Mwanaume ukimhudumia mwanamke mapenzi yanakuwa matamu sana

ANKO JEI

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,278
2,364
Habari wakuu,

Msinielewe vibaya na hiyo heading,nimekaa nimefikiria sana kuhusu kuboresha maenzi na hawa wanawake,kwa uzoefu wangu mdogo nilionao nimegundua kuna vitu vinapuuzwa ila vikifanywa,mwanamke anafurahi kwakua inakua very romantic,nakupa mfano,binafsi nilikua napenda sana misosi mitamu so nikajifunza kupika vyakula mbalimbali, hivyo ninapokua na mpenzi napenda kumpikia na kumuandalia kila kitu on the table.

Hiki kitendo huwa naona kabisa mwanamke anafurahia sana, na kuna vitu vingi vimezoeleka mwanaume ndo afanyiwe ila ukifanya kinyume na ukamfanyia mwanamke anafurahi, mfano ukimfulia anafurahi,badala ya yeye kubeba vitu vyako ukambebea mkoba anafurahi, badala ya yeye kukufunga kama za viatu mfunge yeye kiatu chake inakua romantic ndomana unaona vipicha vya mwanaume kumfunga kamba za viatu mwanamke vinazagaa sana kwasababu it looks ROMANTIC.

-Anko Jei
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom