VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Wengi tunajua kuwa Balozi Bashiru Ally Kakurwa alikuwa kipenzi cha Mwendazake. Alianza naye kwenye ukaguzi wa mali za CCM na baadaye kumteua kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa. Na mwishoni, akamteua kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi. Jana, Balozi Bashiru ameteuliwa kuwa Mbunge. Hiyo ni njia ya kumuondoa Bashiru kisiasa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi. Pigo kwenye ngome ya Mwendazake.
Mwingine aliyeaminiwa na Mwendazake na wengi wetu kujua ni Suleiman Jaffo ambaye jana amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais. Jaffo alikuwa akisifiwa na Mwendazake kwenye utendaji wake TAMISEMI na hata kuoneshwa kama mfano wa kuigwa. Sasa TAMISEMI imekabidhiwa kwa mdogo wangu Ummy Mwalimu. TAMISEMI imeonekana inapwaya chini ya Jaffo aliyekuwa akionekana mahiri na Mwendazake. Ngome imetikiswa.
Profesa Kabudi alikuwa akisifiwa na kupigiwa mfano katika kuitetea nchi kimataifa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Alionwa na Mwendazake kama 'kiboko' katika majadiliano na mazungumzo na hata kufikisha ujumbe kwa wazungu. Jana, amempisha Balozi Liberata Mulamula kwenye Wizara hiyo. Yeye 'amerejeshwa' Wizara ya Katiba na Sheria alikoanzia mwaka 2016. Ngome ya Mwendazake imeguswa na kugusika.
Mazao ya Kikwete (Balozi Mulamula na Dr. Mwigulu Nchemba) yameshaini. Mzee Kikwete ndiye aliyemteua Balozi Mulamula kuwa Balozi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na kadhalika. Mzee Kikwete ndiye aliyemteua Mwigulu kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Taifa na Naibu Waziri wa Fedha chini ya Saada Mkuya. Ni Mzee Kikwete ndiye aliyekuwa akifanya kazi kwa uakaribu mkubwa na Balozi Mulamula na Mwigulu. Upande wake umeshaini.
Mzee Kikwete amewaimarisha Balozi Mulamula kwenye diplomasia/ushirikiano wa kimataifa na Mwigulu kwenye mambo ya fedha. Mzee Kikwete amepata matunda kwenye mbegu alizozipanda chamani na Serikalini. Mzee Kikwete ameshaini huku Mwendazake akitikisiwa ngome yake.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)