Ukimwona mtu tajiri, Tamani kuwa kama yeye, na ukimwoma Masikini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukimwona mtu tajiri, Tamani kuwa kama yeye, na ukimwoma Masikini...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Nov 5, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Kwenye Uchina ya Kale kulikuwa na mwanafalsafa kwa jina la Comfucius. Katika mafundisho yake mengi aliyopata kumpa mwanafunzi wake Tzu Kung mojawapo linahusu dhana ya utajiri na mahusiano yake na umasikini.

  Comfucius anasema; ukimwona mtu tajiri(aliyefanikiwa kimaisha),basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye maskini, basi, jitafakari wewe mwenyewe.

  Kwa mwanafalsafa Comfusius, dhana ya utajiri haikuwa na maana kuwa na mali pekee, bali, pamoja nazo, ni uwezo wa mtu kuishi maisha adilifu na yenye fadhila (virtues). Na katika fadhila zote, ile ya unyenyekevu na ukweli ndio chanzo cha fadhila nyingine zote.

  Umaskini vilevile, yumkini unaweza kuwa na maana ya kukosa mali na uadilifu. Ndio, mwanadamu waweza kuwa na mali lakini ukakosa uadilifu. Ni dhahiri, katika hali hiyo, hata mwenye mali naye ni maskini sana.

  Ndugu zangu,

  Nayaandika haya baada na huku nikiendelea kusoma alama za ukutani.

  Kuna kitu kinatokea katika jamii yetu. Wengine wanakiona, wengine hawakioni. Na kuna wanaoonyeshwa , lakini wanashindwa kukiona. Tunafanyaje?


  Ndugu zangu,
  Hakuna kitu kingine bali ni watu ndio wenye kuifanya nchi. Kuna kitu kimetutokea waTanzania. Kinaendelea kuota mizizi. Na kwa vile kitu ndicho hufanya vitu, basi, mimi naviona vitu vya hovyo hovyo vikitokea katika jamii yetu. Na pengine, kwa vile tumeanza kuwa na hulka za hovyo hovyo, basi, vinavyotokea hatuvioni kuwa ni vya hovyo hovyo.

  Naam, vinatokea kila leo, na kuna wenye kusimama kuvitetea vitu hivyo vya hovyo hovyo. Ni kuanzia namna tunavyouza rasilimali zetu na wenye kuuza, ni viongozi wetu waliogeuka ' madali' wa kutanguliza tenipasenti. Hawa wa kundi la pili ndio matajiri wetu wapya waliopungukiwa chembe nyingi za uadilifu, hivyo basi, nao ni masikini.

  Na tumeimbiwa sana, kuwa nchi yetu ni maskini (japo wanamaanisha kipato pekee) na wanasahau au hawaju kuwa sisi ni maskini zaidi kwenye maadili.


  Ndugu zangu,

  Na tunavyoelekea sasa kwenye miaka hamsini ya Uhuru , tujifunze kutoka kwa mwanafalsafa Comfusius . Kwamba katika umasikini wetu huu kama taifa, basi, walau tujitahidi kujitafakari tulivyo huku tukiwaangalia wenzetu waliopiga na wanaondelea kupiga hatua za mafanikio ya kiuchumi.


  Ndugu zangu,
  Oneni kule Marekani. Hawa ni matajiri wa kipato. Wanafanya kazi usiku na mchana kutimiza ndoto ya taifa lao. WaMarekani wanaijua ndoto yao na huungana dhidi ya yeyote anayetaka kuikwamisha. Ni pengine ni katika kutimiza ndoto hiyo sisi tunalalamika kuwa Marekani ni taifa baya.

  Tujiulize; ni taifa gani litaishi bila kuwa na ndoto na haja ya kuwa na maslahi ya kudumu? Hivi, ni nini ndoto na maslahi ya kudumu ya Tanzania? Je, ni WaTanzania wangapi wakiwemo viongozi wanaijua sera ya Tanzania inapohusu uhusiano wake na mataifa mengine?

  Fikiri, tumepeleka majeshi yetu kuzikomboa nchi nyingine, lakini, ni vigumu kuona tumepata nini kiuchumi ukiacha sifa ya kuwa ni taifa karimu.


  Angalia Rwanda. Ni kanchi kadogo sana lakini kameshajua ni nini maana ya kuwa na ndoto na haja ya kuwa na maslahi ya kudumu . Ndio maana hukusikia Rwanda ikitafuna maneno katika kuitambua Serikali ya Mpito ya Libya.

  Leo Rwanda wako ndani ya DRC na wana maslahi ya migodi ya madini ya huko. WanyaRwanda wale wamepenya hadi Uganda na Burundi. Na nani atabaisha, kuwa WanyaRwanda wamepenya hata kwenye uchumi wetu.

  Ndugu zangu,
  Tumekuwa ni watu wa hovyo hovyo. Tupo kama hatupo. Tunayakimbia mambo ya kimsingi kwa taifa letu. Tumejikita zaidi kwenye hoja nyepesi nyepesi ikiwamo fitina na majungu. Ndio, WaTanzania tunabaguana kisiasa na kuna ambao, piga ua, watahakikisha tunapata Katiba Mpya ya hovyo hovyo ili tuendelee na mambo yetu ya hovyo hovyo.

  Hatujachelewa, na tujifunze kutamani kuwa kama walio matajiri(katika maana ya mwanafalsafa Comfucius).

  Ndugu zangu,

  Naomba kuwasilisha hoja.


  Maggid Mjengwa
  Iringa.
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Makala nzuri Majjid, kweli inabidi tujitafakari kama nchi tunakwenda wapi na nini malengo yetu. Haya mambo ya vyama yanaturudisha sana nyuma.
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwenye kuelewa na ameelewa
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mie natamani siku moja tutoane ngeu nchi nzima pengine itaamsha walio isingizini na wasiotaka kuelewa shida za watanzania walio wengi. Ni muda tu, ukifika kila kitu kitakaa kwa mstari. Isitoshe wengi wetu tumeamka tunasubiri muda tu kufanya kile ambacho wengine wamekifanya na kurudisha heshima ya utu wao. Ngoja tu muda hauko mbali!
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Makala yako ina mafundisho kweli hilo ni Neno la leo
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Maggid kwa hilo umenena, thanks...
   
 7. m

  maggid Verified User

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]Ndugu zangu,

  JAMBO moja kubwa ni dhahiri, kuwa Watanzania bado tuna safari ndefu sana kufikia hatua ya kuitwa taifa la kisasa.[/FONT] [FONT=&amp]

  Tuyafanyayo mengi bado ni mambo ya hovyo hovyo, na wenye kuongoza kuyafanya hayo ya hovyo hovyo ni viongozi wetu. Lakini hatuna jinsi, hatua tunayopitia sasa ni lazima tuipitie. Hakuna njia nyingine ya kupita na kutufikisha kwa haraka tunakotaka kwenda. Tusisahau tu , kutunza kumbukumbu. Tufanye hivyo ili Watanzania wa vizazi vijavyo waje wajifunze kutokana na matendo yetu.[/FONT] [FONT=&amp]

  Tulikuliku ni aina ya ndege. Viongozi wetu wanaweza kujifunza kutoka kwa ndege huyu. Tulikuliku ana kanuni inayomwongoza. Mara ile tulikuliku anapotaga mayai, basi, hufanya maamuzi magumu ya kujinyonyoa manyoya yake.

  Kwa pamoja, tulikuliku dume na jike watafanya tendo hilo.

  Kwanini?[/FONT] [FONT=&amp]
  Wanajiwekea wenyewe mazingira ya kushindwa kuruka. Wanafanya hivyo ili waatamie mayai yao hata atakapotokea nyoka mpenda mayai wapambane nae hapo hapo. Kwamba wangebaki na manyoya, huenda wangemwogopa nyoka. Hivyo, wangeruka na kuacha mayai yakiliwa na nyoka.


  Kwa kiongozi kujinyonyoa manyoya ina maana ya kukubali kushuka chini kwa watu. Kuyaelewa matatizo ya watu anaowaongoza. Kuwa tayari kupambana kuyatatua matatizo ya watu akiwa na watu.[/FONT] [FONT=&amp]

  Ilivyo kwa viongozi wetu wengi wa leo, ni kuwa, katikati ya dhiki kubwa ya wanaowaongoza, si tu wamefuga manyoya mengi, bali, hata pale wananchi wanapokabiliwa na adui maradhi, wao, viongozi, wana mbawa za kuwawezesha kuruka juu angani huku wakiwaimbia watu wao nyimbo za kejeli. Na bado watafanya hila ili kuwachonganisha na kuwagawa watu wao walio kwenye dhahma ya umasikini.[/FONT] [FONT=&amp]

  Na kuna mawili ambayo yaliwezekana kutumiwa na yakafanya kazi miaka ya sitini hadi themanini, na mawili hayo hata yanapotumika sasa, hayafanyi kazi tarajiwa. Maana, wakati umebadilika. Ni yepi hayo?[/FONT] [FONT=&amp]

  Naam, ni kwa kiongozi kutumia Uongo na kutishia nguvu za mamlaka. Kiongozi anayetaka kufanikiwa katika zama hizi ni yule aliye tayari na kuachama na mambo ya zama hizo; kuwaongopea watu wako na kutishia nguvu za mamlaka. Badala yake, kuwa tayari kufanya maongezi hata na wale ambao huko nyuma haikuwezekana kukaa nao meza moja.[/FONT] [FONT=&amp]


  Vinginevyo, Watanzania tungali na safari ndefu sana. Njia ina miba mingi, lakini ni lazima tuipite. Hakuna njia nyingine. [/FONT]

  [FONT=&amp]Nilipata kuandika, kuwa kwenye Uchina ya kale kulikuwa na mwanafalsafa kwa jina la Comfucius. Katika mafundisho yake mengi aliyopata kumpa mwanafunzi wake Tzu Kung, mojawapo linahusu dhana ya utajiri na mahusiano yake na umasikini. [/FONT]

  [FONT=&amp]Comfucius anasema; ukimwona mtu tajiri(aliyefanikiwa kimaisha),basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Kwa mwanafalsafa Comfucius, dhana ya utajiri haikuwa na maana kuwa na mali pekee, bali, pamoja nazo, ni uwezo wa mtu kuishi maisha adilifu na yenye fadhila (virtues). Na katika fadhila zote, ile ya unyenyekevu na ukweli ndio chanzo cha fadhila nyingine zote.[/FONT]

  [FONT=&amp]Umasikini vilevile, yumkini unaweza kuwa na maana ya kukosa mali na uadilifu. Ndio, mwanadamu waweza kuwa na mali lakini ukakosa uadilifu. Ni dhahiri, katika hali hiyo, hata mwenye mali naye ni masikini sana. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Kuna kitu kinatokea katika jamii yetu. Wengine wanakiona, wengine hawakioni. Wengine wanakiona lakini hawataki kukiona. Na kuna wanaoonyeshwa , lakini wanashindwa kukiona. Tunafanyaje?[/FONT]

  [FONT=&amp]Hakuna kitu kingine bali ni watu ndio wenye kuifanya nchi. Kuna kitu kimetutokea waTanzania. Kinaendelea kuota mizizi. Na kwa vile kitu ndicho hufanya vitu, basi, mimi naviona vitu vya hovyo hovyo vikitokea katika jamii yetu. Na pengine, kwa vile tumeanza kuwa na hulka za hovyo hovyo, basi, vinavyotokea hatuvioni kuwa ni vya hovyo hovyo. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Naam, vinatokea kila leo, na kuna wenye kusimama kuvitetea vitu hivyo vya hovyo hovyo. Ni kuanzia namna tunavyouza rasilimali zetu. Na wenye kuuza, ni viongozi wetu waliogeuka ' madalali' wa kutanguliza tenipasenti. Hawa wa kundi la pili ndio matajiri wetu wapya . Ni watu waliopungukiwa chembe nyingi za uadilifu, hivyo basi, nao ni masikini.[/FONT]

  [FONT=&amp]Na tumeimbiwa sana, kuwa nchi yetu ni masikini (japo wanamaanisha kipato pekee). Wenye kutuimbisha wanasahau, au labda hawajui, kuwa sisi ni masikini zaidi kwenye maadili. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Ndugu zangu, [/FONT]

  [FONT=&amp]Katika wakati huu tunaoenda nao, na tujifunze kutoka kwa mwanafalsafa Comfucius. Kwamba katika umasikini wetu huu kama taifa, basi, walau tujitahidi kujitafakari tulivyo huku tukiwaangalia wenzetu waliopiga na wanaondelea kupiga hatua za mafanikio ya kiuchumi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Maana, nasi tutamani kuwa taifa la kisasa. Lakini hatuwezi kuwa taifa la kisasa kwa staili hii tunayoenda nayo. Oneni kule Marekani. Hawa ni matajiri wa kipato. Wanafanya kazi usiku na mchana kutimiza ndoto ya taifa lao. WaMarekani wanaijua ndoto yao na huungana dhidi ya yeyote anayetaka kuikwamisha. Na pengine ni katika kutimiza ndoto hiyo sisi tunalalamika kuwa Marekani ni taifa baya. [/FONT]

  [FONT=&amp]Tujiulize; ni taifa gani litaishi bila kuwa na ndoto na haja ya kuwa na maslahi ya kudumu? Hivi, ni nini ndoto na maslahi ya kudumu ya Tanzania? Je, ni WaTanzania wangapi wakiwemo viongozi wanaijua sera ya Tanzania inapohusu uhusiano wake na mataifa mengine? [/FONT]

  Na hilo ni Neno La Leo:
  Maggid Mjengwa,
  Dar es Salaam
  13, Septemba, 2011
   
 8. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Maggid,

  Ulanzi uliokunywa leo unaonekana ni mzuri sana. Umezungumza maneno mazito na yanayotaka watu kufikiri kwa kina. Tanzania tuna na njia ndefu sana kwani ile dhana ya cheo ni dhamana imetoweka.
   
 9. m

  maggid Verified User

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180

  Asante ndugu yangu Rufiji,

  Inanikumbusha pia kisa kile cha Idi Amin na mwandishi wa Kitanzania!
  Siku Njema.
  Maggid
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Maggid,
  Articles zako huwa zinakuwa nzuri mno, ila kibaya ni kwamba wakati mwingine huwa unajifanya chizi
   
 11. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  asante maggid . ...umeongea jambo la maana sana....kuna tatizo jingine....tofauti za itikadi zetu za kisiasa tumeziweka mbele zaidi ya uzalendo......kuna baadhi wako radhi kuhujumu jambo fulani jema kwa jamii ili mradi wafaidike kisiasa......
   
 12. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Ukitulia unakuwa mwalimu mzuri ila ukinusa mkangafu tu unaharibu
   
 13. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,702
  Likes Received: 8,239
  Trophy Points: 280
  Reminds me of mraba wa maggid...ngoja nijitafakari walau nifight kuupata utajiri wa maadili ili taifa la kesho wasije kunitukana.
  Thnks Maggid...
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Is Maggid again!!....
  Alamsiki.
   
 15. m

  maggid Verified User

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mtanzania 1,

  Asante sana,
  Kwa bahati nimechelewa kupitia thread hii kwa vile nilikuwa safarini. Kuna jambo nataka kuongezea katika ulichoongolea. Inahusu utaifa.

  Ni kweli, Watanzania tunaendekeza sana siasa za vyama na kuiahau Tanzania yetu. Leo asubuhi sana niliianza safari yangu kutoa Msamvu , Moogoro kuja Irina. Ni kawaida kando ya barabara kwenye makazi ya watu au vibanda vya biashara kukuta ikipepepea, ama, bendera ya CCM, Chadema, CUF, Simba au Yanga. Lakini, ni nadra sana kuiona ipeperushwa bendera ya taifa letu. Leo pale nje kidogo ya Ruaha Mbuyuni niliona kwenye banda moja la biashara ikipepea bendera ya taifa. Nilishtuka kuiona , niliguswa pia. Nlipunguza hata mwendo kumwangalia kijana yule aliyekuwa akifanya biashara yake ya vitunguu huku bendera ya nchi yake ikipepea.

