Ukimwi unatumaliza jamani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukimwi unatumaliza jamani.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by dada white, Oct 9, 2012.

 1. dada white

  dada white JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jaman UKIMWI unatumaliza jamani ARV ni kichaka kinachowaficha simba wakali sana
  NB;TULIENI JAMAN NITARUDI KUTOA USHUHUDA
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  haya tumetulia tuliiiiiiiiiiii kama maji ya mtungini
   
 3. data

  data JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,747
  Likes Received: 6,518
  Trophy Points: 280
  mmmhhh...wenzako tuna appointment leo.. em njoo na huo ushuhuda fasta... naweza cancel app.
   
 4. dada white

  dada white JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bora utulie wafu wazima wengi mno humu kwa jamii zetu na wanamuonekano mzuri tu ila expire date yao ipo karibu sana.
   
 5. dada white

  dada white JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hujachelewa pitien kupima kwanza
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  Ooohhh Fatuma ukiambiwa sitakuona leo?
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hawafi na umechelewa. Mtu ambaye yuko stable kwenye dawa na mambo ya lishe anaishi miaka zaidi ya ishirini. Nani anajua atafikisha umri gani bila kufa? Siku hizi wanaokufa ni wale wasiofuata masharti ya dawa na wanaoona aibu. Usimnyanyapae mtu kwani unasababisha wawe na hasira na kuusambaza zaidi. Toa elimu ya kujikinga na maambukizi ili kupunguza kasi zaidi. Huwezi jua kwani unaweza ambukizwa na yule unayemuamini kwani hata mkienda kupima anaweza kuwa kwenye window period ambayo ni very infectious. Take this msg. Tuache unyanyapaa, kwani unavyottenda mwathirika ndivyo na ye anavyotamani na we uje kuathirika! Ndo maana wengine wanaambukiza watoto wenu makusudi. Kwani unadhani huwa hawajui?
   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160

  Hiyo pointi muhimu sana umesema kwenye blue hapo
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Msilaume nanyi umalizeni wanangu kwa kuachana na tamaa na ujinga na upumbavu wa kusema: 'Huyu hawezi kuwa nao".
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Cheupe yamekukuta? Uliangalia umbile na kajitambi ka kubabaishia?
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  nimeipenda hiii.......
  Ingawa nilikuwa nasubiri mhusika aje kwanza kusimulia ndo tumshushie nondo na kumwelimisha......loh
   
 12. BJBM

  BJBM JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 545
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  mwenye kutoa ushuhuda kakimbilia wapi tena?
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280

  ..  ..  Mh!!

  Wewe mtoto mie nafikiri ARV ni dawa kama zilivyo dawa nyingine kazi yake kukuu ni kumuahirishia binadamu kifo, sio kuzuia kifo!!

  Watu wanakufa kila siku kwa mambo mengi, ajali magonjwa ya kawaida kabisa n.k na hilo utalisemaje?

  Usifikiri utaishi miaka 100 kwa sababu tu huna ngoma, utakuwa unajidanganya na kumkufuru mungu wako!!!

  Watu tunaishi na watoto yatima waliozaliwa na ugonjwa huo kwa upendo na kuhakikisha wanapata lishe bora na wana afya nzuri sana tu na wanaendelea na masomo vizuri.....wewe unawaita Simba waliojificha kwenye kichaka!?

  Sikiliza mdada, ndio maana kuna nyumba za ibada... ili uweze kuishi maisha marefu yenye tija nayenye kumpendeza Mungu unahitaji kuwa mcha Mungu!!
  Kuishi ukiwa malaya, mhuni, jamabazi na muovu wa kila aina na kutegemea kuwa utaishi maishi marefu eti kwakuwa tu huna Ngoma utakuwa unajidanganya!!!

  Kumbuka "Nyumba isiyolindwa na BWANA wailindao wanakesha bure!!''


  ..
   
 14. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Heri yako mwenye mkataba na mungu, ipo mbali.
   
 15. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0


  Pole sana kwa yote yaliyokukuta! Shusha ushuhuda wako bila shaka utawasaidia wengi humu. Maana kuna watoto wanaokuja juu kama moto wa kifuuu, kutwa wako humu wanaomba wafundishwe mapenzi lol!
   
 16. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hili nalo neno, ila pia tahadhari aliyeitoa mtoa mada ni muhimu sana kuzingatiwa!
   
 17. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  SAWA BABA! BAK kuna wimbo wa sikinde sijui una hii title vipi unao?au we ni za kidhungu tu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  unajua dada angu hili suala ni gumu sana. Unakumbuka enzi za tufe wengi? Ile ilitokana na pointing fingers walizokuwa wanapewa waathirika. Nina dada yangu aliambukizwa na mumewe makusudi kwani alimsema wifi yake aliyeathirika. Kitendo hicho kilimuudhi mume akaamua kwenda kuutafuta kwa nguvu zote na kuuleta nyumbani. Huwa nashtuka sana ninapoona watu wanawazungumzia vibaya waathirika kwani ni suala linaloongeza waathirika wengine. Kuna jamaa mwingine alisikia afisa mmoja anatumia arv akamsema vibaya kwa watu na yule afisa akasikia. Alichofanya alimuwinda mke wa yule jamaa mpaka akampata tena ukichukulia jamaa alikuwa tra!, na sasa hivi wote ni waathirika wanatumia arv. Hawa watu wanahitaji kupendwa na jamii ili wajue kwamba wana umuhimu wa kuwalinda wengine. Hizi kauli za living dead sizipendi kabisa!
   
 19. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  tutoe tahadhali kwa kuelimishana sisi na wao pia ila tusitoe tahadhali kwa kuwasema wao. Ndo maana siku hizi hata kanisani hakuna mahubiri makali kuhusu hiv.
   
 20. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kuna masimulizi yanayotoa elimu kwa umma tutayafurahia, lakini masimulizi yenye sura ya unyanyapaa tuyakatae kwa nguvu zote! Kuna watu humu ni waathirika, wanaishi na watoto yatima, ndugu waathirika, unadhani watajisikiaje? unajua mtu ukimpenda hata kufanya jambo baya nafsi itamsuta. Hata mwizi akiona unapenda kukuibia atajiuliza mara nyingi,labda iwe njaa tu!
   
Loading...