Ukimwi v/s Mimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukimwi v/s Mimba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sipo, Nov 5, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kati ya wanaume na wanawake ni wapi wanaogopa Ukimwi sana kuliko mimba na ni wapi wanaogopa mimba sana kuliko Ukimwi? Hasa kwenye mahusiano ambayo bado hayajawa kwenye mfumo wa ndoa.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Sipo, ungejaribu kuwa specific zaidi. Nadhani unakusudia kwenye mahusiaono yasiyo rasmi (yasiyo ya ndoa). Ndani ya ndoa, sioni ni vipi mtu aogope zaidi mimba kuliko ukimwi (awe mwanaume au mwanamke). Lakini katika mahusiano yasiyo rasmi, wengi (hasa wanawake) wanaogopa zaidi mimba kuliko ukimwi.
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Ukimwi mbaya jamani,japo wote tutakufa lakini kufa na gonjwa hili ni noma.
  Cha muhimu watu kabla ya kuanza sex nendeni kupima, mkikutana salama ndio hapo mule tunda then hata ukipata mimba ni heri.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hilo swali ni on a person to person basis kwa hiyo usijaribu kupata a general answer. Personally no matter the case I believe in the long run its better to impregnate or get impregnated rather than contact HIV. Ni mtazamo wangu tu.
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MwanaFA, hapa kunahitaji ufafanuzi kidogo esp katika kipindi hiki ambacho mazingira ya mahusiano ya kuingiliana maungoni yanabadilika. Kuna yale weye mahusiano ya jinsia moja ( Mwanaume kwa mwanaume (Gays relationships) na yale ya wanawake kwa wanawake (lesibians) majibu yanaweza kuibuka ya ajabu mkubwa!.....kwani hao nao wapo kwnye dunia yao.

  Kama ni mahusiano ya "Adamu na Eva" (legal relationships), ukimwi mzee hakuna asieogopa, na mimba inayoogopwa sana ni ile isiyotarajiwa, tu yaani isiyo na maandalizi wala mategemeo ila bado kama mlikuwa mnacheza peku, kuna dhana (presumption) kuwa hata mkiambukizana au kupeana mimba, mlitarajia (foreseable effects).


  Kwa suala la ukimwi, mzee hiyo habari nyingine kabisa, kwa upande wa wanaume wengi hujaribu kujikakamua tu kuwa hawana hofu na hilo gojwa, lakini mzee nafsi ya kila mtu inajibu lake.....na ukitaka kujua jinsia zote zinahofu na hilo gojwa, hebu jaribu kukaa na mtu ambaye unaamini kiafya yupo shwari, muda huo huo utumiwe ujumbe mfupi kuwa huyo mwenzio hakidhi viwango vya ubora ( yaani muda wake wa matumizi umekwisha (expired). Hata kama ni ujumbe wa uzushi, utasinyaa..., na utataka kuthibitisha kwanza hiyo habari,......


  ANGALIA HIZO PICHA NA TOA JIBU KADILI YA HISIA ZAKO:

  [​IMG][​IMG]


  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 6. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Pretty, nimepata tetesi mitaani ambazo hazijathibitishwa kwamba mtu mwenye VVU akitumia antibiotics let's say for a week, then akaenda kupima VVU, majibu yanakuwa Negative. Any Idea?
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Aaaa jamani ukimwi unatisha kwani mimba ni ugonjwa??
  Mungu atuondolee hila balaa lililoko mbele yetu
  watoto wa shule na wasio na permanent uhusiano ndo wanaogopa mimba
  kama uko kwenye mahusiano halali kwa nini uogope mimba??
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  aaah basi wagonjwa wote wangekunywa antibiotics si kweli hayo maneno
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu ndoa si jibu la kukwepa ukimwi. Wangapi wana wenza wao lakini bado ukimwi una tawala? Angalia age group inayo andamwa sana na HIV. Uta kuta ni kuanzia 15 hivi mpaka 45 au kitu kama hicho. Sasa hapo ukiangalia watu wengi wenye umri kuanzia 30 mpaka 45 majority lazima wata kuwa wana ndoa. Njia bora ya kuji linda na ukimwi ni kuto kua na wenza wengi kwa wakati mmoja. Kujali afya yako kwa maana una pima mara kwa mara, una tumia kinga na hauamini afya ya mwenzio kirahisi. Ndoa ingekua jibu ya Ukimwi basi kwa jamiii zetu za Kitanzania ambazo zina thamini ndoa kusinge kua na HIV rate kubwa tuliyo nayo.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Kwanza tukubaliane kwamba hivi viwili japo vyaweza kupatika kwa njia moja, UKIMWI ni janga wakati Mimba ni heri!
  Sasa hebu tuone ni nani wanaogopa heri kuliko janga na vice versa.
   
 11. GP

  GP JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  utafiti mdogo niliouna ni kwamba kwa vijana wengi ambao wanakua wanamegana tu bila mpango wala kua na fyucha ndio hao wanakua waoga kupata mimba au kidume akiambiwa demu wake ana mimba anadata yuko tayari akaichoropoe, ndio maana utakuta akipata taarifa ya mimba anastuka kuliko ingekua ukimwi
   
 12. L

  Ligoma New Member

  #12
  Nov 11, 2009
  Joined: Nov 11, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Tena umesahau kuwa UKIMWI ni JANGA LA TAIFA ambalo linaua watu wengi sana.

  _____________________
  DAWA NI KUACHA ... NA KUMUOMBA MUNGU
   
Loading...