Ukimya Wetu Watanzania ndio unaotuponza katika suala la Tozo na Katiba Mpya

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
1,727
3,286
Nawasalimu Wakuu,

Nianze pasipo kupoteza Muda.

Kauli ya Serikali ya kusema kua Watanzania wamekubali Tozo haina tofauti hata kidogo na ile kauli yao waliyo toa wakisema Watanzania hawataki katiba mpya wakisema kipaumbele chao ni Maendeleo.

Ifikie hatua tuseme kua tunaburuzwa sana kwa ukimya wetu huu na uhakika wataanzania wengi hawakubaliani na TOZO hizi hata kwa Mapunguzo yanayoendelea kuwekwa,hivohivo katika swala la Katiba Mpya Watanzania wengi sidhani kama wanakubaliana na Katiba iliopo. Ila kwa kua Viongozi wetu wametuona Bongolala wanatoa tu matamuko kua watanzania wamesema hivi hata kama hatujaulizwa, tunalishwa Maneno kila uchwao.

Ukweli ni kuwa ukimya Wetu unatuponza sana na utaendelea kutuponza sana sisi Watanzania, tubadilike tuseme isiwe tu upinzani ndio wasemee kila kitu.

Ikumbukwe kua Tukisubiri wanasiasa waliopo Madarakani watusemee itakua tunajipiga jenga wenyewe kwa sababu wote ni wa chama kimoja.
 
Kweli tupu.
 
Huu uzi umesuswa hata na wafia upinzani wenyew kwa sababu mleta mada umeandika upuuzi sana. Hili ni funzo kuwa sio kila muandika utumbo kuhusu serikali, au msifia upinzani atapata watu wakumuunga mkono hapa jukwaani. Kama unajiona una uchungu sana wa kupigania katiba mpya kuliko viongozi wa upinzani ambao wanapokea mamilioni ya hela kila mwezi kama vile mch Msigwa, Sugu na wengineo wapo kimya majumbani mwao na familia zao ingia barabarani ukaidai hiyo katiba peke yako. Kuna mambo mengi ya kuandika hapa Jf na ukapata wachangiaji chungumzima. Sio lazima kila mtu alazimishe kuandika habar za siasa.
 
Huu uzi umesuswa hata na wafia upinzani wenyew kwa sababu mleta mada umeandika upuuzi sana. Hili ni funzo kuwa sio kila muandika utumbo kuhusu serikali, au msifia upinzani atapata watu wakumuunga mkono hapa jukwaani.
Siyo kweli. Sema tu hivi sasa kuna mengi yaliyochukua uzito wa juu. Mleta uzi kajenga hoja vizuri tu mbona. Na kusema kweli uwoga na ukimya wa watanzania ndio chanzo cha matatizo yetu yooote kama taifa.
 
Nawasalimu Wakuu,

Nianze pasipo kupoteza Muda.

Kauli ya Serikali ya kusema kua Watanzania wamekubali Tozo haina tofauti hata kidogo na ile kauli yao waliyo toa wakisema Watanzania hawataki katiba mpya wakisema kipaumbele chao ni Maendeleo.

Ifikie hatua tuseme kua tunaburuzwa sana kwa ukimya wetu huu na uhakika wataanzania wengi hawakubaliani na TOZO hizi hata kwa Mapunguzo yanayoendelea kuwekwa,hivohivo katika swala la Katiba Mpya Watanzania wengi sidhani kama wanakubaliana na Katiba iliopo. Ila kwa kua Viongozi wetu wametuona Bongolala wanatoa tu matamuko kua watanzania wamesema hivi hata kama hatujaulizwa, tunalishwa Maneno kila uchwao.

Ukweli ni kuwa ukimya Wetu unatuponza sana na utaendelea kutuponza sana sisi Watanzania, tubadilike tuseme isiwe tu upinzani ndio wasemee kila kitu.

Ikumbukwe kua Tukisubiri wanasiasa waliopo Madarakani watusemee itakua tunajipiga jenga wenyewe kwa sababu wote ni wa chama kimoja.
Mimi naamini jinsi tunavyoteswa na serikali, ndio tutabadilika hatimaye. Historia inasema haiwezekani Watanzania wooote tuwe kondoo miaka yooote.
 
