Ukiona mtu anateua na kutengua mara kwa mara ujue yeye ndo mwenye tatizo

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,801
Je ni kweli wateule wake hawamuelewi?Anateua kila mara na anatengua kila mara. Kila sehemu anayofanya ziara anakuta uozo uko pale pale. Wengine wanasema uongozi wa Jazba, vitisho, mihemko na chama kushika hatamu kila mhimili ndio kikwazo kinachomwangusha. Wengine wanasema haambiliki na hashauriki. Mimi naona ajitathimini kwanza kabla ya kuendelea na hiring and firing he might be wrong somewhere.
 
Je ni kweli wateule wake hawamuelewi?Anateua kila mara na anatengua kila mara.Kila sehemu anayofanya ziara anakuta uozo uko pale pale. Wengine wanasema uongozi wa Jazba,vitisho, mihemko na chama kushika hatamu kila mhimili ndio kikwazo kinachomwangusha. Wengine wanasema haambiliki na hashauriki. Mi naona ajitathimini kwanza kabla ya kuendelea na hiring and firing he might be wrong somewhere.
Ukiona unaowaongoza hawakuelewi basi jitafakari,ama hawakuelewi kwa kuwa si waelewa ama hawakuelewi kwa kuwa hueleweki
 
Watanzania wenye uwezo wapo wengi,tutatengua tu,Magufuli si wa kwanza kutengua
 
Ukitunga mtihani darasa zima likafail basi jua tatizo hapipo kwenye kichwa cha hao wanafunzi tatizo lipo kwa mwalimu na saa nyingine hata yeye akitungiwa mtihani huo huo anaweza akafail pia.
 
Watanzania walizoea kuiba kwe kutumia vyeo vyao maofisi huku wakiwa ma mamgimeza. Kwenye hili Niko pamoja na JPM aendelee kuwafundisha adabu
 
Je ni kweli wateule wake hawamuelewi?Anateua kila mara na anatengua kila mara.Kila sehemu anayofanya ziara anakuta uozo uko pale pale. Wengine wanasema uongozi wa Jazba,vitisho, mihemko na chama kushika hatamu kila mhimili ndio kikwazo kinachomwangusha. Wengine wanasema haambiliki na hashauriki. Mi naona ajitathimini kwanza kabla ya kuendelea na hiring and firing he might be wrong somewhere.
Tutaelewana tu ngoja tuoneshane makali kidogo!! Hata mke ukimuoa ukiona hakufai unatengua na ndo mana kuna talaka!!
 
Ukiziba mianya ya watu kula pesa hamu ya kazi inaisha jpm hataki watu wamwibie na haongezi mishahara na mianya ya kula inazibwa kwa MTU mwenye kuzoea awamu zilizopita inakuwa shida kufanya Maxi
 
Kuna vdo nimeiona mitandaoni inamuonyesha mh. Akiwa rungwe akihitubia juu ya gari na baada ya muda mfupi ukazuka moshi flani hivi hadi akaacha kuhutubia na akasikika akisema wazee wa rungwe mmeleta mpaka moshi!" Ni kama palitokea sintofaham hivi vdo iliishia akionekana anarudi garini!

Sina uhakika na vdo ile kama ni editing au vp"

Mi ilinitisha. Kama ni ya kweli ama ni kishirikina au kidigitali zaidi kivovote vile itakuwa ni aina ya shambulio!
 
Hiyo uliyoona ilikuwa ni nusu ya tukio zima.

Ni kweli alipokuwa anahutubia moshi ulipita na kiusalama ilibidi rais arudi kwenye gari, ule moshi ulipita na akaendelea kuhutubia.

Alimaliza hotuba yake vizuri kabisa kama alivyopanga. Rais wetu ni mzima kabisa.
 
Lakini kukiwa na mapungufu, tunalalamika akiwaondoa tunalalamika.
Nchi ina watu zaidi ya milioni 45, sioni kwanini watu mkariri ni mtu mmoja tu anaweza. Nchi yetu sote, nisawa akiwapa wengine nafasi kutumika, hata ingekuwa kwa mwaka mmoja mmoja ili woote tupate nafasi kutumikua nchi yetu. Sioni tatizo tukijaribiwa wote, iko siku titamfahamu anayeweza na asiyeweza.

Wasipotumbuliwa wanajisahau, hivi anavyofanya ni sawa pia. Hata yeye anaweza kuwa hawezi, lakini hakuna wa kumtumbua isipokuwa wananchi kupitia kura.
Hakuna mfumo wa kupika watumishi siku zote ni hivi hivi, kwa kutujaribu kwenye majukumu tofauti tofauti.
 
Ukiona unaowaongoza hawakuelewi basi jitafakari,ama hawakuelewi kwa kuwa si waelewa ama hawakuelewi kwa kuwa hueleweki
Kwaakili ndongo kama wewe ni mwanaume ukaoa mke wa kwanza, ukamtimua, ukaoa wa pili ukamtimua ukaoa wa tatu hiv jamii itakuchukuliaje? Na maranyingi lawama hutoka kwa wake zako na kuhamia kwako. Ndo haya ya meko sasa
 
Je ni kweli wateule wake hawamuelewi?Anateua kila mara na anatengua kila mara.Kila sehemu anayofanya ziara anakuta uozo uko pale pale. Wengine wanasema uongozi wa Jazba,vitisho, mihemko na chama kushika hatamu kila mhimili ndio kikwazo kinachomwangusha. Wengine wanasema haambiliki na hashauriki. Mi naona ajitathimini kwanza kabla ya kuendelea na hiring and firing he might be wrong somewhere.
Tatizo ni mazoea ya wateuliwa kutowajibika kutokana na kasumba kwamba uongozi ni fursa ya kula na kupora Mali za umma. Nikupe mifano michache
1. Waziri mkuu ziarani Singida anakuta kitasa cha mlango wa bweni LA chuo ni cha sh 25,000 single lock. B.O.Q inaonesha ni triple lock cha 75,000. Hapo tatizo mteuzi au mteuliwa kushindwa kusimamia?.
2. Waziri ndalichako anakuta mlango wa bweni ni soft wood lakini B.O.Q INA hardwood, viongozi wa wilaya na mkoa wapo wanalipwa mishahara minono, posho na usafiri hawajabaini hilo.
3. Mheshimiwa JPM anakuta wakulima wa korosho Wamedhulumiwa na vyama vya ushirika, Takuluru wilaya na mkoa wapo na wanalipwa tu vizuri.
4. Nachingwea anakuta soko limefungwa na ujenzi hauendelei, stendi INA hali mbaya lakini DC na DED wapo.
Anapotengua nia ni kusukuma maendeleo mbele ili kutatua kero za wananchi. Kuna haja ya kukaza sheria ulu MTU akizembea sio tu atenguliwe Bali aitapike mishahara na posho alizopokea ktk cheo hicho.
Bila ukali katika nchi za dunia ya tatu, mambo hayaendi. JPM big up, teua-tengua tusonge mbele baba
 
"Sometimes to bring a change in a society you must have a level of madness"........capt Thomas Sankara former president of Burkina Faso
 
Back
Top Bottom