Ukimjulia Rais Magufuli utajua kwanini lazima Upinzani utoweke nchini

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Wadau, wengi wanauliza ni kwa nini Rais Magufuli anachukia Upinzani kiasi cha kufanikisha Bunge kugeuka kuwa Halmashauri Kuu ya CCM, NEC.

Ukweli ni kwamba Magufuli si rafiki na watu weupe na product yoyote inayotoka huko. Mengine anakubali tu kwa kuwa hakuna alternative. Lakini angetamani kila kitu kiwe cha Afrika.

Kwa asili ya demokrasia ya vyama vingi ni product kutoka uzunguni uliosokomezwa kwetu na "wajomba" bila ridhaa yetu.

Kwa mantiki hiyo, Magu anapopambana na bidhaa za wazungu ni pamoja na mfumo wa upinzani. Hivyo, Chadema lazima kife kifo cha mende.

#HachanjwiMtuHapa
 
Hamtaki kutoa hela kununua chanjo wala sio shida ya chanjo semeni kweli
 
Hachukii weupe kwa falsafa, bali ni mtu asiyependa kuhojiwa na ni mlevi wa madaraka, hivyo kwake yeyeto asiyekubaliana na utashi wake na anayeweza kuhoji maamuzi yake, anakuwa na chuki naye automatically. Kama angekuwa na chuki na watu weupe, basi hata wachina ni weupe, hivyo alipaswa kuwachukia. Kwa ujumla ni mlevi mwenye kiburi cha madaraka, na sio zaidi ya hapo.
 
Magufuli ni mtu mwenye uelewa finyu, ambaye hawezi kuhimili hoja nzito. Watu wa aina yake hujenga chuki nafsini dhidi ya wenye hoja tofauti na wao. Wakiwa na nafasi ya mamlaka, basi hutumia mamlaka hayo kukandamiza hoja.
Hata hivyo upinzani si Chadema wala ACT Wazalendo pekee. Umo mioyoni mwa mamilioni ya watu. Hauwezi kufa kwa kuwa Magufuli anaitumia mabavu; la, hasha!
 
Mkuu tafuta kazi ya kufanya, Hapa mtandaoni hakuna atakayekulipa

Hata ccm hawakufahamu, unapoteza muda wako bure, Fanya kazi

Hakuna malipo ya kuandika habari za ccm, unapoteza muda wako
 
Upinzani hauwezi kuawa kwa kuwa hata serikali inauhitaji ndiyo maana Leo akina mdee wako bungeni.
 
Hii nchi ujinga bado ni tatizo kubwa sana.

Sishangai tumiemdelea kua masikini wa kutupwa miaka 60 ijayo tena.

Utashangaa mtoa mada ana mume na watoto wanamtegemea kwa mawazo na ushauri. Wanaume kazi tunayo.
 
Upinzani wa kwetu ulienda mbaaali Sana, kiasi cha kuwazidi hata waliotuletea!!

Upinzani wa kwetu hapa Africa sio wa kistarabu na uzalendo wake ni wa mashaka makubwa, upo tayari kuuza nchi! Ni Bora tuanze upya
 
Zilikuwa nyakati za giza sana.

Back
Top Bottom