Ukimtongoza mwanamke akakujibu nipe muda nikufikirie, mwanaume unatakiwa kufanya nini ili upate jibu zuri?

SuperHb

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
897
697
Habari zenu ndugu zangu...

Kama kichwa cha habari kinavyooeleza...

Kidume ushapiga sounds zako, umeeleza hisia zako kinaga ubaga kwa Demu halafu Demu anakwambia "NITAKUPA JIBU NGOJA NIKUFIKIRIE"... Hapo kweli kuna matumaini mazuri ?

Je, Kidume ukishaambiwa hivyo inabidi uendelee kumsumbua kukupa jibu au unakausha mpaka pale atakapojisikia kukupa jibu?

Karibuni...
 
Kwenye heading kuna tatizo

Ila cha kufanya wewe endelea na maisha tu umpe muda wa kuchakata sera zako, ni kama vile unavyoomba kazi hujibiwi hapohapo umepata kuna muda kidogo then ndiyo unapata majibu
inamaana hata ukikutana nae...ni salamu tu...ayo mambo ya kukumbushia jibu unakaushia?..na je kama una namba zake unakausha humtext wala kumpigia kukumbushia??..
 
Ukishaambiwa hivyo 97℅ ni ushakubaliwa kinachotakiwa ni kujiongeza tu. Ila kuwa makini wengi siku hizi wanaweka huo mtego wa nakufikiria halafu unaanzwa kuhenyeshwa na vibomu vya haja. Baadae anakukataa😀😀

Wa kukukataa huwa anakukataa saa hiyo hiyo.
 
Kama ilivyo binadamu wote tunatofautiana, wanawake pia wanatofautiana!.. Kuna mwengine akikuambia hivyo anakupima inategemea namna anavyodhani,anataka umsumbue! I mean usumbuke juu yake.. yeye hiyo anaichukulia kama upendo!
Wengine hawataki uwasumbue hususani wale ambao wapo busy na mambo yao anakuona Kama mzinguaji!!

Jibu ni moja hakuna kanuni maalum mkuu ila utaipata kanuni hiyo ukimjua vyema aliekusubirisha.
 
ukishaambiwa hivyo 97℅ ni ushakubaliwa kinachotakiwa ni kujiongeza tu. Ila kuwa makini wengi siku hizi wanaweka huo mtego wa nakufikiria halafu unaanzwa kuhenyeshwa na vibomu vya haja. Baadae anakukataa😀😀

Wa kukukataa huwa anakukataa saa hiyo hiyo.
asante kwa madini yako mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom