Ukiona mwanamke anaikataa ndoa jua yamemfika hapa!

Unadiriki kumuita mtu shetani bila kuusikiliza upande wake! Isije kuwa huyu kiherehere ndo mwenye mapungufu makubwa sana!

Mkuu naona umeyachukulia haya maneno kama nilivyoandika.
Nilichomaanisha ni kwamba, kwa huyu mama kusema mabaya/mapungufu ya mwenzake pasipo kusema ya kwake maana yake ni kwamba, yeye ni mwema zaidi (malaika) na mwenzake ndo mbaya (shetani). Kwa minajili hiyo, malaika hawezi kuishi na shetani.
 
Hilo la kutotunza watoto na familia hata Mimi namshangaa huyo mwanaume mwenzangu.
Lakini suala la kusema anakusaliti siwezi kukubaliana na wewe.!!
Kwani Kuna mahali mliandikiana kuwa hatagusa mwanamke mwingine?

Mwanamke mmoja hatoshi kwa mwanaume rijali.
Na mkishazaa Upendo wooote unahamia kwa watoto.

By the way, one sided story, yawezekana akaja kujibu.
Maana jf ya siku hizi Ni tit for tat
Kiapo cha ndoa cha ntakua mwaminifu unataka kusema umekisahau?
Ama kanisani huwa wanasemaje?.
Urijali huo vipi nyumbani tu hatoshelezi?.
 
Kwanza hamna ndoa ya mume singida mke mtwara. Hii sio asili ya ndoa. Lazima ife tu haina mbadala.

Pili hizi tabia zake za uchoyo kipindi cha uchumba hukunotice hata moja, ukimbie mapema?!

Halafu kwanini uliendelea kumshushia watoto wakati hali yako tia maji tia maji na yeye hatoi huduma za kueleweka.
Unaweza dhani ulikua sahihi sana lakini ukubali una nafasi uliyochangia katika yote yaliyokukuta, kipindi unaolewa sijui ulikua umeshakua desperate.

Ila hujatupatia funzo sisi ambao hatujaolewa au ambao wababa watarajiwa. Umetoa tu mada kama story. Wakati uko na experience nzuri ya maisha ya ndoa.

Mwisho nikupe pole kwa yote.
 
Pole sana ndugu.
Ila Kuna mambo mengine umechangia kwa kiasi fulani. Unaendeleaje kuzaa na mtu hana muelekeo?! Na naamini hizi dalili hazikuanza ndoani wakati wa uchumba hukuziona ama ndo Ile ya kuamini atabadilika mkishaoana?!
Ukitaka kujua uchungu wa maisha kosea kuoa ama kuolewa!
 
Mwanaume akiwa ahudumii usitoe hata kumi yako kama ni chakula cha watoto jikaze tu hiyo siku usinunue uone atawaacha wafe na njaa? Kama ni ada waache wakae nyumbani hata mwezi mzima uone ataacha kutoa ada? Asiponunua chakula na kulipa ada ni heri uondoke tena na watoto muachie
Hapana wewe huna utu mkuu huwezi ukashindana na mwanaume juu ya matumizi ya mtoto eti kisa mwanaume hasomeshi na wewe unawaacha eti tuone kama atawaacha wasisome uo ni ujinga anae umia ni mtoto.....
 
Mkuu Kingsmann umeamua kunichana dada yako LIVE dah
Kweli mwishoni wakati nafanya maamuzi ya kuachana na mimi niliona sikupendwa kwa kweli.... Mwanaume tena mume wa ndoa hawezi kuwa anakupenda halafu mahitaji ya familia yake unaenda kuombaomba asikokujua na wala haoni shida....
Historia kuna mtu kauliza nimemjibu tayari
Sijakuchana ila tunaambizana ukweli tuu dada angu kwani sote tu watu wazima, kuna vitu vingine huwa vinaonekana kwa ishara tuu sio mpk lazima ufanyiwe kwa vitendo.

Unforgetable
 
Habari za muda huu wakuu

Nimejiskia kushare historia yangu ya safari ya ndoa KWA UFUPI SANA wakuu ukiona mwanamke kachoka kavumilia mengi

Mimi ni mwanamke mwenye watoto3 niliolewa miaka14 iliyopita nkajaliwa watoto wa3.

Nimeishi kwenye ndoa ya mateso kwa miaka 12 hadi nilipoona inatoshaa na kuamua kukaa pembeni kujiepusha na malumbano.

Kwa kifupi tulipoingia kwenye ndoa na aliyekua mume wangu nikiwa naanza kazi wakati huo yeye alishafanya kazi sehemu tofautitofauti kwani hata kwa umri ni mkubwa kwangu amenipita miaka karibu 10

Tulipoana mwenzangu alikua anafanya kazi mbali na mimi (mikoa tofauti) na wakati huo mimi nilikua nafanya kazi ya mkataba mfupi. Tulikubaliana nisiache kazi hadi hapo nitakapopata kazi kule alipo.

Mungu mkubwa miezi miwili baada ya ndoa niliconcive nikaendelea na kazi hadi nilipojifungua.

Wakati nikiwa mjamzito nilianza kuhisi mwenzangu hajui majukumu yake kwani alikua anajua nilikua nalipwa kidogo sana tena nalipwa kwa wiki lakini hakuwahi kunisupport chochote kama mke iwe kodi, mavazi, au pesa ya kula.

Ikitokea amenipa pesa basi ujue labda laki1 au moja na nusu kwa miezi 6 tena baada ya kuomba sana na kulalamikiwa sana.

