Ukimuamini mpenzi wako na kupuuza maneno ya watu, mtadumu milele! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukimuamini mpenzi wako na kupuuza maneno ya watu, mtadumu milele!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by eRRy, Nov 12, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]


  Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndio maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kulizungumzia. Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. Kwenu ninyi mlio katika mapenzi, aidha ya ndoa au uchumba, kwanza yawapasa mfahamu kitu mapenzi ni tunu au zawadi, mimi niite maalum kutoka kwa mola wetu.

  Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani katika maisha yetu, hivyo kwa wale wanaoyachezea chezea na kuyavuruga mapenzi kwa makusudi kwa kuumiza hisia za wenzao na kuwasababishia vilio vya simanzi si watu wa kupendeza kabisa mbele ya macho ya wale wanaojua hasa nini maana ya mapenzi. Sasa nikirudi katika kile nilichodhamiria kukiandika wiki, nazungumzia mambo mawili yanayokwenda sambamba ambayo endapo utayazingatia, yanaweza kuwa ni yenye manufaa katika ndoa na hata uhusiano wako wa kimapenzi.

  Moja miongoni mwa hayo mawili ni hili la kutosikiliza maneno ya watu. Ukae ukijua kwamba, wapo watu wasiopenda kuwaona wenzao wakiwa katika ndoa au uhusiano wenye furaha na amani. Watu hawa ndio wanaosababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi huku wapenzi wengine wakiachana wakiwa bado wanapendana. Maneno ya watu ndiyo yamekuwa yakijenga ama kubomoa ndoa nyingi hivyo basi sikushauri usiyasikilize kabisa ya watu, kuna mambo mengine ambayo unaweza ukaambiwa na watu yakakusaidia sana katika maisha yako.

  Wapo watu ambao wanaweza kukuhabarisha juu ya mambo mbalimbali, si vizuri ukawapuuza, wasikilize na pima maneno yao, angalia kama yanaweza kukusaidia ama laa. Ila sasa, kwa mfano anakuja mtu na kukuambia amemuona mumeo ama mpenzi wako na mtu mwingine, mtu huyu utamchukuliaje? Je anakuambia kwa nia njema au anafanya hivyo ili muachane afurahi? Endelea kujiuliza kwamba, endapo mkiachana yeye aliyekuletea taarifa hizo atafaidika na nini? Kwa kifupi hakuna.

  Ndio maana nasema, nayoambiwa na watu yachuje kwanza kabla ya kuyafanyia kazi sio kila unaloambiwa unakimbilia kuchukua uamuzi. Maneno ya watu mara nyingi sana yanasababisha kuvunja ndoa za watu wengi sana kama sio kusasabisha machafuko katika ndoa hivyo ni vyema ukaepukana nayo.

  Hata hivyo, utaweza kuepukana nayo kama tu utakuwa unamuamini mpenzi wako. Uaminifu ni kitu cha msingi sana kwani unaposhidwa kumuamini mwenza wako mara nyingi sana utakuwa ukidhani kwamba anakusaliti hata kama unavyodhani au kuambiwa na watu vinaweza vikakosa ukweli. Hali hiyo inaweza kukufanya ukakosa raha kila mwenza wako anapokuwa mbali na wewe. Si kukosa raha tu anapotoka ama anapokuwa mbali na upeo wa macho yako bali pia anaporudi unaweza kushindwa kuonesha upendo wako kwake na kuweza kujenga chuki dhidi yake.

  Ni wachache sana ambao ni waaminifu kwa wanandoa wenzao. Wengine wakipewa maneno ya uongo tu kwamba mwenza wake ana uhusiano na mtu mwingine anakubali mara moja hata kama habari hizo hazina ukweli wowote, matokeo yake unachukua hatua ambazo zinaweza kuteteresha penzi lenu.

  Amini kwamba mwenza wako ni mwaminifu kwako na jijengee mazingira ambayo na yeye ataamini kwamba wewe ni mwaminifu kwake. Muamini ili naye akuamini. Epuka sana kufanya mambo ambayo yanaweza kumsababishia mwenza wako akadhani una uhusiano wa kimpenzi na mtu mwingine. Waweza kufanya hivyo kwa kuwa makini na maneno yako pamoja na matendo yako ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kudhihirisha kwamba sio mwaminifu katika ndoa.

  Kitendo cha kuchelewa kurudi kazini kila siku bila kuwa na sababu za msingi, kulala nje, kuwa na uhusiano wa karibu na watu jinsia tofauti bila kuwepo na sababu za msingi, kupunguza mapenzi, kutokuwa na heshima ni baadhi ya matendo ambayo yanaweza kuonesha kwamba sio mwaminifu hivyo ni vyema ukaepukana navyo​
   
 2. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mtadumu na kulea watoto wa wanaume wenzio,
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nimeipenda hii post
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  yaani unataka watu waaminiane BLINDLY!
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  UKIMWI je maana unaweza ukaambiwa tunda linamegwa ukapuuza kumbe ndo ushaingiziwa kimeo hapo utadumu au unaenda kufa na wewe
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  wewe jamaa unamiakili sana..kesho ukitoka kazini pitia baa yeyote iliyo karibu nawe mwambie mhudumu akupatie ndovu mpya tatu.
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Na mie namuongezea serengeti tano
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  lakini na sisi wana ndoa kwa nini tusiwe waaminifu jamani

  Mtoa mada una ukweli hapo ila sasa ndo jamaa naona kina burn hawaamini kabisa
  Kuna mikasa ya ndoa
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  samahanini wanaume
  kuna baadhi ya wanaume wengine ni wazinzi sana ila wanona wivu hata wife akienda sokoni wanakuwa na mashaka kwanini??
  ama ukiwa mwizi na wewe masaa yote unaota unaibiwa
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha hata kama akizaa mzungu ukadanganywa ni zeru zeru ndoa itadumu kikubwa ubwege wa mwanaume ndo unadumisha ndoa lakini mwanaume ukiwa .....
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Tusiongee nadharia Tu, lazima ufanyie kazi maneneo ya watu, ww unafikiri kama mkeo/mmeo anamegwa atakuja kukwambia kwamba amemegwa? watu wanaomuona mitaani ndy watasema, na wewe utafanyia uchunguzi kujua ukweli, SIYO UPUUZE TU, MTAKUFA WOTE!!!!! Mtoa mada hapo juu naona ana matatizo, huwezi kuambiwa kuwa mkeo anagongwa na baba ubaya gesti ya mchammbawima UKACHUNA NA KUCHEKELEA eti unadumisha mapenzi!! kama umeolewa na mkeo sawa
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  FL1 na kuna baadhi ya wanawake wazinzi mno
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Na ndio maana watu wanakufa kwa presha zisizo na msingi.kujipa wasiwasi usio na maana.Na watu wengi ambao hawawaamini wenzao ni grat cheaters,wanadhani wanayofanya wao na wenzao hivohivo.
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Ni bora kufa kwa presha zisizo na msongi kuliko kufa kwa UKIMWI kwa uzembe.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Nov 12, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kupuuza maneno ya mtaani ni ujinga, inabidi kujiridhisha kama maneno hayo ni ya kweli au la, hapo nadhani mtaishi kwa upendo zaidi kuliko kupuuzia.
   
 16. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hapana burn,unajua kuna mambo mengine yamezidi jamani,mtu unamchunga hadi ****** unaenda nae.Kumchunguza sawa ,lakini tumia hekima.
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,502
  Trophy Points: 280
  Ndio mwendo wake huo mama. Kukabana mpaka kwenye penalti.
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  na wewe hujiamini na mimi?
   
 19. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dunia ya leo ni tofauti unacheka nae moyoni anamwazia mwingine
   
 20. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Najua una machungu ya wako kumegewa na midume 2 si chanzo cha kugundua ni kupata information kutoka kwa watu!
   
Loading...