Ukioa Kilimanjaro unakuwa ni sawa na umeolewa wewe, kila mwisho wa mwaka unatakiwa kwenda Moshi sherehe za mwisho wa mwaka

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Mwanaume ukioa Moshi/Kilimanjaro unakua tu ni sawa umeolewa maana kila mwisho wa mwaka wakwe na mashemeji wanaporudi kwao kwa ajili ya sikukuu na wewe utakua unalazimishwa kwenda.

Nina ndugu zangu 4 wameoa Kilimanjaro, wafanyakazi wenzangu na marafiki zangu na watu wengine ninaowafahamu ambao sio wenyeji wa Kilimanjaro ila kila inapofika mwisho wa mwaka lazima waende huko.

Hata Pascal Mayala amesema yeye kila mwisho wa mwaka huenda Moshi wakati ni Msukuma wa Kanda ya Ziwa.

Ukioa Moshi ni kama umeolewa wewe maana utapelekeshwa kama mbuzi.

Anyway, haya ni maoni yangu na mtazamo wangu, sio lazima uyapende.
 
Hahahaaa Hakimu Mfawidhi hakuna anayelazimishwa bhana. Ni mapenzi tuu kwenye ule utaratibu wa kusherekea kumaliza mwaka unawavutia wengi.
Halafu wanaoenda sio walioowa huko tuu, hata marafiki wanaenda kwa marafiki zao wa mkoa huo kwaajili ya kufurahia tuu. Hata wewe ukienda na Pascal Mayalla Mara moja unatamani kwenda kila mwakamwaka,,,, Kale kautaratibu ni kazuri na kakuigwa
 
Ukienda lazima mashemeji uwazungushie bia za kuonyesha kuweka heshima na kumjengea mkeo heshima kwa kaka zake
FB_IMG_1577123456440.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kwenda ukweni ni kosa kubwa namna hiyo?? Sasa ka sisi tuliooa kule West Lake tena Ngara tutakaa tufike huko kweli?? Nikipiga hesabu ya mafuta ya gari na misukosuko ya tochi hadi nifike naona nitazeekea njiani. Hivyo huwa nawaalika kuja kukaa kwangu miezi 2 . Wakwe na mashemeji 4 na wake zao. Hiyo gharama nadhani waweza jenga nyumba ningine. Sasa hapo aliyeolewa ni huyo anayeenda kwa wakwe au mimi ninayewaleta darisalama?
 
Back
Top Bottom