Ukiniuliza nani ungependa awe Rais wa Tanzania

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Nitakujibu ni Dr. John Pombe Magufuli, pamoja na ushabiki wangu ndani ya Ukawa lakini nimeshindwa kuushawishi moyo wangu uweze kukubali kuwa kuna kiongozi zaidi ya Magufuli anaweza kuliongoza vema Taifa hili

Kwa mara ya kwanza nitapiga kura ya Urais kwenda CCM iwapo huyu ndiye atakayekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Kwanini Magufuli, ni mtendaji na msimamizi nzuri ambaye hana wa kumfananisha naye kwa ubora wake wakati fulani nikiwa mfanyakazi ktk halmashauri fulani nilishuhudia jinsi fedha za RF zilivyokuwa zinaogopwa.

Kama binadamu Magufuli ana mapungufu yake lakini ubora wa Magufuli na umuhimu wake kwa nchi hii unazidi mapungufu aliyo nayo, Kila la heri Magufuli.
 
Kumpata mtu safi ccm ni kazi ngumu kama kutafuta maji ya chemchemi dodoma sema tu tunawalinganisha kwa uozo wao kwa mfano magufuli na lowasa mbele ya umma ni rahisi zaidi kumsafisha magufuli kuliko lowasa
 
Magufuli si Mtu wa kusafisha, kwani anakashifa gani?. Kusema ukweli kama Raisi atatokea CCM, basi Raisi Bora ni JOHN POMBE MAGUFULI PEKE YAKE. Hakuna Waziri ndani ya Serikali ya CCM anaye mzidi Magufuli.

Magufuli, Aliselema, Alija.

Angalia kwanza jinsi alivyotangaza nia, alivyochukua form, anavyo kusanya saini za uungwaji mkono, Hajafanya mbwembwe zozote kama wengine. Lakini tu mie nitashauri kama Magufuli hatatendewa haki kwenye NEC yao, kwanini UKAWA tusimshawishi na ashawishike kung'oka CCM tumpe nchi? Atashinda zaidi ya 75% au zaidi Ndani ya UKAWA.

Hayo ni maoni yangu lakini.
 
magufuli mwizi tu.....hakuna sehemu penye uwizi kama ujenzi
 
Mm kiukweli toka moyoni wala c mnafiki bhana mm n TEAM LOWASSA hakuna atakayenishauri nimtenge huyu ndugu
 
Mtu yeyote anayeshabikıa Edo, ajue fika anavutwa na uchawi wa wa Nıgeria na DRC na sıo bure.Amerogwa na akarogeka huyo.
 
Magufuli si Mtu wa kusafisha, kwani anakashifa gani?. Kusema ukweli kama Raisi atatokea CCM, basi Raisi Bora ni JOHN POMBE MAGUFULI PEKE YAKE. Hakuna Waziri ndani ya Serikali ya CCM anaye mzidi Magufuli.

Magufuli, Aliselema, Alija.

Angalia kwanza jinsi alivyotangaza nia, alivyochukua form, anavyo kusanya saini za uungwaji mkono, Hajafanya mbwembwe zozote kama wengine. Lakini tu mie nitashauri kama Magufuli hatatendewa haki kwenye NEC yao, kwanini UKAWA tusimshawishi na ashawishike kung'oka CCM tumpe nchi? Atashinda zaidi ya 75% au zaidi Ndani ya UKAWA.

Hayo ni maoni yangu lakini.

Mkuu kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa huoni alafu kingne usiseme aje ukawa kwan ukawa wao kuhangaika miaka yote mpaka leo wategemee mgombea ataye toka ccm haiwezekani
 
Nitakujibu ni Dr. John Pombe Magufuli, pamoja na ushabiki wangu ndani ya Ukawa lakini nimeshindwa kuushawishi moyo wangu uweze kukubali kuwa kuna kiongozi zaidi ya Magufuli anaweza kuliongoza vema Taifa hili

Kwa mara ya kwanza nitapiga kura ya Urais kwenda CCM iwapo huyu ndiye atakayekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Kwanini Magufuli, ni mtendaji na msimamizi nzuri ambaye hana wa kumfananisha naye kwa ubora wake wakati fulani nikiwa mfanyakazi ktk halmashauri fulani nilishuhudia jinsi fedha za RF zilivyokuwa zinaogopwa.

Kama binadamu Magufuli ana mapungufu yake lakini ubora wa Magufuli na umuhimu wake kwa nchi hii unazidi mapungufu aliyo nayo, Kila la heri Magufuli.

Chama ni taasisis inayoongozwa na watu wengi kitu ambacho ccm kwa sasa karibu woote wanaogombea au wasiogombea kila mmoja ana lizigo lake la ufisadi sasa huyo unayemsema hata akichaguliwa ataiendeshaje nchi wakati wanaomzunguka ndio hao hao tusiowahitaji? Na ndio maana nasema ndani ya CCM hata ashuke malaika mweupe kama theluji atatoka akiwa kama mkaa.
 
Magufuli hadi kufikia hatua ya watu kumtaka awe rais ni sifa yake ya uchapaji kazi wake kila mtu anajua suala hilo. Sasa mie naona tungetizama sifa za Dr.Slaa na Mh.Magufuli tuone ni nani mwenye sifa zenye kufaa kuweza kuwa rais.

Maana sie wengine hatuna vyama vya kushabikia na ukiangalia humu kumejaa ushabiki wa vyama tu.
 
Nilisikia makandarasi wanamsaidia Magufuli kukusanya saizi zinazohitajika kwa ajili ya mchakato, hilo pekee linaonyesha jinsi anavyotumia ofisi yake kujinufaisha na ndoto zake.
Malipo ya zaidi ya bilioni 200 kwa makandarasi wasioeleweka au hewa aliyosemaga mkuu wa ACT-Wazalendo ni wizara yake ilihusika
 
Yani mimi ndo bado sjaona nimpgie nani iwe ccm au ukawa naona kama wote ni siasa tu sdhan kama kuna mchapakaz
 
Nitakujibu ni Dr. John Pombe Magufuli, pamoja na ushabiki wangu ndani ya Ukawa lakini nimeshindwa kuushawishi moyo wangu uweze kukubali kuwa kuna kiongozi zaidi ya Magufuli anaweza kuliongoza vema Taifa hili

Kwa mara ya kwanza nitapiga kura ya Urais kwenda CCM iwapo huyu ndiye atakayekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Kwanini Magufuli, ni mtendaji na msimamizi nzuri ambaye hana wa kumfananisha naye kwa ubora wake wakati fulani nikiwa mfanyakazi ktk halmashauri fulani nilishuhudia jinsi fedha za RF zilivyokuwa zinaogopwa.

Kama binadamu Magufuli ana mapungufu yake lakini ubora wa Magufuli na umuhimu wake kwa nchi hii unazidi mapungufu aliyo nayo, Kila la heri Magufuli.

Magufuli amalize Ujenzi wa Barabara ya kilwa road ndiyo aombe Urais !! HANA SIFA YA KUWA RAIS LABDA DIWANI....!!
 
Ningepewa nafasi ya kuteua haraka ningemteua Lipumba awe raisi na mbatia awe msaidizi wake ama waziri mkuu
 
Mkuu kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa huoni alafu kingne usiseme aje ukawa kwan ukawa wao kuhangaika miaka yote mpaka leo wategemee mgombea ataye toka ccm haiwezekani
Ni heri huyu kawauzia nyumba Watanzania wenyewe kuliko wengine tunaowataka
ambao wana sifa ya kuiuza Tanzania kwa Wageni.
 
Chama ni taasisis inayoongozwa na watu wengi kitu ambacho ccm kwa sasa karibu woote wanaogombea au wasiogombea kila mmoja ana lizigo lake la ufisadi sasa huyo unayemsema hata akichaguliwa ataiendeshaje nchi wakati wanaomzunguka ndio hao hao tusiowahitaji? Na ndio maana nasema ndani ya CCM hata ashuke malaika mweupe kama theluji atatoka akiwa kama mkaa.
Unafikiri hata huko nje ya CCM kuko salama kihivyo, kinachotakiwa ni
kiongozi jasiri anayeweza kusimamia na kuhakikisha Nidhamu ya nchi inazingatiwa
 
Magufuli hadi kufikia hatua ya watu kumtaka awe rais ni sifa yake ya uchapaji kazi wake kila mtu anajua suala hilo. Sasa mie naona tungetizama sifa za Dr.Slaa na Mh.Magufuli tuone ni nani mwenye sifa zenye kufaa kuweza kuwa rais.

Maana sie wengine hatuna vyama vya kushabikia na ukiangalia humu kumejaa ushabiki wa vyama tu.
Mkuu mimi ni Mwanachama wa CHADEMA nimeweka ushabiki kando.
 
Nitakujibu ni Dr. John Pombe Magufuli, pamoja na ushabiki wangu ndani ya Ukawa lakini nimeshindwa kuushawishi moyo wangu uweze kukubali kuwa kuna kiongozi zaidi ya Magufuli anaweza kuliongoza vema Taifa hili

Kwa mara ya kwanza nitapiga kura ya Urais kwenda CCM iwapo huyu ndiye atakayekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Kwanini Magufuli, ni mtendaji na msimamizi nzuri ambaye hana wa kumfananisha naye kwa ubora wake wakati fulani nikiwa mfanyakazi ktk halmashauri fulani nilishuhudia jinsi fedha za RF zilivyokuwa zinaogopwa.

Kama binadamu Magufuli ana mapungufu yake lakini ubora wa Magufuli na umuhimu wake kwa nchi hii unazidi mapungufu aliyo nayo, Kila la heri Magufuli.
Uligawiwa nyumba mini? Mbona husemi kuhusu kashfa ya meli ya kigamboni kwenda bagamoyo?
Mbona huongelei kashfa ya nyumba za serikali?
Mbona hutukumbushi kauli ya kama huwezi kulipa feri piga mbizi?
 
Back
Top Bottom