Ukilitazama vyema Baraza 'jipya' la Mawaziri, Mzee Kikwete 'ameshaini' ila Mwendazake ametikisiwa 'ngome' yake

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,097
2,000
Wengi tunajua kuwa Balozi Bashiru Ally Kakurwa alikuwa kipenzi cha Mwendazake. Alianza naye kwenye ukaguzi wa mali za CCM na baadaye kumteua kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa. Na mwishoni, akamteua kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi. Jana, Balozi Bashiru ameteuliwa kuwa Mbunge. Hiyo ni njia ya kumuondoa Bashiru kisiasa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi. Pigo kwenye ngome ya Mwendazake.

Mwingine aliyeaminiwa na Mwendazake na wengi wetu kujua ni Suleiman Jaffo ambaye jana amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais. Jaffo alikuwa akisifiwa na Mwendazake kwenye utendaji wake TAMISEMI na hata kuoneshwa kama mfano wa kuigwa. Sasa TAMISEMI imekabidhiwa kwa mdogo wangu Ummy Mwalimu. TAMISEMI imeonekana inapwaya chini ya Jaffo aliyekuwa akionekana mahiri na Mwendazake. Ngome imetikiswa.

Profesa Kabudi alikuwa akisifiwa na kupigiwa mfano katika kuitetea nchi kimataifa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Alionwa na Mwendazake kama 'kiboko' katika majadiliano na mazungumzo na hata kufikisha ujumbe kwa wazungu. Jana, amempisha Balozi Liberata Mulamula kwenye Wizara hiyo. Yeye 'amerejeshwa' Wizara ya Katiba na Sheria alikoanzia mwaka 2016. Ngome ya Mwendazake imeguswa na kugusika.

Mazao ya Kikwete (Balozi Mulamula na Dr. Mwigulu Nchemba) yameshaini. Mzee Kikwete ndiye aliyemteua Balozi Mulamula kuwa Balozi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na kadhalika. Mzee Kikwete ndiye aliyemteua Mwigulu kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Taifa na Naibu Waziri wa Fedha chini ya Saada Mkuya. Ni Mzee Kikwete ndiye aliyekuwa akifanya kazi kwa uakaribu mkubwa na Balozi Mulamula na Mwigulu. Upande wake umeshaini.

Mzee Kikwete amewaimarisha Balozi Mulamula kwenye diplomasia/ushirikiano wa kimataifa na Mwigulu kwenye mambo ya fedha. Mzee Kikwete amepata matunda kwenye mbegu alizozipanda chamani na Serikalini. Mzee Kikwete ameshaini huku Mwendazake akitikisiwa ngome yake.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,615
2,000
Mtu Prof mzima anatukana wahisani sijawahi ona wallah, Yani kwa wizara ya Mambo ya nje mama Samia kateua mtu mzuri, shida ya mwendazake aliamini kuwa Prof na PhD ndo wako vzuri Bila kuangalia historia na experience
Ndiyo maana nchi iliharibiwa vibaya sn na mwendazake
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,665
2,000
Mimi hata angeteua mnyama lakini kwa kuwa tunaanza upya kwa matumaini mapya bila yale mambo hasi naona sawa tu. Yaani ghafla Tanzania iligeuka Rwanda na Burundi. Ni maisha mabovu mno kutokea. Mh. Rais teua tu kulingana na unavyoona inakupendeza wala usisikilize miluzi. Tunakuombea mema mno. Mungu ni hakimu mzuri sana na alihukumu vilivyo kabisa.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,918
2,000
Mama Samiah, Raisi wa awamu ya 6, amiri jeshi, ndiye aliyeSHAINI. Hakuna cha mwendazake wala JK.
Tujaribu tuache habari za makundi.
Tunajuaje kama siyo influence ya Mabeyo?
Hata kama alishauriwa mwisho wa siku yeye ndiye aliyefanya maamuzi.

Everyday is Saturday............................... 😎
 

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
963
1,000
Mkuu Vute Nkuvute, nilichokiona ni uhamisho tu wa mawaziri,, yule akae pale huyu akae huku na wala sio kutikiswa kama ulivyotamani iwe

Pili, kwenye paragraph yako ya kwanza unasema Bashiru kupewa ubunge ni njia ya kumuondoa kisiasa baada ya kuondolewa ktk Ukatibu mkuu kiongozi. Hili sidhani kama ni sahihi kwasababu nafasi ya ukatibu mkuu sio ya kisiasa bali kiutendaji zaidi na haina platform ya kumfanya katibu mkuu awe anaonekana mara kwa mara mbele ya media,

Ila nafasi ya ubunge ndio ya kisiasa zaidi na inamfaa sana Dk Bashiru, na pengine inaweza kumpa milleage kubwa sana huko baadae,, who knows..!!!

Dk Mpango alikuwa mbunge wa kuteuliwa, leo ni VP
Dr Shein aliula ubunge wa kuteuliwa 1995 kutoka kwa Dr Salmin Amour, kisha 2001 akawa VP - JMT kisha uraisi

Hvyo tusimalize sana wino kwa kudhani hilo ni anguko forever, maana hata kwa Mwigulu mlifanya sherehe alipobwagwa ktk post ya uwaziri mambo ya ndani

Mwisho, tusisahau kwamba ILANI YA CCM 2020-2025 ndio dirá kuu ya Serikali hii inayowahitaji wenye dhamana kuitekeleza vyema
 

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,239
2,000
Mama Samia karocha kumuacha bashungwa..na ndungulile..Hawa mawaziri ni zero kabisa...hawana ubunifu wapo wapo tu Kama.mapopoma
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
6,193
2,000
Mara nyingi mvinyo ukiwa ule ule hata ukibadilisha chupa outcomes utamu / uchungu ni ule ule...

Ila Awamu ya Tano badala ya kuwa na watendaji / wafanyakazi tulikuwa na washangiliaji/cheerleaders na wanapropaganda...., yaani mvinyo tulikuwa tunakunywa kwenye visosi.....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom