kazi nikapata na maisha yakaendelea.

Mwenzangu hakuwahi badilikaaa, kila kitu nilikua najifanyia mwenyewe, kodi, matibabu, kula, kuvaa na bills zote. Ikitokea amekuja basi ataweka laki mezani itatumika na kwisha kabla hata ya yeye kuondoka..lakini hasemi kitu achilia mbali mimi kumwambia nimekopa hapa na pale kujikimu. Kuna wakati niliomba wakubwa zake wamshauri lakini hakuna lililobadilika.

Miaka 5 baada ya ndoa nilikuja kugundua na wanawake kibao Kati yao akiwa girlfriend wake wa shuleni ambae alikua mke wa mtu ambae katika mawasliano yao ya email waliapa kutokuachana.NILIUMIA SANAAA NIKASEMA BASI NDOA STAKI TENA MAANA NATESEKA BILA SABABU ZA MSINGI.

Aliomba msamaha sikuweza kumsikiliza wazazi wakaanza kusuluhisha na baada ya kama miezi8 yaliisha tukaanza upya. Tuliishi hivyo siku zikawa zinasonga sikuskia tena habari za wanawake ila huduma ya familia haikuwepo bila ugomvi na ukitokea ametoa labda ada ya mtoto kama ni 1M atatoa laki4 na akishaoa hiyo chakula, matibabu, kodi, kuvaa sio juu yake uksema umjaribu kwa kumshauri kumhamishia mtoto shule za serikali anakataa

Miaka mi3 iliyopita hali ilizidi kuzorota, watoto 3 mzigo akanizidi, nikamwambia lazima kukaa na kujadili mstakabali wa familia hapo kwa Mara ya kwanza alinitukana na kuniambia sitakiwi kumsemesha chochote kwani kila ninachomwambia anakijua......nilishangaa NIKASEMA majukumu tuu yanatufikisha hapa! Wacha ninyamaze.

Baada ya siku chache nikagundua kumbe ana wanawake wanamsumbua hata yule old girlfriend bado yuko nae

Hapa ndipo nilifanya maamuzi kwamba mimi na yeye basi. Tuna watoto wazuri na nawapenda sana nadhani hata yeye anawapenda japo siwezi kumsemea....

Sikuona sababu ya mimi kuendelea kuishi na mtu ambaye

1.Hanijali

2.Hanipi support yoyote na zaidi

3.Ananisaliti kitu ambacho ni hatari magonjwa haya mengi tusijeacha watoto kizembe

Aanakuja akiomba msamaha nimemsamehe kabisa lakini siwezi kurudiana nae

Nilichoka roho, akili na mwili hata akioa leo aoe tuu

Nilichoka kufanya majukumu ya mama na ya baba na kusalitiwa juu
Ulichonacho huwezi kujua thamani yake mpaka kikuponyoke..
 
Huyo achukui round niamini mimi, lazima atakuja anatembelea magoti kutaka muyasululishe hili apate hata ile amani ya moyo tu.

Halafu wanaume huwa hatujuagi tu, hakuna mwanamke aliye timamu anaweza akakuamini na kuwa na mahusiano serious na wewe, pale atakapojua kwamba umetelekeza familia yako wala hauijali na badala yake una mjali yeye. Hayupo nasema!! sana sana atakuwa na wewe kimikakati hili aweze kutimiza mipango yake ya kiuchumi kwa sjri halafu baada ya hapo anakumwaga na wewe utabaki kama reference kwake kila mara atakapokuwa anawaongelea wanaume wa ovyo.

Huyo ex-mume siku sio nyingi hao mahawara watamuona hana maana na watamkimbia maana naamini hana kisima cha hela zitaisha tu.. kwanza ataanza kuku miss,kumiss watoto,atakumbuka zile good moments zote mlizokuwa mna spend together halafu ataanza kuwatumia watu wako wa karibu kukulainisha hili mkae meza moja atubu.

Mimi sina neno nae amesema amekosea sawa nimesikia, sina kinyongo wala chuki nae. Ila siwezi tena kuishi nae. Wacha na wanawake wengine wajitwalie labda kwao itakua heri
 
Stori umeandika lakini kuna maswali mengi na yanahitaji majibu

1. Mlipokuwa mbali (mikoa tofauti) tuna uhakika gani ulikuwa huchepuki?
2. Kwa maelezo yako inaonekana Mwanaume amechoka na tabia zako ambazo si rahisi ww kuziona. Maana kitendo cha Mwanaume kuacha Laki inamaana amekadiria ni siku za kumtunza mtoto huku ww akikuweka kando.

3. Inaonekana kabisa na ww unacheet na Mumeo amegundua ila Mwanaume hajawahi kukwambia na ndio maana yy yupo hivyo

4. Nyie wanawake mna matatizo sana na nyie ndio mnapelekea Wanaume kupata msongo wa mawazo na hata kupata Strokes. Wanawake kila mkiambiwa mfanye hiki nyie mnaenda kinyume. Na tabia ya kujibizana na Mwanaume pale anapoongea wanawake huwa mnayo sana hasa mkiolewa. Wanaume kuepuka hayo huwa wanarudi usiku hata akiwahi kutoka kazini lazima atafute sehemu ya kupoteza muda ili aingie nyumbani usiku. Kila mwanaume atakachoongea lazima mwanamke aseme ulikuwa kwa mahawara zako
Why so much of baseless prejudgements?

Hili bandiko lako limejaa assumptions ambazo hazina kichwa wala miguu. Hauna tofauti na wale wanawake wanaoamini "ukiona mwanamke kakengeuka basi ujue chanzo ni mwanaume" very stupid notion.
 
Mpeleke dada yako atampenda pia na wewe utafaidi vya shemeji
Sasa unagegedwa na nani au umekistaafisha? Kumbuka una watoto watatu wewe ndo baba na mama bora ukitulize ukishindwa nunua toy maana ukizaa tena utaisoma namba mamy wangu .
 
Stori umeandika lakini kuna maswali mengi na yanahitaji majibu

1. Mlipokuwa mbali (mikoa tofauti) tuna uhakika gani ulikuwa huchepuki?
2. Kwa maelezo yako inaonekana Mwanaume amechoka na tabia zako ambazo si rahisi ww kuziona. Maana kitendo cha Mwanaume kuacha Laki inamaana amekadiria ni siku za kumtunza mtoto huku ww akikuweka kando.

3. Inaonekana kabisa na ww unacheet na Mumeo amegundua ila Mwanaume hajawahi kukwambia na ndio maana yy yupo hivyo

4. Nyie wanawake mna matatizo sana na nyie ndio mnapelekea Wanaume kupata msongo wa mawazo na hata kupata Strokes. Wanawake kila mkiambiwa mfanye hiki nyie mnaenda kinyume. Na tabia ya kujibizana na Mwanaume pale anapoongea wanawake huwa mnayo sana hasa mkiolewa. Wanaume kuepuka hayo huwa wanarudi usiku hata akiwahi kutoka kazini lazima atafute sehemu ya kupoteza muda ili aingie nyumbani usiku. Kila mwanaume atakachoongea lazima mwanamke aseme ulikuwa kwa mahawara zako

silas maswe mbona umekuja na hukumu juu yangu? Siwezi wala sina haja ya kujitetea kwako sababu nayajua maisha yangu niliyoishi. Sikulazimishi unielewe wala kuniamini pia sababu hunijui
Wewe endelea kumtetea huyo unayejiona kumfahamu sanaaaa zaidi yangu ila ukumbuke mimi ndio nimeishi nae, mimi ndio mzazi mwenzie na hivi hapa ninalea wanae kwa roho safi kabisa
 
Kwaio mwanamke anafanya kazi lakini anaona uchungu kununua chakula chake, kulipa kodi yake mwenyewe, kununua mavazi yake mwenyewe? Sasa hio kazi unayoifanya ni ya kazi gani? Ila nimeona wanawake wa kiafrica wamelelewa katika namna ya kua watu tegemezi
 
Huyu hajielewi
 
Wewe punguani kweli wewe unazungumziaje dada zangu wasiokuepo? Haya mpeleke mamako mzazi naye ajaribu uone raha ili mfaidi vizuri
Punguza povu mbona mkali hivyo Kama umechomwa msumali wa makali.. i kama huyu aliye andika mada hii ni mkeo jirekebishe.
 
Kwaio mwanamke anafanya kazi lakini anaona uchungu kununua chakula chake, kulipa kodi yake mwenyewe, kununua mavazi yake mwenyewe? Sasa hio kazi unayoifanya ni ya kazi gani? Ila nimeona wanawake wa kiafrica wamelelewa katika namna ya kua watu tegemezi

Habari ya ulaya mkuu, nikuulize wewe unaishi na mke ndani unafanya kazi ya kudumu yeye ana kibarua cha kulipwa kwa wiki tena kinaisha muda wowote halafu yeye ndio analipa kodi, ananunua chakula, mavazi, anasomesha watoto........ Hebu ji assess kwanza.
Hivi sasa naishi mwenyewe lakini nimeweza kupunguza gharama....sihitaji nyumba nzima tena. Hata chumba na sebule tuu vinanitosha (nalala na wanangu) pesa nyingine inaenda kwenye mahitaji ya baadae ya watoto
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom