Ukimgonga Twiga mwenye mimba hadi akafa adhabu yake ni nini?

Mzee wa vijisenti aligonga mtu kwa gari akalipishwa 700,000/=,kwa maana hiyo Twiga anathamani kuliko binadamu.
 
TEMBO = USD 15,000 ~ mil 34.6 NYATI = USD 1,900~ mil 4.3 SIMBA = USD 4,900~ mil 11.3 CHUI = USD 3,500~ mil 8 TWIGA = USD 15,000~ mil 34.6 FISI = USD 550~ mil 1.2 NGIRI = USD 450~ mil 1 NYANI = USD 110~ laki 254 PUNDAMILIA = USD 1200~mil 2.7 SWALA = USD 390~ laki 9 ukipata ajali ndani ya mbuga Tsh 200,000 ukizidisha mwendo faini yake ni Tsh . 30,000/= . .

Sijui twiga mwenye mimba na yeye ana charges zake au vipi
Itakua milioni 34 na nusu yake yaani 17 M
Jumla 51M
 
Hapo ukiangalia haraka unaona dereva hana kosa na gari haikua speed ila inaonesha twiga alikua anakimbia au alivuka ghafla......kama gari ingekua speed bas isingesimama hapo na ingeharibika vibaya na kudondoka....issue sio kugonga twiga...wanaangalia na ajali imetokeaje kwanza
 
Hivyo akiwa kwake ni haki yake kutugongea magari yetu, kama ni hivyo kulikuwa na sababu gani kuruhusu barabara ipite mikumi ikiwa watumiaji hatuna haki na wajibu??

Gari ipo 20 igongwe na twiga ikunjike hivyo?!!!!
 
hio impact hapo sio 20kph angalia vizuri mkuu
Wadau msihukumu kwa kutazama upande mmoja kuna uwezekano dereva hana kosa lolote na hata kama lipo ni mpaka mahakama idhibitishe....

Hamjiulizi ikiwa twiga ndie kaligonga gari itakuaje?

Tuseme dereva alikuwa speed 20 ghafla twiga katokea anakimbizwa na mnyama mkali then kalivaa gari! Hapo dereva anakosa gani?

Endapo dereva akijitetea ndio alimuona twiga mapema na akasimamisha gari ila twiga ktk harakati za kujiokoa akalivaa gari nani atapinga? Huyo twiga hapo anajiteteaje? Ikiwa hilo eneo halina camera zilizoweza kurekodi hilo tukio utapingaje dereva hakusimamisha gari?

Jiulize kama binadamu na akili zake timamu anagonga treni vp kwa mnyama??
 
Bima inalipa
Izo sheria mbugani hazitumiki mkuuu
Yale ni makazi ya wanyama na ndio maana speed zimewekwa na mabango ya faini za wanyama endapo utagonga. """Kipepeo ukimgonga na ikathibitisha unalipa Tshs 24,000"""".
 
Gari ipo 20 igongwe na twiga ikunjike hivyo?!!!!
Unajua twiga alikuwa speed ipi na uzito wake?
Twiga hukimbia mbio fupi 35 miles kwa lisaa, sasa anapokuvaa ktk speed hiyo kwann asikusage sage?
 
Back
Top Bottom