Ukiona dalili hizi jua mahusiano yako yashakufa yanasubiri kuzikwa tuu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,697
Penzi ni makubaliano baina ya watu wawili walioamua kuacha kila kitu na kuwekana moyoni lakini sio mara zote unayempenda na wewe akupende swali linabaki utajuaje kama uliyenaye anakupenda, leo tupate nafasi ya kuangalia mambo matano(5) ambayo ukiyaona ujue wazi kuwa penzi lenu lipo rehani

1. Hakueshimu
Hata kwenye mafundisho ya dini mapenzi ni kuheshimiana ukiona upo kwenye penzi na mtu na hata hakupi heshima yako hata kidogo ndugu yangu upo kwenye mahusiano na mtu wa mtu kuwa makini pengine mpo wengi na mwingine mwenye malengo naye ndiye anayepewa hiyo heshima unayonyimwa wewe

2. Mawasiliano hafifu
Pengine amkai pamoja na huwa mnapigia simu mara kwa mara lakini unashangaa mwenzio kila ukimpigia yuko bize na ukaribu wa mawasiliano baina yenu umepungua sio kidogo sanaa yani kila saa mwenzio hayupo sehemu nzuri ya kuongea na simu mara ana kazi mara sijui sms hajaiona yupo ambaye anatumiwa text mpaka zinaisha na anapigiwa mpaka dakika zinaisha jiongeze

3. Hafurahii Tendo
Kama hakupi kabisa au akikupa ndo kishingo upande basi kaa ujua kabisa yupo anayepewa mpaka ambavyo wewe hata nusu hufiki tendo ndo msingi wa penzi ukiona mwenzi wako hana raha tena ya kushiriki kitendo hiki kilichobarikiwa na wewe upo uwezekano mkubwa kabisa kuwa asali yako wanalina na wengine

4. Anakuendesha
Yaani kila anachokitaka yeye ni sawa na hakuna mabadiliko kila anachokisema yeye ni sahihi hapo ipo shida maan anayekupenda kweli hawezi kukufanya mjinga na kukuamlisha kila anachotaka yeye Jipange kutafuta mpenzi
 
Penzi ni makubaliano baina ya watu wawili walioamua kuacha kila kitu na kuwekana moyoni lakini sio mara zote unayempenda na wewe akupende swali linabaki utajuaje kama uliyenaye anakupenda, leo tupate nafasi ya kuangalia mambo matano(5) ambayo ukiyaona ujue wazi kuwa penzi lenu lipo rehani
Kwa kuongezea tuu kuna dalili 4 muhimu

1. Mpenzi wako anakuwa na hasira za mara kwa mara na wewe kitu kidogo tuu ukikosea unashangaa ugomvi

2. Mpenzi wako anageuka mkosoaji wa kila jambo unalolifanya yaani chochote utakachokifanya kwake anakukosoa

3. Mpenzi wako anataka uwe unaanza kuzungumza point mnapoongea au anataka kujua leo una jipya gani kama hauna jipya basi anakuaga

4. Mpenzi wako anaacha kukuita yale majina kimahaba kama my love, sweat,mpenzi anaanza kukuita majina yako kama vile fred, ashura

5. Mara nyingi wewe ndio unakuwa kinara wa kuomba msamaha hata umegundua wewe huna makosa yeye ndo ana makosa ila wewe unaomba msamaha ili mradi yaishe tuu
 
Penzi ni makubaliano baina ya watu wawili walioamua kuacha kila kitu na kuwekana moyoni lakini sio mara zote unayempenda na wewe akupende swali linabaki utajuaje kama uliyenaye anakupenda, leo tupate nafasi ya kuangalia mambo matano(5) ambayo ukiyaona ujue wazi kuwa penzi lenu lipo rehani

Kwakweli😃😃😃😃
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom