Ukimsikiliza Jumanne Kishimba mbunge wa Kahama, unajua kwanini Musukuma anawadharau wasomi wetu

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Kusema ukweli tukipata watu wenye uwezo wa kufikiri kama huyu mheshimiwa, nchi hii itaenda mbali sana.

Bahati mbaya sana kwa wasomi wetu wengi wamebaki na vyeti na wamekuwa wakitambia hivyo huku kichwani wakiwa watupu kama kama roboti iliyokuwa programmed tu na hawafikiri tena nje ya box.

Kwa bahati mbaya ukweli kwamba wengi wamepata hizo digrii kimagumashi na hawana walichobaki nacho kichwani baada ya kumaliza chuo, huwa hausemwi.

Ukimsikia mheshimiwa Kishimba mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, akiwa darasa la saba tu, jinsi ambavyo amegusa wasomi wanaojielewa na kufikia kumwita jina profesa, utajua kwa nini King Musukuma anawadharau sana wasomi wetu.

Tafuta mchango wa jana wa Mh. Kishimba utaona jinsi tusivyoweza kuziona fursa za uwekezaji kwa upana wake.
 
Subiria umwagiwa upupu na matusi mazito kutoka hapa maana jamii forum 98.4% ni graduates, Drs, na Phd!

Elimu ya Tanzania inazalisha maroboti tu. Kuna wakati JPM aliwahi kulinganisha uwezo wa kiakili wa Mh. Kishimba na Mtumishi wa Wizara ya Nishati na Madini mwenye Phd kwenye mbinu ya kutathmini thamani ya dhahabu/almasi kulingana na soko na kuonyesha Kishimba yupo juu zaidi pamoja na kuwa aliishia "STD 3"

Nina mradi wangu hapa ambao mwakani naweza kuanza kuajili na nimechagua kutumia mbinu hii.... bila kujali vyeti vyako nitakulipa nusu ya mshahara kwa mwaka mmoja ambapo kwa kipindi chote usipoweza kubuni kitu kipya cha kuendeleza kiwanda na utendaji wa kazi kwa ujumla hesabu huna kazi.
 
Ukweli usemwe
 
Kama walioishia Darasa la Saba,wanauwezo mkubwa kuriko wanazuoni wenye shahada na kuendelea,Basi waende kwenye zahanati zote wawe madakitari(maana Kuna upungufu),waboreshe kilimo Cha sukari,mafuta,maana wengi wako huko na hayo mazao Bado tunaagiza kutoka nje,

Waje watuanadalie utafiti jinsi ya kuondoa tatizo la ajira.
Ukienda Mloganzira,Muhimbili,Bugando,Itakuwa vzr Hawa Darasa la Saba tuwaachie ofisi na shughuri za kibingwa wafanye wao.
 
Ninaowateua Wameshindwa Kufikiria Nje Ya Box
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Akiwa Kondoa, Aliongea Kuhusu Maji, 2020

Hatuwezi Kuwasaidia Wananchi Wetu Kuhusu Changamoto Ya Maji Hapa Bahi Kwa Yale Tuliyosoma, Details Design,

Tuchukue Caterpillar Tuchimbe Bwawa Kubwa
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Akiwa Bahi 2021
 
Nchi vululu vululu, kila kitu shaghala baghala

Kazi anayofanya Prof na anayofanya alieshia Darasa la Tatu haina tofauti katika ubora

Mawazo yao wote sawa sawa tofauti mmoja ana mbwembwe za kunukuu misemo na nukuu za wataalam wa zamani kwa lugha ya kigeni

Nani ana mzuka wa kujua tofauti ya Kielimu kati ya Prof Muhonga Prof bingwa wa Miamba Duniani na Jumanne Kishimba au kibajaj Bungeni?
 
Kusema ukweli tukipata watu wenye uwezo wa kufikiri kama huyu mheshimiwa, nchi hii itaenda mbali sana.

Bahati mbaya sana kwa wasomi wetu wengi wamebaki na vyeti na wamekuwa wakitambia hivyo huku kichwani wakiwa watupu kama kama roboti iliyokuwa programmed tu na hawafikiri tena nje ya box.

Kwa bahati mbaya ukweli kwamba wengi wamepata hizo digrii kimagumashi na hawana walichobaki nacho kichwani baada ya kumaliza chuo, huwa hausemwi.

Ukimsikia mheshimiwa Kishimba mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, akiwa darasa la saba tu, jinsi ambavyo amegusa wasomi wanaojielewa na kufikia kumwita jina profesa, utajua kwa nini King Musukuma anawadharau sana wasomi wetu.

Tafuta mchango wa jana wa Mh. Kishimba utaona jinsi tusivyoweza kuziona fursa za uwekezaji kwa upana wake.
Kishimba ana facts zenye malalamiko /manung'uniko ila anapungukiwa na baadhi ya facts.

Ana-advocate watoto kuto vaa viatu. Nadhani hapa ndipo changamoto ya kufikiri inapoanzia na isipokuwa well handled Kishimba anaweza kuonekana hero, yet atatengeneza umasikini wa kifikra za kimfumo hasa kwa small scale farmers wa vijijini.

Kishimba anakandia kuvaa viatu akidai ni gharama isiyo ya lazima na haina uhusiano na masomo. Je yeye huwa anapekua au anavaa viatu?
Wanae wanapekua au wanavaa viatu?

Basic knowledge ya sayansikimu shule ya msingi.
Tunavaa viatu ili
Magonjwa say watoto wakiingia chooni
Kujikinga na wadudu watoto wakitembea kwenda shule, wakiwa shule au wakiwa wanaelekea nyumbani.
Tunavaa viatu ili kujikinga na miiba, mbigili misumari ambayo ikimchoma mtoto miguuni akaumia, tiba inaweza kuongeza gharama kuliko thamani ya viatu ambayo ni sh. 20,000

Tunavaa viatu ili kuwa na sare, watoto wakizea kuwa na sare na unadhifu inajenga nidhamu, leo na kesho baadhi yao wakiwa wanajeshi msingi wa kuvaa sare na unadhifu unakuwa ushajengwa.

Kishimba anatakiwa ku-advocate wakulima walime zaidi na kuzalisha ili kumudu basics kama viatu.

Ninaunga mkono hoja yake ya elimu ambayo watoto wanasoma mpaka Chuo kikuu then wanakutana na dunia ambayo maarifa ya shule na chuo hayawezi kumfanya aikabili.

Hili la kuwa na wasomi wengi then walichosoma hawana sehemu ya kufanyia kazi ni tatizo ambalo Africa litazidi kumea unless tuje na suluhisho la pamoja.

Nitoe mfano wa Japan.
Japan ina population ya 123 mil

Kwa mujibu wa World Economic Forum karibu nusu ya raia wa Japan wanafanya kazi. Na kuna woga working class itapungua kwa asilimia 8 ifikapo 2040.

Japan inaingia mara 2.5 kwa Tanzania.
Hawana mafuta, gas, madini, ardhi suitable ya kilimo kama yetu, vivutio vya utalii asilia.

Tunakwama wapi; sio Kishimba, sio Waziri wa Kazi anafikiri nini kifanyike ili kutengeneza mifumo jumuishi ambayo itazalisha kazi.

Leo tukija na mifumo jumuishi tukawa na mifumo ya uzalishaji wa bidhaa na huduma ambayo kwa wastani kila organized system ambayo itakuwa kampuni itazalisha ajira 100-500;
Tanzania ya neema utawezekana.

Ili tufikie hapo lazima tuwe na elimu inayofukunyua fikra za nini tufanye ili madini, gas, maliasili, mazao ya kilimo, mifugo, nyuki na uvuvi vitagusa mahitaji ya dunia tokea Tanzania na mauzo yake ndio solution.

Sio sawa tunanunua Toyota mpya na used toka Japan halafu sisi hatujawa na fikra za tunawezaje kuuza Samaki wa maji baridi kama Sangara au Sato tokea hapa kwenda Japan.

Kama elimu yetu itaendelea kuwakaririsha watoto
A for apple au Gavana wa mwisho wa Uingereza Tanganyika ni Richard Turbull; tutabaki tunashangaa speech ya Kishimba akisikitika kwanini watoto hawali mihogo, mbute na mayai instead wanataka chips, sausage na mayai.

Wasalaam
 
Kama walioishia Darasa la Saba,wanauwezo mkubwa kuriko wanazuoni wenye shahada na kuendelea,Basi waende kwenye zahanati zote wawe madakitari(maana Kuna upungufu),waboreshe kilimo Cha sukari,mafuta,maana wengi wako huko na hayo mazao Bado tunaagiza kutoka nje,

Waje watuanadalie utafiti jinsi ya kuondoa tatizo la ajira.
Ukienda Mloganzira,Muhimbili,Bugando,Itakuwa vzr Hawa Darasa la Saba tuwaachie ofisi na shughuri za kibingwa wafanye wao.
Wewe ni zwazwa tu, hivi unajua water for injection inayotumika ku-dilute penadul ya kukutibu kaswende inanunuliwa kutoka India na China, maji ya sindano tu! Alafu tuna wafamasia wengi Sana!
Hao ndio maroboti wetu wanaotibu wagonjwa wetu hapa Tanzania
 
@Freddie Matuja kishimba hoja yake ni kwa nini iwe lazima kuvaa viatu vyeusi wakati rangi hiyo ya viatu ni gharama kubwa, na wakati kuna viatu vya rangi nyingine vyenye gharama nafuu na mzazi ataimudu na mtoto atasoma vizuri kuliko kulazimisha tu viatu vyeusi kwani rangi nyeusi inachangia nini kwenye ubongo wa mtoto?
 
Kishimba alisema pia kwa nini mtoto aende shuleni saa kumi na mbili asubuhi halafu ashinde huko na njaa anarudi saa kumi jioni hata aliyosoma ashayasahau maana ukiwa na njaa huwezi kuelewa hata masomo yenyewe, akashauari tujitahidi kurekebisha muda walau watoto asubuhi wafanye mambo mengine halafu mzazi ajipigepige ili mtoto aende shuleni saa tano mchana akiwa amepata japo chakula na itamsaidia sana kuelewa hata masomo.
 
Kama walioishia Darasa la Saba,wanauwezo mkubwa kuriko wanazuoni wenye shahada na kuendelea,Basi waende kwenye zahanati zote wawe madakitari(maana Kuna upungufu),waboreshe kilimo Cha sukari,mafuta,maana wengi wako huko na hayo mazao Bado tunaagiza kutoka nje,

Waje watuanadalie utafiti jinsi ya kuondoa tatizo la ajira.
Ukienda Mloganzira,Muhimbili,Bugando,Itakuwa vzr Hawa Darasa la Saba tuwaachie ofisi na shughuri za kibingwa wafanye wao.
Kuwa mpole acha jaziba
 
Umepaniki bro.

Ni vile hujui kuwa corona wameachiwa wao ndio wawe starring?

Kwamba waende huko unakotaka kwani ni sokoni?Hujui kuwa kuna sheria zinazowalinda watu wenye cheti ndio wafanye huko?Hujui wao wameruhusiwa kisheria kumfanyia majaribio ya upasuaji binadamu hata kama itagharimu maisha yake?Unadhani hatujui intern doctors wanayofanya?
Kama walioishia Darasa la Saba,wanauwezo mkubwa kuriko wanazuoni wenye shahada na kuendelea,Basi waende kwenye zahanati zote wawe madakitari(maana Kuna upungufu),waboreshe kilimo Cha sukari,mafuta,maana wengi wako huko na hayo mazao Bado tunaagiza kutoka nje,

Waje watuanadalie utafiti jinsi ya kuondoa tatizo la ajira.
Ukienda Mloganzira,Muhimbili,Bugando,Itakuwa vzr Hawa Darasa la Saba tuwaachie ofisi na shughuri za kibingwa wafanye wao.
 
Kusema ukweli tukipata watu wenye uwezo wa kufikiri kama huyu mheshimiwa, nchi hii itaenda mbali sana.

Bahati mbaya sana kwa wasomi wetu wengi wamebaki na vyeti na wamekuwa wakitambia hivyo huku kichwani wakiwa watupu kama kama roboti iliyokuwa programmed tu na hawafikiri tena nje ya box.

Kwa bahati mbaya ukweli kwamba wengi wamepata hizo digrii kimagumashi na hawana walichobaki nacho kichwani baada ya kumaliza chuo, huwa hausemwi.

Ukimsikia mheshimiwa Kishimba mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, akiwa darasa la saba tu, jinsi ambavyo amegusa wasomi wanaojielewa na kufikia kumwita jina profesa, utajua kwa nini King Musukuma anawadharau sana wasomi wetu.

Tafuta mchango wa jana wa Mh. Kishimba utaona jinsi tusivyoweza kuziona fursa za uwekezaji kwa upana wake.

Jamaa huyu hapa, msikilizeni...

Upogo wa hoja yake uko kwenye ishu ya "sare ya shule" tu. Otherwise kwa mengine yote ametoa hoja za msingi sana...

Amenifurahisha sana anapomuuliza Waziri wa Elimu ampe "definition" ya "Education"..

Yeye anashangaa kwa sababu yeye anaelewa maana ya " EDUCATION " ni Busara, Maarifa, Ujuzi na Ufahamu wa mtu...

Lakini kiserikali wao wanajua kuwa, "EDUCATION" maana yake ni "vyeti - Makaratasi"

Yeye ana watoto wake 6 na wote wana vyeti vya "digrii" lakini hata haoni namna ambavyo "digrii" hizo zinaweza kuwatoa hatua moja ya maisha kwenda hatua nyingine ya juu....

Tukumbuke kuwa Kishimba ni mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio huko Kahama. Kiwango chake cha elimu sijui hata kama alimaliza darasa la saba...

Lakini ana manage makampuni yalio ajiri mamia ya wafanyakazi. Nadhani akitazama mafanikio yake yeye mtu binafsi mmoja na akitazama dude kubwa kama serikali lenye wasomi wenye "madigrii - makaratasi" lakini tuko hivi, anachoka kabisa na anashindwa kabisa kuona hata maana ya "madigrii" hayo...!!!
 
