Ukimuacha Tundu Lissu, hivi kuna Mtanzania mwingine ameshawahi kuhudhuria kipindi cha HardTalk?

Lisu amesomea Lugha kwahiyo watu wa kumfananisha nao lakini wamemwacha mbali sana ni hawa akina Tulia Ackson na Palamagamba Kabudi.

Mtu wa sayansi ngeli inamsaidia nini?! Tatizo hapo Ufipa hakuna wanasayansi wamejazana watu wa " Tokomeza Kisarawe" watupu!
Unathibitisha kuwa Jiwe lugha inampiga chenga?
 
Nakumbuka enzi zetu kama umefeli umepata Div III basi watu wanakushauri uombe SAUT.. Div I wote huwa tunaomba UDSM tuu maaana lazima tupate tuu

Kitu pekee ambacho nakijua tu ni kwamba kama Wewe siyo Mwerevu ( Intelligent ) kabisa huwezi Kusoma Chuo Kikuu changu bora mno cha SAUT.
 
James Martin,

Inaonekana umeanza kuisikia Hardtalk mwaka 2019 ndiyo maana umekuja na huu uzi. Tukusaidie HardTalk kilianza mwaka 1997, na aliyekua anahoji ni Broadcaster nguli Tim Sebastian, Lissu angeonana na Tim angechanganyikiwa zaidi ya pale alipokutana na Stphen Sackur. Halafu kuna watanzania wengi wamehojiwa na programme kubwa hata kabla ya hii Hardtalk mmojawapo Mzee Nyerere alipohojiwa na Johnathan Dimbleby. Kuna mtu anaitwa Martni Neil wa BBC pia hawa ni magwiji wa habari wa BBC siyo Stephen Sackur. Angeonana na hao watu wangemmaliza zaidi. Mkapa alihojiwa na Tim Sebastian wa HardTalk mwaka 2001
 
Attachments

  • 1597648309767.png
    1597648309767.png
    18.1 KB · Views: 1
Kitu pekee ambacho nakijua tu ni kwamba kama Wewe siyo Mwerevu ( Intelligent ) kabisa huwezi Kusoma Chuo Kikuu changu cha SAUT.
hawa jamaa wanamfanya marehemu baba yangu aliyeishia darasa la pili aonekane Profesa. Yaani mtu anathubutu kuweka uzi hapa sababu tu Lissu kahojiwa na HardTalk, kipindi ambacho hapa UK watu hata hawakiangalii sababu siyo muhimu. Ukiona time slot ya kipindi hakipo Prime Time ujue hawana muda nacho. Kama wanataka waingereza wamuone mwanasiasa yeyote basi atahojiwa katika kipindi kiitwacho News Night ambacho kinarushwa baada ya taarifa ya habari ya saa nne usiku. Ama wamamuhoji katika kipindi cha Andrew Marr cha jumapili saa mbili ya asubuhi. Hiyo HardTalk wanaioiangalii ni watu kama huyu mtoa habari na na wengine nje ya UK
 
James Martin,

Weka Clip ya Tundu Lissu akihojiwa na Chris Cuomo ama Don Lemon basi tuone? ama hata akihojiwa na Rachel Madow wa MSNBC. Huizo TV alizohojiwa USA ni kama hizi za kina Mirad Ayo tu
 
Tunaomba hawa walio hai
Akishakufa anaacha kuwa mtanzania? Mentality zetu zina kasoro sana. Tunataka kuwafurahisha wazungu tu. Si mhamie Ulaya mtuache na Tanzania yetu? Nani kasema kipimo cha kuwa sawa ni lazima ufurahishe wazungu? Yes tumeona haya haya tena wakati wa Corona. Na Mwenyezi Mungu amewaaibisha, maana wanakufa kama kuku wa mdondo pamojana science yao
 
weka clip aliyohojiwa na CNN
Halafu Kikwete si alihojiwa na CNN na mwanamama Christiana Amanpour ama Hardtalk ndiyo kipindi special. Mkiambiwa mashokolo mageni mtakasirika? Mmeanza tu kukifahamu kipindi cha hardtalk sababu ya Lissu ndiyo maana mnakiona kipindi kikubwa sana lakini hamhujui kuna vipindi vingi zaidi ya hicho.
 
Hawa watu tuwaonee huruma tu. Sera sasa hivi ni kuhojiwa na Hardtalk ama kuzungumza kiingereza kwenye mdahalo hakuna kitu kingine wafuasi wa CDM wanakijua na ndiyo maana watapigwa chini uchaguzi huu
 
Mwal. Nyerere alisema hizo ni dalili za kufilisika..ukianza kujivunia au kujisifia vitu vya kijingajinga kama ukabila, udini, kuhojiwa hardtalk..n.k

TL amehangiaka weee, mwisho wa yote amerudi pale alipoanzia. Ameacha wazungu wanapambana na Corona yao, pamoja na kwamba wamefanya interview ya hardtalk. A lot of hopeless people in that party. Khaaa
 
Halafu Kikwete si alihojiwa na CNN na mwanamama Christiana Amanpour ama Hardtalk ndiyo kipindi special. Mkiambiwa mashokolo mageni mtakasirika? Mmeanza tu kukifahamu kipindi cha hardtalk sababu ya Lissu ndiyo maana mnakiona kipindi kikubwa sana lakini hamhujui kuna vipindi vingi zaidi ya hicho.

Ndio point zao kwanini TL anafaa kuwa Rais. Yaani utopolo mtupu.
TL aendelee kufanya mahojiano tu. Ila hana sifa za kuwa Rais.
 
Akishakufa anaacha kuwa mtanzania? Mentality zetu zina kasoro sana. Tunataka kuwafurahisha wazungu tu. Si mhamie Ulaya mtuache na Tanzania yetu? Nani kasema kipimo cha kuwa sawa ni lazima ufurahishe wazungu? Yes tumeona haya haya tena wakati wa Corona. Na Mwenyezi Mungu amewaaibisha, maana wanakufa kama kuku wa mdondo pamojana science yao
Mapovu yote haya ni kwa ajili ya hiyo sentensi yangu moja ?
 
Bora kutoenda kabisa kuliko kwenda kuchuma aibu. Hii kitu ilimusanya Tundu Lissu akakili ushoga bila yeye kutarajia.
 
hawa jamaa wanamfanya marehemu baba yangu aliyeishia darasa la pili aonekane Profesa. Yaani mtu anathubutu kuweka uzi hapa sababu tu Lissu kahojiwa na HardTalk, kipindi ambacho hapa UK watu hata hawakiangalii sababu siyo muhimu. Ukiona time slot ya kipindi hakipo Prime Time ujue hawana muda nacho. Kama wanataka waingereza wamuone mwanasiasa yeyote basi atahojiwa katika kipindi kiitwacho New Night ambacho kinarushwa baada ya taarifa ya habari ya saa nne usiku. Ama wamamuhoji katika kipindi cha Andrew Marr cha jumapili saa mbili ya asubuhi. Hiyo HardTalk wanaioiangalii ni watu kama huyu mtoa habari na na wengine nje ya UK

Sasa si bora waende kwenye Hardtalk ambayo haipo kwenye prime time kuliko kwenda kuaibika kwenye prime time programmes zinazoangaliwa na watu wengi?!
 
Back
Top Bottom