Mtoto wangu akiwa na miezi5 kazi yangu iliisha tukaamua niungane mwenzangu anakofanyia kazi. Tuliishi kwa amani, mwenzangu akiwa anaenda kazini Mimi nabaki nyumbani pia aliahidi kunitafutia kazi.

Basi wakati huo nikiwa mama wa nyumbani mtoto anaweza akawa anaumwa mwenzangu anaenda pharmacy ananunua dawa ananiambia nimpe yeye anaenda kazini.

Nilikuwa nabaki nyumbani nina chakula tuu ila senti tano sina. Kuna kipindi nilibaki na mtoto akazidiwa sina hata vocha ya kupiga sim.

Nilihisi kumpoteza mwanangu nikaomba wasamaria wema msaada mwanangu akatibiwa nikiahidi nitawalipa pesa zao. Jioni aliporudi mwenzaàngu nilimwambia alinyamaza nikampa namba za walionisaidia na kiasi walichonipa.

Hakuonyesha Kujali ila baada ya siku 2 aliwatafuta na kuwapa pesa yao. HAPO KENGELE ZA HOFU ZILIANZA KULIA KICHWANI NIKAONA ILI NIISHI MIMI NA MWANANGU LAZIMA NIFANYE KAZI.

Kama mwanamke yoyote nilimweshim sana mume wangu sikutaka kabisa kumuudhi nilikua naongea nae kwa busara kuhusu maisha na majukumu yetu kama wazazi ila hakuwahi kunipa majibu ya wasiwasi niliokua nao wala kuonyesha njia ya kupata suluhu. Niliumia na kuogopa sana na moyoni nilijua lazima nifanye kazi sana.

Basi nikampigia kaka yangu aliyekua ananitaftia vibarua, nikamwambia kaka huku sina kazi mwaka sasa,nikamwomba anitumie msg kuna kazi (japo haikuwepo) ili niweze kuomba nauli na kurudi sehemu ambayo ni kama nyumbani na ni rahisi hata kupata msaada

Nilirudi nikatafuta kazi nikapata na maisha yakaendelea.

Mwenzangu hakuwahi badilikaaa, kila kitu nilikua najifanyia mwenyewe, kodi, matibabu, kula, kuvaa na bills zote. Ikitokea amekuja basi ataweka laki mezani itatumika na kwisha kabla hata ya yeye kuondoka..lakini hasemi kitu achilia mbali mimi kumwambia nimekopa hapa na pale kujikimu. Kuna wakati niliomba wakubwa zake wamshauri lakini hakuna lililobadilika.

Miaka 5 baada ya ndoa nilikuja kugundua na wanawake kibao Kati yao akiwa girlfriend wake wa shuleni ambae alikua mke wa mtu ambae katika mawasliano yao ya email waliapa kutokuachana.NILIUMIA SANAAA NIKASEMA BASI NDOA STAKI TENA MAANA NATESEKA BILA SABABU ZA MSINGI.

Aliomba msamaha sikuweza kumsikiliza wazazi wakaanza kusuluhisha na baada ya kama miezi8 yaliisha tukaanza upya. Tuliishi hivyo siku zikawa zinasonga sikuskia tena habari za wanawake ila huduma ya familia haikuwepo bila ugomvi na ukitokea ametoa labda ada ya mtoto kama ni 1M atatoa laki4 na akishaoa hiyo chakula, matibabu, kodi, kuvaa sio juu yake🤗 uksema umjaribu kwa kumshauri kumhamishia mtoto shule za serikali anakataa

Miaka mi3 iliyopita hali ilizidi kuzorota, watoto 3 mzigo akanizidi, nikamwambia lazima kukaa na kujadili mstakabali wa familia hapo kwa Mara ya kwanza alinitukana na kuniambia sitakiwi kumsemesha chochote kwani kila ninachomwambia anakijua......nilishangaa nikasema majukumu tuu yanatufikisha hapa! Wacha ninyamaze.

Baada ya siku chache nikagundua kumbe ana wanawake wanamsumbua hata yule old girlfriend bado yuko nae

Hapa ndipo nilifanya maamuzi kwamba mimi na yeye basi. Tuna watoto wazuri na nawapenda sana nadhani hata yeye anawapenda japo siwezi kumsemea....

Sikuona sababu ya mimi kuendelea kuishi na mtu ambaye

1.Hanijali

2.Hanipi support yoyote na zaidi

3.Ananisaliti kitu ambacho ni hatari magonjwa haya mengi tusijeacha watoto kizembe

Aanakuja akiomba msamaha nimemsamehe kabisa lakini siwezi kurudiana nae

Nilichoka roho, akili na mwili hata akioa leo aoe tuu

Nilichoka kufanya majukumu ya mama na ya baba na kusalitiwa juu
Pole sana dada yangu! Hakika ni uamuzi mgumu but mzuri uliouchukua. Hakukuwa na ndoa hapo.
 
Tangu mmeanza uhusiano ilikuaje kwani? Au alibadilikia ndoani?!! Haya mambo ni ya kuyaangalia mapema sana mnapoanza uhusiano. Mtu hatoweza kuact kila siku utamjua tu.
 
Story tamu sana
Lakini hujajitambua. Ndoa haziko hivyo , mume ni mwenzi wako , hukumpa haki yake ulimwachai akiteseka , akaona isiwe tabu , mwisho karudi kwa mpenzi wa ujanani kupumua kidogo. Sasa usilalamike.shida ni wewe.
 
Back
Top Bottom