Ukimya wa Kamati ya Usalama na Ulinzi ya Bunge...

Jina zuri la hiyo kamati iwe "Kikundi cha ulinzi na usalama wa ccm" kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa msuli na maslahi ya ccm na si kwa ajili ya watanganyika
 
Walioingia kwenye hizo kamati walikuwa wameingia si kwa maslahi ya wananchi bali ya kwao binafsi ndio maana kamati zote nyeti hata zile za wapinzani wanaoziongoza lazima wawe na msimamo usiopingana na maslahi yao angalia Cheyo,Mrema na Zitto wote kwa nyakati tofauti misimamo ya kisiasa imekuwa inatia mashaka,Serukamba,chenge,Lowasa wanajulikana ni watu wa kundi moja wameshika kamati nyeti ili kupanga timu zao na mipango yao hata ya Nishati walimweka January makusudi
 
Kamati hii inaongozwa na nani vile? Huyu mwenyekiti si yuko kwenye katuni ya wesite ya CDM kakumbatiwa na serikali? Tena huyu si anatuhumiwa kufanya kazi ya kuhujumu CDM kwa kuchakachua matokeo huko kaskazini? Huyu si gamba gumu? Si anataka kuwa rais kupitia CHAMA CHA MAFISADI? Hawezi kujikaanga kwa mafuta yake!..
 
Hii kamati inasimamiwa na vigogo wa ccm mnategemea waseme nini? They r all hypocrites
 
Kamati haiwezi kuongea kitu hapo, ukichukulia Polisi wanamsafishia njia ya kuingia ikulu Mwkt wa Kamati iyo.Kutapakaa kwa CDM hasa mikoani ni tishio kwake kisiasa. Shughuli nyingine za kamati ni kuangalia "uwajibikaji" wa waziri wa Mambo ya Nje. Nje ya hapo kamati haiwezi kusema neno, vinginevyo kuwepo tishio or upenyo wa kumtangaza Mwkt husika wa kamati hasa kuelekea 2015. Case ya Malawi ni mfano mzuri.
 
kwitega kwa hilo na mimi naomba niombe radhi miaka 5 kurudi nyuma binafsi kwenye huo mtego nillingia na nikawachukia CUf kabisa, lakini these days, akili za watu zimefunguka,hata facebook generation sasa hivi inajua mengi ila pia CUF mmejipoteza wenyewe hamuoni mlipokosea jamani? all i can say is, NCCR na CUF ni pioneers kwenye kipindi kigumu ila Chadema wanapata urahisi sababu watz wanaanza kuwa wajanja sasa
 
Ukweli viongozi wa CCM ni wabinafsi mno na watanzania hatutapiga hatua ya maendeleo bila kuwatoa madarakani. Unajua chama kingine kikichukua madaraka CCM watajipanga upya na kuwa waangalifu zaidi. Laiti ile katiba ya CCM ingekuwa inatumika!!! Hivi kwa nini tunawapa madaraka watu wanaoibaka katiba ya chama chao wenyewe na wakati mwingine kuivunja katiba ya nchi aidhakwa kujua au kutokujua na kwa vyovyote ni makosa?
 
Labda kwa sababu kamati inaongozwa na mbunge ambae ni wa chama kinachoongoza nchi hivyo si rahisi kwake kukosoa utendaji wa vyombo vya dola lakini kiuhalisia alitakiwa kukemea matukio haya ambayo yanafanywa dhidi ya watanzania wanyonge na wasio na hatia.
 
lowassa hana kabisa uchungu na watu maskini. yeye alitaka kua mwenyekiti ili asisahaulike kisiasa kwa ajili 2015.
 
Kwa kuangalia wenyeviti ambao huongoza kamati hii, ni rahisi kugundua kuwa kamati yenyewa ina majukumu zaidi ya yale ambao watu wa kawaida tunayaona au kuyafikiria!!

Baadhi ya watu ambao wamewahi kuwa wenyeviti wa kamati hii ni:

1. William Kusila (former Minister...ila nasikia ni mfanyakazi mwaminifu wa kule mahali....)

2. John Samuel Malecela (former PM and VP)

3. Edward Lowasa (PM aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond na aspirant wa Urais 2015)


Wanaokumbuka wengine wanaweza kutuwekea hapa...ila kwa ufupi, hawa watu wanatokea jikoni sana kiasi kwamba hata chakula kikiungua hawawezi kusema lolote!!
 
Sababu ni kwamba hiyo agenda haitamwongezea mtu kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea. Suala la Malawi ilidhaniwa ni agenda ya nguvu kuonyesha kuwa mtu ana stahili kuwa Amir jeshi Mkuu maana anajua historia ya nchi na kwamba hawezi kutishwa kwani anajua namna ya kutumia madaraka yake. Mimi nashangaa watu eti wanaongelea umri na sijui na afya yake. Mimi nasema hana sifa NI AIBU NA ITAKUWA KICHEKESHO CHA MWAKA KUMFIKIRIA HATA KUWA MJUMBE TU WA NEC KWA SIKU ZA USONI!! Chunguza kwa makini na ndio maana CHADEMA wametulia tu ili aogezwe yeye.
 
kamati ziko busy kufuatilia mambo ya mshiko tuu..mambo ya maana kama haya huwezi kuwasikia........
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom