MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kwa sisi tuliokulia mazingira ya karibu na hifadhi za wanyama tulikua tukifundwa na wazee wetu kua unapokua unachunga ng'ombe ukipita mahali porini ukamwona simba amelala, kama anakuangalia akikukodolea macho wewe mfuate huko ukimtazama machoni hata kama huna silaha, ataamka taratibu, akikuonea aibu,atakimbia na kuondoka zake.
Kwa muktadha huo, kama umemona simba amelala porini huku macho yako wazi akikutazama halafu wewe ukaanza kukimbia hovyo huku ukipiga kelele basi utakua unajitaftia matatizo! atakuona mwoga, atakuona usiyejiamini, hivyo kama simba huyo ana njaa akishagundua madhaifu yako basi ataamka atakufua pamoja na kelele zako zote kokote utakapokimbilia ili akukamate na kukugeuza kitoweo.
Simba akishakuona unamkodolea macho huku ukimfuata alipolala atajiuliza kua huyu binadamu anaujasiri gani kiasi cha kunifata huku nilipo? huenda akawa na nia ya kunidhuru, huenda akawa yuko tayari kwa lolote na mimi. Simba akishagundua hilo kama alikua amelala kwenye nyasi ndefu huamka na kutumia mbio akimwogopa binadamu.
Kama kuna binadamu wa aina ya yule asiyeogopa simba kwa kuangalia historia yake au desturi ya maisha yake, basi mwanadamu huyu safari ya mafanikio yake hua ni fupi sana! Hawezi kuchelewa kufika anapopataka kwa maana ya kutotishwa na mingurumu ya sauti za simba, humnyookea simba akiwa amelala akiwa amelala hata kama hana silaha yeyote itakayomkinga na madhara yeyote ili mradi tu simba akubali yaishe.
Kwa binadamu asiyekua na ujasiri akisikia tu neno simba huishiwa na pumzi haraka hajauona, mapigo ya moyo huenda mbio yakiambatana kijasho chembamba.Siku akimuona ana kwa ana hutamani hata ardhi ipasuke, hata kama akisikia sauti ama akiangalia picha huishia kupiga kelele ambazo huambatana na ndoto zenye kumtisha.
Ninachotaka kumaanisha hapa ni kwamba... katika maisha yako ya kisiasa macho yasikutie woga kutaka kuthubutu jambo, Mwangalie simba kisha mfuate alipo ataondoka tu.