Ukiona maisha yako ni magumu basi jua kuwa kuna Mtu amekuchezea (amekuroga)

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Habari zenu,

Waswahili husema wendawazu ni kufanya jambo ulilofeli awali kwa namna ileile lakini ukitegemea ushindi.

Watu wengi Afrika wana bidii ya kutafuta fedha au maisha lakini maisha yenyewe hawayaoni. Afrika wananchi hurogana ili tu kuipa furaha mioyo yao ya wivu.

Haijalishi umesoma au hujasoma, haijalishi umezaliwa mjini au kijijini.

Kama unaishi maisha yasiyo na furaha na magumu basi pigia tu mstari kuwa tayari umesharogwa na ukarogeka. Huu ndio ukweli ambao wengi hawaupendi kuusikia.

Hata maandishi matakatifu yamekiri kuwa kuna uchawi. So ukiona unapinga kuwa hakuna uchawi basi wewe ni kafiri.

Ukiona umevurugwa hujui nini chakufanya basi pigia mstari kuwa tayari umesharogwa.
 
Hakuna kurogwa. Miaka 5 hujapandishwa mshahara maisha yatakuwaje tambarare. Sasa ni mitano tena!!! Tutaimba kihutu.
Sasa si ndio uchawi wenyewe huo. Mtu anaamua tu kuwaroga watumishi wa umma. Mtu anajisikia tu asikuongezee mshahara.
Katika kila jambo jua nyuma yake kuna jambo limejificha.

How come 5 yrs with no salary increment?
 
NAONGELEA MADEMU, SIO MABINTI WALA WANAWAKE, NAONGELEA MADEMU TU

Mademu wabaya sana, wanashinda sana kwa waganga. Atakuroga umpende, ataenda kwa mganga mwingine kuroga uwe unampa hela, ataenda PEMBA kukutengeneza mama yake akutawale, yaani utarogwa hadi ukome.

Fikiria sasa kama umekuwa na mademu kumi hali yako ikoje?

Halafu wakimaliza kukuroga wanapeleka picha yako baharini wanaufukia huko.
 
Hivi nyongeza ya Tsh 10,000/ inaweza kukutoa stage gani ki maisha?
Fikiri tena ulichokiandika. Kumbuka hatuzungumzii kima cha chini cha mshahara hapa na si mwaka mmoja. Kumbuka mshahara unaendana na madaraja. Usifikiri madaraja ya kitoto.

Unajua mafao yako ya kustaafu yanaendena na cheo na mshahara wako wa mwisho? Kwa miaka 5 ni wangapi watapata haki pungufu mpaka kifo chao kutokana na kutoongezewa tu mishahara na kupandishwa madaraja. Unajua hawa watakufa lini? Adha yatakayoipata miaka yote hii ni utoto?!?
 
Sometimes hiyo ni njia ya kujipa moyo. Unakuta mtu ana dreams kubwa lakini hazifanyii kazi akitegemea maajabu.. Mfano mimi nilikuwa na ndugu yangu alipata pesa akafungua biashara kwa kutaka kuwakonga wabinti wenzake, duka kubwa frem kubwa ndani ina private ofisi, choo, kodi yake tu ni hatari. Nikamwambia hivi wewe unaanza biashara hii kodi mbona kubwa, jibu alilonipa sikurudia uliza. Kuendesha ile biashara cost ilikuwa kubwa sana kuliko mapato haikuchukua hata mwaka ikafa.

Maisha yake yakawa magumu, akaokoka, yeye ikawa ni kuomba tu Mungu amtendee miujiza. Hatafuti kazi waala hataki kuanzia chini na anadai karogwa. Yeye anaomba tu, ukimuona anakwambia flani ndiyo kaniroga kila mtu kuanzia ndugu, majirani, mwenye nyumba wake wote wachawi na ndiyo chanzo cha maisha magumu yake.

Sometimes failures zetu tunataka kuzibebesha watu. Maisha yake yalikuwa magumu hasa. Lakini mara zote ilikuwa anadai karogwa. aliuwa hafikirii huwezi kuwa kwa mwezi unaingiza kipato c halafu matumizi yako ni L ukategemea hutoanguka.

Ukifikria sana kuwa una maisha magumu kwasababu umerogwa, muda mwingi unakuwa unakosea. Una maisha magumu kwasababu huna connection, au hujajatafuta vya kutosha au umeridhika na maisha hayo magumu. Sikatai uchawi upo hata umetajwa kwenye vitabu vitakatifu ila watu wnautumia kama njia ya kujipa moyo kuwa wamefail kwasababu wamerogwa kama ambavyo vijana siku hizi tunajipa moyo kuwa kila kijana aliyefanikiwa anauza unga ila kujustify failures zetu.
 
Watanzania ni wanafiki sana. Wengi wanakwenda kwa waganga lakini hapa wanaandika hakuna uchawi au mtegemee Mungu wako.

Kuna wanaonasa kaka wa watu kwa uchawi mpaka wanaolewa. Lakini siku ya send off wanasema asante Yesu, like fuvu la kondoo aliloliacha pangoni au kwenye kaburi la mtoto mchanga halitaji.
 
Nimekusoma sana mleta mada. Kuna washenzi walinifunga, nilikwenda interview 5 zote ninapigwa chini kazi niliyosomea. Shost alinipeleka kwa mtaalamu, baada ya shughuli tu, nilipass interview.
Ndg, haya mambo yapo tena sana.

Na unaambiwa ukiona 'ntu' anatumia nguvu nyingi kukupinga ktk hayo mambo ujue ni walewale wanao kanyagia chini wenzaoooo.
 
Watanzania ni wanafiki sana. Wengi wanakwenda kwa waganga lakini hapa wanaandika hakuna uchawi au mtegemee Mungu wako.

Kuna wanaonasa kaka wa watu kwa uchawi mpaka wanaolewa. Lakini siku ya send off wanasema asante Yesu, like fuvu la kondoo aliloliacha pangoni au kwenye kaburi la mtoto mchanga halitaji.
umenena vyema mkuu umenena vyena sanaa
 
Back
Top Bottom