Ukiona mume na mke hawazungumzi ndani ya gari, elewa kuwa ni wanandoa

Endapo utawaona Mwanamume na Mwanamke wako ndani ya gari wawili tu wanaenda kazini mathalan. Au wanatembea kwa miguu pamoja na hakuna mazungumzo kati yao. Na ukiwaangalia nyuso zao hakuna mwenye furaha. Au bashasha, tabasamu. Elewa kuwa ni mume na mke (wanandoa) hao.

Na ukiona Mwanamume na Mwanamke wako ndani ya gari wawili tu wanaoenda kazini, au ukute wanatembea pamoja na kuna mazungumzo yenye kuashiria furaha, bashasha, tabasamu. Fahamu kuwa ni mpango kando. Si watu ambao wameoana yaani sio (wanandoa.)

Hapo unajiuliza ni kwanini furaha ikosekane kwa wanandoa, halafu ipatikane kwenye mpango kando? Yamkini kuna shida mahala si bure.

Nawasilisha
Na kama ni wanandoa ukiwaona wanacheka na kutabasamu ujue kuwa watakuwa wamempokea Yesu kama bwana na mwokozi wao...
 
Hahahaha Tafiti za humu bana ukiangalia kwa jicho moja ni kweli ukifumba macho si kweli ukiangalia kwa macho yote ni kweli si kweli.
 
mkuu umeambiwa wanandoa wantakiwa kuongea muda wote na kucheka cheka tu kwenye gari?

hujajiongeza labda wanasikiliza kitu muhimu kwenye redio..

wewe umekutana nao barabarani tena kwa bahati mbaya unajuaje kama walikuwa hawajacheka au kuongea ...
Au pengine tushaongea mengi tu home, au kabla ya kukutana na mtoa mada
 
Endapo utawaona mwanamume na mwanamke wako ndani ya gari wawili tu wanaenda kazini mathalan. Au wanatembea kwa miguu pamoja na hakuna mazungumzo kati yao. Na ukiwaangalia nyuso zao hakuna mwenye furaha. Au bashasha, tabasamu. Elewa kuwa ni mume na mke (wanandoa) hao.

Na ukiona mwanamume na mwanamke wako ndani ya gari wawili tu wanaoenda kazini, au ukute wanatembea pamoja na kuna mazungumzo yenye kuashiria furaha, bashasha, tabasamu. Fahamu kuwa ni mpango kando. Si watu ambao wameoana yaani sio (wanandoa.)

Hapo unajiuliza ni kwanini furaha ikosekane kwa wanandoa, halafu ipatikane kwenye mpango kando? Yamkini kuna shida mahala si bure.

Nawasilisha
Hii haina ukweli,Nikiwa na mke wangu tunaongea na kucheka bila shiida,Akianza kuleta stori zake za kuchekeshachekesha mimi nakuwa mchombezaji, zingine ananitaniatania basi tunacheka na kufurai maisha yanaenda, hakuna stress.
 
Tafiti huwa na uhalisia kwa % inawezakana wapo kwa sababu kuna nyumba zingine zina migogoro ya ndani kwa ndani mtu anaumia lakini kwa kuwa aliapa mpaka kifo kitengenishe hana jinsi na wengine kougopa aibu mbele ya jamii kwani watazikumbuka zile mbwembwe za ukumbini na hawataamini kama ndiye mhusika anafanya upuuzi,mfano watu wamenyimana chakula cha usiku unategemea asubuhi watashikana mikono,mtoa thread yupo sahihi nampa 75% kwa sababu migogoro ipo ktk ndoa.
 
Asante..!

Lazima kuwa shida hapo
 
Kumbe huyu niliyeoa sio mke wangu, aise nakutafuta unionyeshe alipo mke wangu
Ukoje muunganiko wako hapo mkiwa pamoja? Kama upo na mke wako na hakuna story za hapa na pale elewa kuwa kuna tatizo mahala.
 
Kwangu haiko hivyo mkuu. Fuatilia hata kwenye foleni za barabarani utaleta mwenyewe mrejesho.

Na pengine ukute kila mmoja anaamua kuchat na simu yake
Ninyi ndio vyanzo vya ajali kwenye foleni za magari, badala ya ku-concentrate kwenye udereva, unakuwa busy kutazama watu kwenye magari yao!!
 
Back
Top Bottom