Ukimya wa Wizara ya Michezo ni uthibitisho kwamba kuna "Mkubwa" alikurupuka

Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,207
2,000
Toka sekeseke la kuvurugika kwa mchezo wa watani wa Jadi,Wizara ya michezo imekuwa bubu licha ya TFF kueleza kuwa ilipokea maelekezo ya kubadilisha muda toka Wizarani. Kuna usemi kwamba "If you hide the truth people will create their truth". Sasa kuna uvumi mwingi na kila mtu anaongea lake.

Kwenye hili lazima wizara itoe maelezo yaliyojitosheleza kueleza:-

1. Ni sababu zipi zilizosababisha waiamuru TFF kusogeza mbele mchezo masaa 3 kabla ya muda wa awali wakati si jukumu lao bali la bodi ya ligi.

2. Pesa za viingilio zitarudishwa vipi kwa mashabiki?

3. Kama kuna uzembe wa kiutendaji kwanini mpaka sasa hakuna aliyewajibika?

Hatuwezi kuendelea kuchezewa akili na viongozi tuliowachagua ili watutumikie badala yake wanataka sisi ndo tuwatumikie. Hapa lazima mtu awajibike.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom