Ukiona Mgombea Urais wa CCM hakubaliki ndani ya Chama huyo ndo anahitajika kwa wananchi.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,352
11,477
Kutokana na harakati za siasa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao kushika kasi. kuna jambo moja ambalo ningependa kuwakumbusha watanzania. Kama kuna Mgombea ambaye ndani ya CCM kwa serikali iliyopo madarakani hawamkubali, huyo ndiye anayepaswa kuwa Rais wa watanzania. tunajua Serikali nyingi barani AFrika zimekuwa na tabia ya kurithishana uongoz/utawala ili anapokuja Rais mpya awalinde wale waliotoka kwa uovu/mabaya waliyotenda.

hivyo katika hili hujitahidi sana kuweka watu ambao wataendana nao kuwalinda na pengine kuwafaidisha kwa namna fulani. tunaona jinsi ambavyo Serikali iliyopo inavyojarib sana kumtengeneza Bwana B.Membe ambaye kwa bahati mbaya kabisa huyu bwana amekataliwa na watanzania kabla hata hajaanza. Ningeweza tu kusema huyu ana bahati mbaya na mbaya zaidi hata hajui kuwa hana nyota au hana mng'aro wa kuwa rais wa tanzania.Membe ni mmoja ya wanasiasa wa hovyo hapa nchini ambao wamewahi kutokea katika nchi hii.

baada ya kuona Membe ameshindikana ikaonekana aandaliwe Bwana P.Pinda. huyu wanajaribu sana kumuuza lakini watanzania weng wameshaanza kumgundua ni mtu wa namna gani. kwa kuwa na Rais kama pinda ni kuendeleza aina ya Uongoz tuliyo nayo hivi sasa. Ni mtu asiyejua nini cha kufanya,asiye na nguvu, anayetegemea huruma za wananchi, asiye na msimamo, mnafiki na asiye na maamuz. tumemuona kwenye mambo mengi akikurupuka na wakati wmingine hata kutoa kaul zenye ukakasi.

ni aibu kubwa hata katika suala la Escrow tukisema hahusiki wakati kama waziri mkuu alipaswa kufatilia kwa makini sana mambo yanaendaje. Huyu atakuwa Rais ambaye mambo yakienda kombo atasema ameshauriwa vibaya. huyu watamdanganya sana maana hajui kufatilia, hana maamuzi na muoga. tusilogwe tena kupata rais wa namna hii.

tumeona baadhi ya viongoz wakiundiwa zengwe na kutafutiwa Makosa mbalimbali ili kuwachafua hii ndiyo inanipa Hari ya kusema huyu kama wana CCM waliopo madarakani hawataki awe madarakani ana kitu gan ambacho wao wanakiogopa? haitosh mwana CCM aje hapa na kusema flan fisadi...tutamwuliza alete ushahid na kama huyo mtu ni fisadi na yupo CCM basi chama chote ni cha kifisadi basi ni wakati wa kuchagua chama kingine.
hivyo zile propaganda nyepesi za kusema mgombea flan ni fisadi pasipo kuleta vielelezo hapa ni siasa mfu zisizo na mshiko ambazo vijana wa sasa wameshazitambua na hawapo tayari kukaririshwa maneno/nyimbo hizo. tunataka Rais ambaye anaweza kufanya maamuzi, akayasimamia pasipo kujali watu watamwonaje....hatutak Rais anayecheka cheka hata katika mambo ambayo ni serious au ambaye atalialia katika mambo yanayohitaj kufanyiwa maamuzi.

tunataka Rais ambaye atafanya maamuzi. tunajua kuna mtu CCM wanamwogopa kwa kujua kuwa atakapoingia madarakani wao watakuwa na wakati mgumu sana kwa kuwa huyu ataingia kwa nguvu ya uma, hatakuwa na mtu yeyote nyuma yake hivyo nguvu ya wananchi itampa uwezo wa kutenda mambo makubwa kwa wananch pasipo kujali wenzake wanatakaje..... nawashauri ndugu zangu kama mpo ndani ya CCM mpitisheni mgombea ambaye Serikali iliyopo madarakani haimtaki maana huyu atakuwa ni wa wananchi.
 
Mwizi.
 
Kikwete alikuwa na sifa zooote mnazompa Lowasa sasa,ikiwamo kufanya maamuzi magumu.
Lakini leo hii zile sifa zoote zimeyeyuka.
Kiukweli inawezekana kabisa"the most popular" akawa ni the worst!
Kukubaliki kwa wananchi kunaweza kutengenezwa kwa hila na uchu ila uwezo ukawa mdogo sana.
Mgombea yeyote asiye na uwezo wa kukemea rushwa hadharani atakuwa HATUFAI KABISA.
 
Sasa iweje richmond atake ikulu. Mwl. Nyerere angefufuka leo akasikia fisadi anataka ikulu angemchapa viboko vya makalio mfululizo mpaka monduli na akawe balozi wa nyumba kumi. NYANGULO.
 
Mwanachama yoyote wa ccm ni sawa na uchafu tu,nilisha apa kitambo sitamchagua mwanaccm yeyote.wao wagombane tu ata wavuane nguo.
 
Maneno ya Ole Sendekwa .." Rushwa pekee ndio inafanya mwenye macho asione...mwanamme akawa mwanamke" mwisho wa kunukuu..kama ukitaka mtu makini ..lazima akubali kuishi kwa kidogo anachopata kihalali
 
Sijawahi kumsikia LOWASA akikemea ufisadi.Kiongozi yeyote asiyeliona hili ni tatizo na kushindwa kulikemea hadharani HAFAI kupewa dhamana ya kuongoza nchi
 
Back
Top Bottom