  Maana, bila shaka kijana yule kwa mapenzi ya nchi yake aliitafuta mwenyewe bendera ile ya taifa. Kwa vile, unapoona mahali kuna vijana wanapeperusha bendera za vyama yaweza kuwa na tafsiri ya ama, ni wapenzi wa vyama hivyo, na kuwa wamezitafuta wenyewe, au kuna kada wa chama husika aliyekuja na kugawa bendera hizo kwa vijana hao.

  Ndio, tunahitaji kufanya jitihada za kuwafanya watu wetu waipende nchi yao waliyozaliwa, kutoka ndani ya mioyo yao. Na moja ya jitihada hizo ni kuwapa maarifa yatakayowawezesha kujitambua, kujiamini na kuthubutu.

  Maggid
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmmmhhhh!
   
 17. S

  SIR DAS Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanx kaka kwa kutuelimisha, big up
   
 18. S

  SIR DAS Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I like it
   
 19. m

  maggid Verified User

  #19
  Feb 10, 2013
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Leo asubuhi nikiwa kwenye jogging hapa Iringa nilikutana na picha ya watu wazima wawili; wote wameshika baiskeli. Hawaendeshi, wanazikokota.

  Mmoja anapandisha, mwingine anashuka. Jua la asubuhi lilikuwa likichomoza. Anayeshuka anapigwa na jua usoni, anayepanda, mgongoni.

  Niliipiga picha ile. Kisha nikaendelea kufanya jogging huku nikitafakari kuhusu maisha. Kuwa katika dunia hii, kama ilivyokuwa kwa watu wale wawili; kuna kupanda na kushuka.

  Kuna masikini na matajiri. Masikini anaweza kuwa tajiri na tajiri anaweza kurudi kwenye umasikini. Hakuna aliyezaliwa kuwa masikini daima na kinyume chake. Ni mazingira tu. Kama mwanadamu, ukisema mimi siwezi hutaweza, na kinyume chake.

  Na wengi walioshinda katika maisha humu duniani wana historia ya kushindwa pia. Wengine wamepata kushindwa mara nyingi, lakini, hawakukata tamaa. Walianguka, wakasimama kuendelea kupambana.

  Ndio, katika dunia hii, mwanadamu unatakiwa upambane mpaka pumzi yako ya mwisho. Kwenye Uchina ya kale kulikuwa na mwanafalsafa kwa jina la Comfucius. Katika mafundisho yake mengi aliyopata kumpa mwanafunzi wake Tzu Kung, mojawapo linahusu dhana ya utajiri na mahusiano yake na umasikini.


  Comfucius anasema; ukimwona mtu tajiri(aliyefanikiwa kimaisha),basi tamani kuwa kama yeye, lakini, ukimwona aliye masikini, basi, jitafakari wewe mwenyewe.


  Kwa mwanafalsafa Comfucius, dhana ya utajiri haikuwa na maana kuwa na mali pekee, bali, pamoja nazo, ni uwezo wa mtu kuishi maisha adilifu na yenye fadhila (virtues). Na katika fadhila zote, ile ya unyenyekevu na ukweli ndio chanzo cha fadhila nyingine zote.


  Umasikini vilevile, yumkini unaweza kuwa na maana ya kukosa mali na uadilifu. Ndio, mwanadamu waweza kuwa na mali lakini ukakosa uadilifu. Ni dhahiri, katika hali hiyo, hata mwenye mali naye ni masikini sana.

  Na hilo ni Neno La Leo.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa
   
 20. akenajo

  akenajo JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 1,578
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Tunashukuru kwa ujumbe mzuri wenye kutia moyo j2 ya leo
   
Loading...