Ukimwi waendelea kuteketeza maisha

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Wednesday, 01 December 2010

Na Waandishi Wetu, mikoani

TAASISI inayojihusisha na utoaji wa huduma mbalimbali za matibabu ya CCBRT, imeibuka kinara kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani.

Kivutio kikubwa kilikuwa jinsi waelimishaji rika na watoa ushauri nasaha wa CCBRT, ambao ni walemavu viziwi walivyomudu kushawishi waliohudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika uwanja wa Tangamano kupima Ukimwi.

“Nimeshawishika kuja kupima virusi vya Ukimwi baada ya kupata ushauri kutoka kwa Neema Abbas, ambaye ni kiziwi kanieleza vizuri hadi nikajikuta nikiingia banda la kupimia”alisema Mary Jumaa, mkazi wa Pongwe jijini Tanga.

Akizungumza na Mwananchi kuhusiana na huduma hiyo, Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa CCBRT, Naomi Lugoe, alisema shirika hilo limeamua kuhusisha walemavu katika utoaji wa huduma hiyo ili kutoa fursa kwa makundi yote kufaidika na upimaji wa hiari.

Akihutubia wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, John Gikene, aliwataka viongozi sekta zote kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuzuia maambukizi ya Ukimwi.

Kutoka Arusha inaripotiwa kuwa, waandishi wa habari wametakiwa kujiepusha na vitendo hatarishi vinavyochangia maambukizi ya Ukimwi.

Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema, alitoa wito jana wakati akifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari mkoani Arusha juu ya masuala ya Ukimwi.

Lema alisema waandishi wa habari kama wanajamii wengine, wanakabiliwa na tishio kubwa la maambukizi ya Ukimwi kutokana na mazingira ya kazi zao.

Wakati huohuo, Mkoa wa Iringa ukiwa bado unaendelea kuongoza kwa kasi ya maambukizi ya Ukimwi nchini, halmshauri za wilaya zimetakiwa kueleza mikakati wanayofanya katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka, alitoa wito huo wakati wa kikao cha kutambulisha mpango kazi wa kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Mpaka alisema katika utekelezaji wa suala lolote ambalo linahitaji kutoka hatua moja isiyokuwa na mafanikio kuingia nyingine ya mafanikio, lazima kuwepo na mikakati madhubuti itakayokuwa muongozo utakaowezesha kuondokana na hali waliyonayo.

Imeandikwa na Burhani Yakub, Tanga, Mussa Juma, Arusha na Tumaini Msowoya, Iringa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom