Ukimya wa Mawaziri: Wanatetea wananchi au matumbo yao?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,532
Baraza la mawaziri chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya Tano ya mhe. John Pombe Magufuli limekuwa kama imepigwa ganzi. Mawaziri hawasimami wao kama wao katika kusimamia wizara zao.

Mawaziri wanatoa "promising statements" kila kukicha ili tu zimfurahishe mhe Rais bila kujali kama wanawafurahisha wananchi kwa kuwatimizia mahitaji yao.

Mifano hai ni mingi, Wizara ya elimu ni kama vile hailewi kile inachosimamia,utumishi wa umma nayo hali kadhalika, wizara ya afya ni wizara nyeti inayokabiliwa na changamoto kibao ikiwemo ukosefu wa chanjo kwa wahusika na mambo mengine mengi of alikes, Wizara zingine pia zinapuyanga tu hovyo hovyo ikiwemo Wizara ya Mambo ya ndani chini ya Mwigulu Nchemba.

Mimi binafsi Wizara ya Ardhi chini ya William Lukuvi naweza kusema ndiyo wizara inayotimiza wajibu wake kikamilifu kabisa bila kujali kama inafurahisha Mhe. Rais Bali inatumikia wananchi kama ilivo ada. Hebu tujiulize na tujadiliane kwa uwazi kabisa,mawaziri wameteuliwa ili kumridhisha/kumfurahisha mhe. Rais au wanatumikia matumbo yao binafsi(maslahi yao)?.

Karibuni.

Rais2020
 
Baraza la mawaziri chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya Tano ya mhe.John Pombe limekuwa kama imepigwa ganzi. Mawaziri hawasimami wao kama wao katika kusomamia wizara zao. Mawaziri wanatoa "promising statements" kila kukicha ili tu zimfurahishe mhe Rais bila kujali kama wanawafurahisha wananchi kwa kuwatimizia mahitaji yao. Mifano hai ni Mingi,Wizara ya elimu ni kama vile hailewi kile inachosimamia,utumishi wa umma nayo Hali kadhalika,wizara ya afya ni wizara nyeti inayokabiliwa na changamoto kibao ikiwemo ukosefu wa chanjo kwa wahusika na mambo mengine mengi of alikes,Wizara zingine pia zinapuyanga tu hovyo hovyo ikiwrmo wizara ya mambo ya ndani chini ya Mwigulu Nchemba. Mimi binafsi Wizara ya Ardhi chini ya William Lukuvi naweza kusema ndiyo wizara inayotimiza wajibu wake kikamilifu kabisa bila kujali kama inafurahisha Mhe. Rais Bali inatumikia wananchi kama ilivo ada.
Hebu tujiulize na tujadiliane kwa uwazi kabisa,mawaziri wameteuliwa ili kumridhisha/kumfurahisha mhe. Rais au wanatumikia matumbo yao binafsi(maslahi yao)?.

Karibuni.
Rais2020

Gombea tu Urais ndugu yangu hawa Baraza la mawaziri wako Tumbo street zaidi hamna kitu huko.
 
Mheshimiwa William Lukuvi amejipambanua kama mzalendo mwenye uchungu na matatizo ya wananchi! Anafanya kazi nzuri sana bila kujali kama kuna kamera au vinginevyo! Huu ndio uteuzi pekee ambao naweza kumpongeza rais JPM!
 
Mheshimiwa William Lukuvi amejipambanua kama mzalendo mwenye uchungu na matatizo ya wananchi! Anafanya kazi nzuri sana bila kujali kama kuna kamera au vinginevyo! Huu ndio uteuzi pekee ambao naweza kumpongeza rais JPM!
Ni ukweli usiopingika. Huyu haangalii makamera kama kina Kigwangala wanaoshughulikia mashoga badala ya kushughulikia mambo makubwa katika Taifa.
 
Wamelemewa na kutaka kumufurahisha aliyewaweka kwenye kigoda na wengine wanafanya kazi kwa tahadhali yasije ya kawakuta ya Nape siunajua mtakatifu mwenyewe haeleweki unaweza ukajiona kuwa unafanya vizuri kumbe kwake ni maudhi.
 
Wamelemewa na kutaka kumufurahisha aliyewaweka kwenye kigoda na wengine wanafanya kazi kwa tahadhali yasije ya kawakuta ya Nape siunajua mtakatifu mwenyewe haeleweki unaweza ukajiona kuwa unafanya vizuri kumbe kwake ni maudhi.
Ni bora kuachia ngazi kuliko kutumika
 
Back
Top Bottom