Siyo kweli. Sema tu hivi sasa kuna mengi yaliyochukua uzito wa juu. Mleta uzi kajenga hoja vizuri tu mbona. Na kusema kweli uwoga na ukimya wa watanzania ndio chanzo cha matatizo yetu yooote kama taifa.
Kwahiyo serikali iache kuleta maendeleo kwa wananchi wake kama vile kujenga shule, hospital, barabara, miundo mbinu ya maji, umeme na upatikanaji wake, ijikite katika kutengeneza katiba mpya ambayo kesho Mungine akiingia kitini atakuja kuibadilisha na kuweka ya kwake mfano wa ile ya vyama vya upinzani ambayo inamruhusu mwenyekiti akae madarakani kwa muda usiojulikana. Mshaambiwa katiba sio msahafu kila mtu anaweza kuingia akatengeneza genge lake la kuibadili kama walivyobadili za vyama vyao. Nashauri serikali ipambane kuleta maendeleo na unafuu wa maisha kwa wananchi wake, haya mambo ya katiba yanataka kutumiwa kama uchochoro na viongozi wa upinzani kupiga hela katika vikao vya katiba.
 
Well Said👏
 
Nawasalimu Wakuu,

Nianze pasipo kupoteza Muda.

Kauli ya Serikali ya kusema kua Watanzania wamekubali Tozo haina tofauti hata kidogo na ile kauli yao waliyo toa wakisema Watanzania hawataki katiba mpya wakisema kipaumbele chao ni Maendeleo.

Ifikie hatua tuseme kua tunaburuzwa sana kwa ukimya wetu huu na uhakika wataanzania wengi hawakubaliani na TOZO hizi hata kwa Mapunguzo yanayoendelea kuwekwa,hivohivo katika swala la Katiba Mpya Watanzania wengi sidhani kama wanakubaliana na Katiba iliopo. Ila kwa kua Viongozi wetu wametuona Bongolala wanatoa tu matamuko kua watanzania wamesema hivi hata kama hatujaulizwa, tunalishwa Maneno kila uchwao.

Ukweli ni kuwa ukimya Wetu unatuponza sana na utaendelea kutuponza sana sisi Watanzania, tubadilike tuseme isiwe tu upinzani ndio wasemee kila kitu.

Ikumbukwe kua Tukisubiri wanasiasa waliopo Madarakani watusemee itakua tunajipiga jenga wenyewe kwa sababu wote ni wa chama kimoja.
Mimi binafsi naunga mkono tozo zote
 
watanzania wakisha kuwa wanakula na kunya basi umewamaliza. Kwa umaskini wetu mtu akishakuwa na uhakika wa kula milo kitatu anajiita tajiri na mambo mengine usimuulize tena
 
Watanzania wa leo ni mapimbi👇

Ukipitia humu jukwaani kusoma threads mbalimbali utashangaa sana.Kwa mfano watu wanalalamikia bunge ambalo halina kibali cha wananchi kupitisha sheria za ovyo,watu wanamlalamikia Rais ambae hana kibali cha wananchi kuwa hana uwezo.

Watu wanamshangaa IGP kuwa mbovu wakati wanajua kuwa ametokana na serikali mbovu.Watu wanafurahi tozo kupunguzwa wakati hakuna anaetaka tozo,watu wanashangaa Polisi kufanya mambo ya hovyo wakati wanajua kabisa kuwa hao Polisi wametokana na mfumo wa hovyo na kadhalika.Ni vituko!
605758310.jpg
 
View attachment 1921361
Nchi hii mbovu san Mkuu Mbovu
 
Kwahiyo serikali iache kuleta maendeleo kwa wananchi wake kama vile kujenga shule, hospital, barabara, miundo mbinu ya maji, umeme na upatikanaji wake, ijikite katika kutengeneza katiba mpya ambayo kesho Mungine akiingia kitini atakuja kuibadilisha na kuweka ya kwake mfano wa ile ya vyama vya upinzani ambayo inamruhusu mwenyekiti akae madarakani kwa muda usiojulikana. Mshaambiwa katiba sio msahafu kila mtu anaweza kuingia akatengeneza genge lake la kuibadili kama walivyobadili za vyama vyao. Nashauri serikali ipambane kuleta maendeleo na unafuu wa maisha kwa wananchi wake, haya mambo ya katiba yanataka kutumiwa kama uchochoro na viongozi wa upinzani kupiga hela katika vikao vya katiba.
Kama maendeleo ndio hayo, basi kina Mandela hawakuwa na sababu ya kupambana na makaburu. Maana hakuna serikali yoyote katika Afrika nzima ambayo inasogelea yale yaliyofanywa na makaburu katika kujenga miundo mbinu.
Suala la Katiba mpya Mbona linaelezwa vizuri sana na Bashiru Ali enzi alipokuwa na akili zake timamu, kabla hajarukwa akili alipokabidhiwa cheo ccm. Ukiibgia ccm tu akili hizooooo bai bai. Wewe pia ukiachana na kutetea serikali hii ya ccm, utajishangaa. Huyu hapa Bashiru:
 
Nawasalimu Wakuu,

Nianze pasipo kupoteza Muda.

Kauli ya Serikali ya kusema kua Watanzania wamekubali Tozo haina tofauti hata kidogo na ile kauli yao waliyo toa wakisema Watanzania hawataki katiba mpya wakisema kipaumbele chao ni Maendeleo.

Ifikie hatua tuseme kua tunaburuzwa sana kwa ukimya wetu huu na uhakika wataanzania wengi hawakubaliani na TOZO hizi hata kwa Mapunguzo yanayoendelea kuwekwa,hivohivo katika swala la Katiba Mpya Watanzania wengi sidhani kama wanakubaliana na Katiba iliopo. Ila kwa kua Viongozi wetu wametuona Bongolala wanatoa tu matamuko kua watanzania wamesema hivi hata kama hatujaulizwa, tunalishwa Maneno kila uchwao.

Ukweli ni kuwa ukimya Wetu unatuponza sana na utaendelea kutuponza sana sisi Watanzania, tubadilike tuseme isiwe tu upinzani ndio wasemee kila kitu.

Ikumbukwe kua Tukisubiri wanasiasa waliopo Madarakani watusemee itakua tunajipiga jenga wenyewe kwa sababu wote ni wa chama kimoja.
wanatudharau sn, ukihoji unapigwa uhujumu uchumi
 
Watu wakimya siku kikijafyatuka hapatakalika kwa yeyote!
 
Kama maendeleo ndio hayo, basi kina Mandela hawakuwa na sababu ya kupambana na makaburu. Maana hakuna serikali yoyote katika Afrika nzima ambayo inasogelea yale yaliyofanywa na makaburu katika kujenga miundo mbinu.
Suala la Katiba mpya Mbona linaelezwa vizuri sana na Bashiru Ali enzi alipokuwa na akili zake timamu, kabla hajarukwa akili alipokabidhiwa cheo ccm. Ukiibgia ccm tu akili hizooooo bai bai. Wewe pia ukiachana na kutetea serikali hii ya ccm, utajishangaa. Huyu hapa Bashiru:
Tatizo la Tanzania vijana wengi ukiwemo ww mwenyew elimu zenu zimeshindwa kuwasaidia kuchanganua mambo ya msingi sababu ya siasa. Cha kusikitisha hao waliowafanya mshindwe kuchanganua mambo sababu ya siasa uchwara kama vile kina Mbowe, Lisu, Lema nk watoto wao wanasoma na kukaa mbali sana na siasa kwa ajili ya faida zao na vizazi vyao. Kwani washagundua kwamba ukiendekeza au kuingiza siasa katika kila jambo la msingi basi kuna nafasi kubwa ya kuharibikiwa katika maisha na elimu yao itakuwa haina maana tena kwao. Ebu fikiria mtu mwenye elimu yako unatoaje mfano wa kipuuzi hivi bila kuishirikisha akili yako vizuri? Makaburu walitoka ulaya kuja kuiba, kubagua na kutawala wenyeji. Lakini serikali ya Tanzania inatokea Tanzania na inaongozwa na Watanzania halisi. Makaburu (kama wageni) waliwabagua weusi (wenyeji) wasifanye kazi katika serikali na ofisi za umma kwa sababu ya rangi zao. Tanzania watu wanafanya kazi katika mashirika mbali mbali ya serikali na kibinafsi bila kujali vyama vyao, rangi zao, dini zao na jinsia zao ilimradi tu uwe na vigezo vya utanzania, elimu au uzoefu. Makaburu hawakutaka weusi (wenyeji) wafike mjini au sehemu wanazoishi weupe bila kibali maalumu. Tanzania mtu yoyote, wa chama, dini, jinsia au rangi yoyote yupo free kuishi mahali popote bila bughudha yoyote. Makaburu hawakujenga, shule, barabara wala miundo mbinu mizuri sehem waliyoishi watu weusi. Sisi huku raisi anataka kusambaza umeme, maji, barabara, shule na hospital nchi nzima ili iwe rahisi watanzania kuzipata huduma hizo karibu na maeneo yao na kwa haraka zaidi. So ni ujinga kufananisha yaliyotokea kaburu na yanayoendelea Tanzania kwani kuna utofauti mkubwa mno. Swala la katiba linataka kutumiwa na wapinzani kama kichochoro cha kupiga hela katika vikao vya katiba na kuvimbisha account zao kwa ajili ya future za watoto wao na familia zao, huku huduma za maji, umeme, barabara, hospital nk zikiwa zimekufa kwa sababu ya kuelekeza hela zote katika vikao hivyo. So swala la katiba kwa sasa msahau maana halina tija. Ni bora mkaliweka kwenye ilani yenu ya mwaka 2025.
 
Back
Top Bottom