Ukimaliza kusoma hadi mwisho, jiulize wewe ni mtumwa wa nani?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
UKIMALIZA KUSOMA HADI MWISHO JIULIZE,
WEWE NI MTUMWA WA NANI?

Pamoja na kuishi kwenye dunia yenye uhuru mkubwa, bado watu wengi wanaishi maisha ya kiutumwa.

Watu wengi wanaishi maisha ambayo hawana uhuru wa kuamua wafanye nini na maisha yao.

Jambo lolote ambalo ni muhimu kwao kufanya, hawawezi kulifanya mpaka mtu au watu ambao amechagua kuwa mtumwa kwao walidhibitishe. Kama wakiona linafaa watamruhusu kufanya, na kama wataona halifai basi watamkataza kufanya.

Utumwa huu ni mbaya kuliko hata ule utumwa wa kulazimishwa na kupigwa. Kwasababu utumwa huu mtu anachagua mwenyewe na mara nyingi haelewi kama yupo utumwani. Vile vile adhabu anayopewa kwenye utumwa huu kama akienda kinyume na wanavyotaka wengine ni adhabu ya kiasaikolojia, lakini ni kali sana.

Je wewe umechagua kuwa mtumwa wa nani?

Ni mtu au watu gani ambao kabla hujafanya jambo ni lazima uwaambie na ukiwaambia chochote wanachosema wao ndio unafanya?

Ni mtu au watu gani ambao unapenda kila unachofanya wakifurahie, unaogopa ukifanya tofauti watakutenga?

Mtu au watu hawa ndio umeamua kuwa watumwa kwao. Wanaweza kuwa wazazi, wanaweza kuwa ndugu, jamaa na marafiki, pia inaweza kuwa jamii nzima.

Ukishajua wale ambao umeamua kuwa watumwa kwao unafanya nini? Unajiondoa kwenye utumwa huo. Na je unawezaje kujiondoa kwenye
 
Kumbuka ktk utumwa huo huenda kukatokea matokeo chanya au hasi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom