Uchaguzi 2020 Ukimya wa Tume ya Uchaguzi na kauli tata za wagombea

Sinamboga

Member
Dec 6, 2012
83
36
Tume yetu ya uchaguzi imekua kimya sana kuchukua hatua kwa kauli tata zinazotoka kwa Wagombea katika uchaguzi huu. chaguzi hasa Barani Afrika hazijawahi kuwaacha salama waafrika na bila ya mifakano ya kutosha.

Inawezekana Imeshatoka miongozo mbalimbali lakini kadri tunavyozidi kufanya chaguzi ndivyo tunavyozidi kutengeneza hasama, Tume mmekua kimya sana, inawezekana kwa uchache wenu lakini watumieni na viongozi wa dini pia.

Msiache pia kutoa kongole kwa mashabiki na wanachama wa vyama kwa mfano wa Vunjo walioamua kucheza kwa pamoja "One love" Bob Marley.

Kwa mfano. kauli ya mgombea akisema nimejenga Barabara hii kwa sababu ya fulani, Bila huyu nisinge jenga hii barabara inaondoa hiari ya uchaguzi huru na inaleta uoga japo sote tunalipa kodi.

Na Siku ikitokea nusu/nusu ni wagombea wa vyama tofauti basi ndio utakua mwisho wetu maanake waliochaguliwa watataka kupeleka maendeleo kwa waliowachagua na wale wengine hawatakubali.

Ni hayo.
 
Back
Top Bottom