Ukilazimisha kuachana na ukang'ang'ania watoto kaa ukijua sitakuhudumia wewe na huyo mtoto

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,852
Kwema Wakuu!

Nisikilize mke wangu, nisikilize vizuri Kabisa, sipo hapa kumwakilisha yeyote Yule isipokuwa Nafsi yangu na Yule aliyenipa Nafsi hii. Usiniangalie Kwa macho yako mabaya Kama ya Kondoo, Kama ukijua ukilazimisha kuniacha na kuwachukua watoto kimabavu kaa ukijua kabisa Kwanza hatutarudiana. Sitaki uwe na shida wala Mimi sitaki niwe na shida ya kurudiana na wewe!

Sitakuhudumia wewe na hao watoto wako Kwa sababu ulinikimbia mwenyewe kwa kiburi chako.

Usiseme ni watoto wangu, nimewakataa pamoja na wewe mama Yao.
Kama mama Yao ulikuwa mjinga hivi na kiburi hata hao watoto sitaki watambulike Kwa jina langu. Nimewakataa tangu Leo hii.

Wala hautahesabika ulikuwa mke wangu, na hao watoto watakuwa wako. Nao watakuwa watoto wasio na Baba, Kwa sababu mama Yao ulikuwa Shetani wa mapangoni uliyejificha katika nyumba yangu.

Nawe ulipojipandisha ukaona utaweza kuwalea mwenyewe, ukaleta mambo ya wanawake makahaba katika nyumba yangu. Mimi Taikon mumeo nitakufukuza wala sitakuonea huruma.

Nami upendo wangu nitauhifadhi uwe akiba Kwa malkia wa Tibeli, hiyo ndiye ataumiliki, naye atatawala Enzi yangu. Nani nitampa yote niliyokuwa nimekupa wewe, tena nitampa nyongeza ya Yale niliyokupunja na kukunyima.

Kwa maana nafasi ya mwanamke Mpumbavu itachukuliwa na Mwanamke mwenye busara.

Nao hao watoto watageuka kumbikumbi watokao kwenye kichuguu, watakuacha mwenyewe ukitanga tanga mpaka utakapoangamia.

Enyi wanangu, iweni na roho za kiume ili mpate kuheshimika na watu wenye heshima, wala msitafute kuheshimiwa na watu wapuuzi! Msitake utukufu Kwa kila mtu isipokuwa watu wa maana ambao wanajua thamani ya Baba.

Ila msisahau kutenda Kama wababa waaminifu mkitenda haki Kwa wenye haki. Na ubaya Kwa waliowabaya.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Utoto Ni raha Sana.

Lkn kumbukeni mtoto halali na pesa,mtoto analala na pampus.
 
Dunia hii principled people huonekana Wajeuri, wakatili, na mashetani. They say " In a mad world only the mad are sane"
 
Ukiachana na mwanamke hakikisha unachukua mwanao, wanawake ndio vinara wa kupandikiza chuki kwa watoto.
 
yote haya yangeepukwa kw usinge oa

kijana usioe
ndoa n utapeli,ubinafs

kataa ndoa
 
Ndio maana wazungu wanapooana wanaweza kuishi hata miaka 10 bila kuamua kuzaa watoto. Lengo ni kuepuka kuja kuwaingiza watoto matatizoni endapo ikitokea wakashindwana huko mbeleni.

Njoo kwetu waswahili sasa, bila mimba mtu hajaoa bado..!
Ndivyo tulivyo watu wa Nyota ya Tibeli MKUU.

Nitawafukuza, mtoto atakayetaka Kurudi atarudi Ila sharti niwafukuze kwanza
 
Ndivyo tulivyo watu wa Nyota ya Tibeli MKUU.

Nitawafukuza, mtoto atakayetaka Kurudi atarudi Ila sharti niwafukuze kwanza
hapo baba unakosea kidooogo....amini nakwambia kuna manamake ukiyatupa umetupa manyota ya mafanikio utasota mpaka kifo..km limke lina nyota jipendekeze tu hivyoooo mkuu litarudi tu...ila km ana kimavi mavi.....hand brake...huyo aende salama usalimini....usimjue....utajua tu akitoka tu miezi sita mingi una gari una nyumba una shule kuubwa ya ujasiria Mali....tycoon!! Wakufa mtu...hapo usigeuze shingo kumtizama...lkn ukilewa mafanikio ukatema mwenye kismart kumpata tena ngumu...badala ya kuwa tycoon wa fashi utakuwa typhoon wa maatizo.nakwambia chunguza uone.
 
Hivi hii ikoje? Kuna Jamaa nikimpa yote🤸 basi hiyo wiki nitapata hela balaa....kitaalamu ikoje hii?
 
Back
Top Bottom