Ukimuacha Tundu Lissu, hivi kuna Mtanzania mwingine ameshawahi kuhudhuria kipindi cha HardTalk?

Weka Clip ya Tundu Lissu akihojiwa na Chris Cuomo ama Don Lemon basi tuone? ama hata akihojiwa na Rachel Madow wa MSNBC. Huizo TV alizohojiwa USA ni kama hizi za kina Mirad Ayo tu

Anaweza akawa amehojiwa na vituo vingine vidogo lakini ukweli unabaki pia amehojiwa kwenye Hardtalk. Kwa sasa sioni mwanasisa mwenye ubavu wa kwenda kuhojiwa kwenye Hardtalk zaidi ya Lissu. Hawa wanasiasa wa Bongo bora tu waendelee kuulizwa maswali laini na waandishi uchwara wa Bongo kuliko kwenda kuwa kichekesho mbele ya dunia.
 
NDEGE KASUKU ANAONGEA SANA LAKINI HAWEZI KUPAA ZAID ANGANI

NDEGE TAI HAONGEI SANA ILA NDIO WANAOPAA ZAIDI ANGANI

UMEJIFUNZA NINI KUPITIA MSEMO HUU??

Nimejifunza kuwa Tundu Lissu anaweza vyote, kuongea sana na kupaa zaidi angani!!
 
Kwani Lisu ngeli inapanda?!!!

Acheni utani bhana...... Ngeli ya Lisu anazidiwa hata na January Makamba au Sugu!
Hata kama una wivu ama chuki, isiwe kwa kiwango hicho. Lissu anazidiwa umombo na mwenyekiti wako?
 
Sasa si bora waende kwenye Hardtalk ambayo haipo kwenye prime time kuliko kwenda kuaibika kwenye prime time programmes zinazoangaliwa na watu wengi?!
mbona hueleweki? umemzungumzia Lissu ama? Mimi nimekusaidia kukueleza kwamba hiyo Hardtalk siyo kipindi kikubwa kivile kwa wenyeji na lengo la Lissu si ilikua kuueleza umma wa UK nini anataka kuueleza? Sasa kama unahojiwa watu wamelala na marudio yake watu bado wamelala kuna u maana gani? Si bora tu ahojiwe na kina Milard Ayo?
 
Kama hunielewi hilo ni tatizo lako siwezi kukusaidia. Mimi mleta mada nilijikita zaidi kwenye ubora wa vipindi na waandishi wa habari, sio audience. Sijali kama kipindi kinaangaliwa na watu elfu moja au milioni moja.

Sasa turudi kwenye mada yangu. Bado siamini kwa sasa kama kuna mtu zaidi ya Lissu ana ubavu wa kwenda kuhojiwa kwenye kipindi chenye ubora wa Hardtalk, kiwe kwenye prime time au kisiwe.
 
Nilitaka nimuulize kuhojiwa HardTalk kuna wasaidia nini watanzania?
Wananchi wanataka maendeleo kama elimu bora, huduma za uhakika na nafuu za matibabu n siyo maneno matupu ya kiingereza.
Kijijin kwetu kuna tajiri mmoja lkn elimu yake ni darasa la 7, akiona vijana waliomaliza chuokikuu hawana hata buku mfukoni uwashangaa na kuwambia hiyo elimu yenu inawasaidia nini ameapa hawezi kumpeleka mwanae shule zaidi ya shule za msingi.
 
James Martin,

Kuzungumzia mdahalo kati ya Magu na Lissu ni uchochezi tena mkubwa. Magu hawezi kujenga hoja jamani kwani hamuelewi? Amejificha tu kwenye kwapa na mbawa za vyombo vya dola, nje ya hapo mimi nafuu
 
Kuna Watu wengine sijui huko Vyuoni mlienda Kufanya nini. Hivi Mtanzania Kuhojiwa 'Hardtalk' ndiyo 'Justification' kwamba ni 'Mwerevu' sana au?
NDIYO. kama unabisha mwambie Jiwe aende kama atakukubalia. Hajui hata nchi yetu ilipata uhuru mwaka gani. Kwenya anga za kidiplomasia jiwe ni sifuri
 
NDIYO. kama unabisha mwambie Jiwe aende kama atakukubalia. Hajui hata nchi yetu ilipata uhuru mwaka gani. Kwenya anga za kidiplomasia jiwe ni sifuri

'Kwenya' ndiyo Kiswahili gani na cha wapi hiki? Angalia ulivyo 'Popoma' yaani unamcheka JPM huku na Wewe tena 'Unachapia' tu hapa Mubashara.
 
Kitu pekee ambacho nakijua tu ni kwamba kama Wewe siyo Mwerevu ( Intelligent ) kabisa huwezi Kusoma Chuo Kikuu changu bora mno cha SAUT.

Nashukuru SAUT kuwepo maana bila wao washkaji waliofeli wangekosa chuo cha kusoma na leo wasingekuwa kwenye ajira zao..
 
Anaweza akawa amehojiwa na vituo vingine vidogo lakini ukweli unabaki pia amehojiwa kwenye Hardtalk. Kwa sasa sioni mwanasisa mwenye ubavu wa kwenda kuhojiwa kwenye Hardtalk zaidi ya Lissu. Hawa wanasiasa wa Bongo bora tu waendelee kuulizwa maswali laini na waandishi uchwara wa Bongo kuliko kwenda kuwa kichekesho mbele ya dunia.

Kwanza ;....
Napinga kuwaita waandishi wa habari Tz kwamba ni uchwara!! Hata nusu ya yale wanayopitia wewe binafsi huwezi chomoka!!

Pili;....
Kukaa meza moja ya mahojiano na Kaka Tundu ni sawa na kujitoa muhanga! Manake atavuka mipaka bila tahadhari wakati mwisho wa siku unawajibishwa wewe(mtangazaji!!)

Mwisho wa siku tuheshimu taaluma za watu!!

Uwepo wa makanjanja kwenye tasnia ya Habari na maudhui yake hakuondoi uhalisia wa hali halisi!!

Hebu tujifunze then turudi kwa wana habari!!

***Ignorance of the society ain’t the ignorance of the whole society!!!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom