Wakuu nimetafakari kwa kina jinsi huyu mgombea wa CCM kwa ngazi ya Urais alivyotengwa na watu makini na wenye mvuto katika siasa za Tanzania hasa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na sasa Balozi nchini Sweden Dkt. Slaa na aliyewahi kuwa Luten Kanali Na waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa. Hii ina maana gani kipindi hiki ambacho Magufuli anahitaji sapoti kubwa kutokana na kupambana na mgombea mahiri na mwenye mvuto kama Lissu?
Je, ni aina fulani ya kuunga mkono hoja za Lissu kwa hiyo hawaoni haja ya kumtetea yule aliyewahonga vyeo? Kwa kawaida manguli hawa huwa wanasikika wakitoa neno na hata walipohamia CCM walitoa mawazo yao kama wadau wa siasa na maendeleo za hapa nchini.
Wako wapi akina Mangula, wako wapi akina Kikwete, wako wapi akina Mwakyembe, wako wapi akina Nchimbi?
Au ndio wameona mgombea wao hauziki tena?
Nawasilisha kwa maoni zaidi.