Uchaguzi 2020 Ukiona kiongozi anaanza ku wa "blackmail" Wananchi ujue maji yamemfika shingoni

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Siku chache za nyuma nilimsikia mgombea wa urais wa CCM akiwaonya wapiga kura. Aliwaambia kwamba wasipomchagua mgombea wa CCM watakosa maendeleo. Pia alisema kwamba sababu iliyofanya eneo lao kukosa lami ni kutokana na wao kumchagua mbunge wa upinzani.

Kutokana na kauli hizo kuna mambo mawili nimejifunza. Kwanza, uwezo wake wa kufikiri ni hafifu. Pili, ni mtu asiyeaminika.

Kwa kuanza na sababu ya kwanza ni kwamba, huyu mtu anafikiri pesa ya serikali ni yake binafsi. Ana mawazo finyu mpaka anajisahau kwamba hata wanaowapigia kura wapinzani pia wanalipa kodi na wanastahili kuona matunda ya jasho lao.

Nimetaja pia kuwa huyu bwana ni mtu asiyeaminika. Hii ni kwasababu kauli zake zinapingana. Wakati mwingine utamsikia akisema maendeleo hayana chama halafu anajisahau na ku wa "blackmail" wapiga kura ili kuwashurutisha wawachague wagombea wa CCM.

Kwa tabia hizi mbili alizo nazo anakosa kabisa sifa za kuwa rais.
 
huyu mtu anafikiri pesa ya serikali ni yake binafsi. Ana mawazo finyu mpaka anajisahau kwamba hata wanaowapigia kura wapinzani pia wanalipa kodi na wanastahili kuona matunda ya jasho lao.
hii imekuwa ni falsafa ya ccm kwa muda mrefu sana. wanaamini nchi ni yao na hakuna wa kuwaambia kitu. Absolutely wrong . . . . Wanancjhi ni lazima waamshwe usingizini kwanza
 
Kama Magufuli na IQ yake ya chini hivi ameweza kuwa rais basi hata Piere Liquid anaweza kutuongoza.

FB_IMG_15985375054443066.jpg


Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Ni kauli za kishamba na aibu kujiapiza na kutishia wananchi.... mtajuta.....sitanii.....msema kweli....maendeleo hayana chama...Bunda hakuna taa.... Lami iliishia kwa Lugola...
 
Back
Top Bottom