Ukiona mtu anashabikia sana Simba na Yanga kuwa naye makini, wengi hawana akili timamu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,204
12,700
Kwa uchunguzi mdogo niliofanya nimegundua kuwa watu wanazi sana wa hizi timu huwa hawako timamu kichwani.

Ukiona mtu muda wote au zaidi ya asilimia 70 ya maongezi yake ni Simba na Yanga. Muda mwingi anashinda amevaa jezi ya Yanga au Simba. Mitandaoni anafuatilia sana habari za Simba na Yanga. Mara Mukoko hivi, mara Manara vile, kuwa naye makini sana. Usimuamini kwa jambo la msingi. Huwa hawana mawazo ya maana. Hawana maongezi ya maana. Na mbaya zaidi wengi huonyesha dalili ya matatizo ya akili.

Jiepushe na watu wa namna hiyo.
 
Ni mapenzi tu kwa anachopenda mtu ,heri sisi wapenda soka na wenye mapenzi na hivi vilabu . Mtu anayeongelea soka ni afadhali kuliko wale wanaoongelea ngono mda wote ,ukikaa tu kidogo mtu lazima aanzishe mada ya ngono.
 
Nina ungana na wewe OP

Narudia, Nina ndoto ya kuziondoa/kuziua Simba na Yanga for the betterment of our sports industry hasa mpira wa miguu
hata ungekuwa na uwezo huwezi kuondoa Simba na Yanga ,na kuziondoa ndo unaua soka ,Simba na Yanga hata zishuke daraja la 3 bado ushabiki tutaendelea nao
 
Ni mapenzi tu kwa anachopenda mtu ,heri sisi wapenda soka na wenye mapenzi na hivi vilabu . Mtu anayeongelea soka ni afadhali kuliko wale wanaoongelea ngono mda wote ,ukikaa tu kidogo mtu lazima aanzishe mada ya ngono.
Tatizo mapenzi yenu kuna mda yanapitiliza had yakuwa ni yakuharibu badala ya kujenga.
 
Ni mapenzi tu kwa anachopenda mtu ,heri sisi wapenda soka na wenye mapenzi na hivi vilabu . Mtu anayeongelea soka ni afadhali kuliko wale wanaoongelea ngono mda wote ,ukikaa tu kidogo mtu lazima aanzishe mada ya ngono.
Kushabikia na kuongea kiasi siyo shida. Kuna wale ukimuona tu unajua hapa hatuna la maana la kuongea zaidi ya kumuongelea Kakolanya na habari za Mkude. Fuatilia vizuri, wengi wao siyo wazima kichwani.
 
Mkuu unatukosea sana.

Kitaalamu ili mtu "asiwe timamu na awe na matatizo ya akili" ni lazima aweze kuingia katika "CATEGORY" mbili zifuatazo:-

1)Delusions

2) Hallucinations

Je katika TAFITI yako ya hao "70%" wana SIFA HIZO?

Mkuu acha bana....ikiwa wewe HUPENDI MCHEZO WA MPIRA mathalani wa vilabu hivi viwili basi utakuwa UNA MAPENZI MAKUBWA NA VITU VINGINE....VINGINEVYO VISIVYOHUSU MPIRA WA MIGUU....je nawe ni "mgonjwa wa akili"?!!!

Endelea kukaa na mkeo mkipiga soga muda ambao sisi wengine tuko "Kwa Mkapa,mabanda umiza na mabishano ya DERBY YA K/KOO humu katika vijiwe vya kahawa na Al Kasus".

Ndimi Yanga Lialia.

#DaimaMbeleNyumaMwiko
#1935ForEver

YETZER-HA-TOV
 
Utakuwa umeifanyia nchi yako jambo kubwa sana.
Nafahamu hilo chief, Nilijaribu kuwagusia watu sehem fulani kuhusu hilo walinielewa sana tena sana tuu japo changamoto ya hoja ilikuwepo.

Naweza kuleta Uzi mzuri kuhusu Hili. If variables remain constant
hata ungekuwa na uwezo huwezi kuondoa Simba na Yanga ,na kuziondoa ndo unaua soka ,Simba na Yanga hata zishuke daraja la 3 bado ushabiki tutaendelea nao
Nimesema kuziua ama kuondoa sio kuzishusha daraja.
 
Kushabikia na kuongea kiasi siyo shida. Kuna wale ukimuona tu unajua hapa hatuna la maana la kuongea zaidi ya kumuongelea Kakolanya na habari za Mkude. Fuatilia vizuri, wengi wao siyo wazima kichwani.
Unalazimishaje maongezi uyapendayo wewe?!!!!

Tuongelee nini ?!!

Kutengeneza ROCKETS za kwenda mwezini?!! Khaaaa😲😲😲
 
Nafahamu hilo chief, Nilijaribu kuwagusia watu sehem fulani kuhusu hilo walinielewa sana tena sana tuu japo changamoto ya hoja ilikuwepo.

Naweza kuleta Uzi mzuri kuhusu Hili. If variables remain constant

Nimesema kuziua ama kuondoa sio kuzishusha daraja.
badala ya kuzikuza na kuziendeleza unawaza kuziua sasa hapo unafanya nini ,? Unaweza kusema zinaua mpira wa bongo kwa sababu ni Yanga tu na Simba sinajadiliwa ,ila hata Spain Barcelona na Real Madrid wametoka mbali na ligi ya Spain ipo juu,Zamalek na Ismail ,Mamelodi na Orlando Pirates, Uwe na mawazo ya kuboresha si kuharibu
 
Back
Top Bottom