Kama we ni msomi na hujamwelewa Kishimba,ni hasara kubwa sana kwa taifa.
Kishimba hajakataa wasivae viatu,ila kwa nini viatu "vyeusi" kwani akivaa viatu vyovyote hatapata hiyo elimu?

Kama ni msomi hujawaza hata ushauri juu ya uwekezaji alioutoa..bali umewaza viatu tu...kweli naamini hizi elimu zinaua fikra na kuwafanya watu wapumbavu zaidi
Kishimba ana facts zenye malalamiko /manung'uniko ila anapungukiwa na baadhi ya facts.

Ana-advocate watoto kuto vaa viatu. Nadhani hapa ndipo changamoto ya kufikiri inapoanzia na isipokuwa well handled Kishimba anaweza kuonekana hero, yet atatengeneza umasikini wa kifikra za kimfumo hasa kwa small scale farmers wa vijijini.

Kishimba anakandia kuvaa viatu akidai ni gharama isiyo ya lazima na haina uhusiano na masomo. Je yeye huwa anapekua au anavaa viatu?
Wanae wanapekua au wanavaa viatu?

Basic knowledge ya sayansikimu shule ya msingi.
Tunavaa viatu ili
Magonjwa say watoto wakiingia chooni
Kujikinga na wadudu watoto wakitembea kwenda shule, wakiwa shule au wakiwa wanaelekea nyumbani.
Tunavaa viatu ili kujikinga na miiba, mbigili misumari ambayo ikimchoma mtoto miguuni akaumia, tiba inaweza kuongeza gharama kuliko thamani ya viatu ambayo ni sh. 20,000

Tunavaa viatu ili kuwa na sare, watoto wakizea kuwa na sare na unadhifu inajenga nidhamu, leo na kesho baadhi yao wakiwa wanajeshi msingi wa kuvaa sare na unadhifu unakuwa ushajengwa.

Kishimba anatakiwa ku-advocate wakulima walime zaidi na kuzalisha ili kumudu basics kama viatu.

Ninaunga mkono hoja yake ya elimu ambayo watoto wanasoma mpaka Chuo kikuu then wanakutana na dunia ambayo maarifa ya shule na chuo hayawezi kumfanya aikabili.

Hili la kuwa na wasomi wengi then walichosoma hawana sehemu ya kufanyia kazi ni tatizo ambalo Africa litazidi kumea unless tuje na suluhisho la pamoja.

Nitoe mfano wa Japan.
Japan ina population ya 123 mil

Kwa mujibu wa World Economic Forum karibu nusu ya raia wa Japan wanafanya kazi. Na kuna woga working class itapungua kwa asilimia 8 ifikapo 2040.

Japan inaingia mara 2.5 kwa Tanzania.
Hawana mafuta, gas, madini, ardhi suitable ya kilimo kama yetu, vivutio vya utalii asilia.

Tunakwama wapi; sio Kishimba, sio Waziri wa Kazi anafikiri nini kifanyike ili kutengeneza mifumo jumuishi ambayo itazalisha kazi.

Leo tukija na mifumo jumuishi tukawa na mifumo ya uzalishaji wa bidhaa na huduma ambayo kwa wastani kila organized system ambayo itakuwa kampuni itazalisha ajira 100-500;
Tanzania ya neema utawezekana.

Ili tufikie hapo lazima tuwe na elimu inayofukunyua fikra za nini tufanye ili madini, gas, maliasili, mazao ya kilimo, mifugo, nyuki na uvuvi vitagusa mahitaji ya dunia tokea Tanzania na mauzo yake ndio solution.

Sio sawa tunanunua Toyota mpya na used toka Japan halafu sisi hatujawa na fikra za tunawezaje kuuza Samaki wa maji baridi kama Sangara au Sato tokea hapa kwenda Japan.

Kama elimu yetu itaendelea kuwakaririsha watoto
A for apple au Gavana wa mwisho wa Uingereza Tanganyika ni Richard Turbull; tutabaki tunashangaa speech ya Kishimba akisikitika kwanini watoto hawali mihogo, mbute na mayai instead wanataka chips, sausage na mayai.

Wasalaam
 
Maendeleo sio rahisi kama tunavyoataka kuamini. Una uhakika haya mambo anayaongea wasomi hawajawahi kuyafanyia utafiti na kutoa ushauri?

Mtu kuna tajiri kama Kishimba sio lazima uwe na elimu, lakini hiyo haina maana kwamba elimu(usomi) sio kitu cha lazima kwenye jamii. Elimu ya watu utaona impact yake kama itatumika, isipotumika ni kama panga lenye makali lililopo kabatini, unalilaumu kwanini halikati miti.
 
Back
Top Bottom