Ukiona maisha hayajakukalia sawa usiogope kutumia uongo kutimiza malengo yako

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
477
1,637
Kuna wakati katika maisha unapoona maji yamefikia shingoni usiogope kusema uongo ili kutimiza malengo yako ya sasa na baadae

Kwa dunia ya sasa mtu kukupa mtaji wa biashara ni ngumu sana hata kama ni mzazi wako, ndugu yako au watu wako wa karibu wengi watakupa stori kibao sijui hivi wala vile mara wee tulia tuu utapata kazi ,vitu kibao unahidiwa lakini hakuna kinachotekezwa mimi upande wangu ilivofika mahali nikaona mambo magumu nilichofanya nilitumia uwongo kama ifuatavyo

1. Cha kwanza nilidanganya ndugu zangu kuna kampuni ipo kigoma nimeitwa kwenye interview wanisapoti katika nauli hela ya kula kulala kwa siku tatu nilivyoupata mpunga nikauweka Tigo pesa kisha nikaenda kukaa kwa mshikaji wangu yupo mbagala siku nne ndo nikirudi dar

2. Cha pili niliwahi kudanganya ndugu zangu kuna shoti kozi flani ya computer nataka kusoma wakanichangia lakini ilikuwa ni fixii mpunga nikautia Tigo pesa

Baada ya muda kupita nikajaga kufungua duka la accessories za simu na umeme lakini hakuna ndugu anayejua kama nina hio biashara ambayo inanilipa kiasi fulani na hio ni siri yangu imebakia moyoni hakuna anaefahamu ila MUNGU anisamehe tuu na ndugu zangu popote walipo wanisamehe tuu lakini imebidi nifanye hivyo laa Sivyo maisha yangenishinda
 
Hata Ibrahim ,baba imani yalimshinda, akadanganya kuwa aliye naye ni dada yake. kumbe ni mke wake
mazingira ya kusalama yalimlazimisha kufanya hivo
 
Duuuh....

Yaani UONGO leo umekuwa ni kitu kizuri eti kwa Sababu ya changamoto za maisha?!!!🤣🤣🤣

Uongo una athari hasi ndani ya FAMILIA
Uongo una athari hasi kwa UTU WA MWANADAMU
Uongo una athari hasi Katika URAFIKI
Uongo una athari hasi NDOANI
Uongo una athari hasi MASHULENI
Uongo una athari hasi MAKAZINI
Uongo una athari hasi BIASHARANI
Uongo una athari hasi MABARABARANI
Uongo una athari hasi MAHOSPITALINI
Uongo una athari hasi kwa MAJIRANI
Uongo una athari hasi ndani ya NYUMBA ZA IBADA.

Hao wasiotaka kumsaidia kijana na ndugu yao ilihali wana UWEZO nao wanaongozwa na KUTOJIAMINI,KUTOPENDANA KIUKWELI,UMIMI CHOYO HUSUDA,WIVU na hata kujawa na UONGO MAISHANI MWAO....

Mkuu sawa kwa KUUCHAGUA UONGO ili UTOBOE ila kufanikiwa kwako hakutaondoa kuwa UONGO ni janga kwa MWANADAMU...na umejaa kwetu WAAFRIKA....
 
good boi, kwa jamii zetu hizi tunazoishi nazo wengi wako na mtazamo hasi... now fanya mishe zako kwa siri na usiwe muongo sana, hapo lazima utoboe.
 
Sio mbaya lakini tafuta hata mtu mmoja umshirikishe je ukipata tatizo nani atajua kuwa una mali sehemu au ndo utaacha ipotee tu.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom