Ukimwi-watanzania Wanafanyiwa Majaribio Kama Guinea Pigs?

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Hebu someni hapa na hii inatia wazimu kuwa kwa kuwa jeshi lina nguvu hivyo linaamua kuwafanyia watanzania wenzetu majaribio bila hata ya kupata vibali huu ni ufisadi wa hali ya juu.


Mbunge wa upinzani aibua kashfa nyingine nzito bungeni kuhusu ukimwi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Karatu (Chadema), Dk Willibroad Slaa, ameibua kashfa nyingine inayomhusisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu, kwamba hospitali yake ilihusika kufanya utafiti wa dawa za ugonjwa wa Ukimwi iliyotengenezwa Afrika Kusini, licha ya serikali kuzuia utafiti huo.


Bila kutaja jina la IGP huyo aliyehusika katika sakata hilo, Dk Slaa alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu suala hilo na chombo kilichohusika kutoa kibali cha majaribio hayo kufanyika Hosptiali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo na kuhusisha Watanzania 64.


Naibu Waziri wa Afya, Dk Aisha Kigoda katika jibu lake alisema hakuna taasisi yoyote ya serikali iliyowahi kutoa kibali cha kufanya utafiti wa dawa za Ukimwi kutoka Afrika Kusini.


Dk Kigoda alisema, kumbukumbu zinaonyesha ombi la kibali cha kufanya utafiti liliwasilishwa NIMR mwaka 2000, lakini baada ya tathmini serikali ilikataa ombi hilo kutokanana maombi ya utafiti huo kuwa na upungufu mkubwa wa sayansi na maadili.


Alisema utafiti huo umefanywa kinyume cha taratibu za utafiti kwa sababu sio serikali wala Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Tume ya Sayansi na Teknolojia (CoSTECH) waliohusika na utoaji wa kibali cha utafiti huo.


Hata hivyo, Dk Kigoda alisema kwa sasa serikali imesimamisha utafiti huo, kuzuia uingizaji dawa pia kuzirejesha Afrika Kusini.


Alisema suala hilo ni kosa la jinai na kwamba, wananchi wana haki kufuata mkondo wa sheria kudai fidia kwa kuhusishwa na utafiti huo ambao hauna baraza za serikali.


Hata hivyo, Waziri Kigoda alisema baada ya serikali kufanya mazungumzo na viongozi wa JWTZ, taarifa zilionyesha kukataa kuhusika na kuwezesha kufanyika kwa utafiti huo.


Naibu Waziri huyo alisema, wizara yake inajitahidi kuongeza uwezo wa TDFA na NIMR,

kuchunguza tafiti mbalimbali zinazofanywa nchini kuhusiana na dawa na magonjwa ili

kuhakikisha zinafanywa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.

source;mwananchi.
 
Mimi nadhani taabu kubwa ni vibali na monitoring of the conduct of research activities in Tanzania...capacity kidogo... kuna wazungu wanafanya utafiti wa kila kitu... hata ngoma zetu za kenyeji!
 
Hapa tatizo lipo kwa wakina Mahita kwani wakati huo alikuwa mkuu wa jeshi la polisi na hosipitali yake inahusishwa kufanya utafiti ambao sio wa kisheria na wa madawa ambayo watengenezaji wa hayo madawa yaani South Africa wameyapiga marufuku kutumika kule kwao.

Hapa ni kuwa sisi tunatumia maisha ya watanzania wenzetu 64 kwa kutumia madawa ambayo yalikotoka wameyapiga marufuku.

Hii nchi hata kama wewe sio daktari ukiwa na cheo na hospitali yako unafanya utafiti tuu kwa vile una nguvu za kipolisi .

Tatizo hapa ni kuwa hakuna hatua zozote za kiserikali ama za kiutawala ziliweza kuchukuliwa dhidi ya hawa waliohusika .
 
Back
Top Bottom