Mwanaume ukimhudumia mwanamke mapenzi yanakuwa matamu sana

Habari wakuu,

Msinielewe vibaya na hiyo heading,nimekaa nimefikiria sana kuhusu kuboresha maenzi na hawa wanawake,kwa uzoefu wangu mdogo nilionao nimegundua kuna vitu vinapuuzwa ila vikifanywa,mwanamke anafurahi kwakua inakua very romantic,nakupa mfano,binafsi nilikua napenda sana misosi mitamu so nikajifunza kupika vyakula mbalimbali,hivyo ninapokua na mpenzi napenda kumpikia na kumuandalia kila kitu on the table,hiki kitendo huwa naona kabisa mwanamke anafurahia sana,na kuna vitu vingi vimezoeleka mwanaume ndo afanyiwe ila ukifanya kinyume na ukamfanyia mwanamke anafurahi,mfano ukimfulia anafurahi,badala ya yeye kubeba vitu vyako ukambebea mkoba anafurahi,badala ya yeye kukufunga kama za viatu mfunge yeye kiatu chake inakua romantic ndomana unaona vipicha vya mwanaume kumfunga kamba za viatu mwanamke vinazagaa sana kwasababu it looks ROMANTIC.

-Anko Jei

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiahangaike mkuu wewe mpe pesa tu akitoka pesa akakikaa pesa akilala pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu katika maisha usijitwishe kitu kama unahakika hauwez kumaintain au unafanya just kumridhisha siku ukiacha utapata tabu milawama isiyoisha
Ishi kama ulivyo mtu akupende the way ulivyo hata siku ukifanya ajue extra na sio mfumo wa maisha yako
 
Sina hakika sana kama wanaridhikaga.. ila ongeza juhud utafika unapotaka na utaona matokeo yake
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom