Ukikutana uso kwa uso na Kikwete mtaani utafanya nini?

nitakumbusha tu kwamba: Nchi bora ni ile inaongozwa na wataalamu(wasomi na wenye ku-analyse mambo) na si wanasiasa(ili mradi wanatupesa twa kuwadanganyia walala hoi na kujifanya wakereketwa wa chama.)
 
Nitamwambia ukweli ambao wasaidizi na wanaojikomba wake hawathubutu kumwambia kuwa UONGOZI HUUWEZI and you have failed our country!
 
Utamlinda
Utamfanyia kweli
Utampa salamu zake
Utamlalamikia
Utakimbia
Je kwanini rais analindwa kana kwamba ni mharifu?
Wanangu huenda uzee,
Msifanyie masihara swali langu
Maana najiandaa kuwa rais

Nikikutana naye nitamsalimia kwanza then nitamwambia nchi imeumia kodi ya nyumba imepanda kwa 50% na bidhaa na huduma zingine zimepanda hadi 250% wakati mshahara unaongezeka kwa 12% only. Nitamwambia apunguze safari za nje afute posho na marupurupu ya ajabuajabu, avunje Loan BOARD apunguze baraza la mawaziri na kuteua mawaziri wenye uwezo usio na shaka asitumie kigezo cha undugu na kujuana.Finally nitamwambia apige magoti ili nimwombee na kubatilisha maroho ya sheikh Yahya Hussein na wengine wanaofanana naye baada ya maombi hayo atakuwa yuko chini ya ulinzi wa Mungu kisha nitamwambia sasa punguza kikosi kinachokulinda kwani haiwezekani watu zaidi ya 100 wanalinda mtu mmoja kama vile ameiba na anatafutwa na raia wenye hasira kali, nitamwambia tafadhali waache hawa vijana wakafanye kazi zingine kwani hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali watu
 
Ntampa pole sana, kwani yanayoendelea sidhani kama alitegemea

alidhani urais ni sawa na ubunge!!!
 
Ntamweleza udhaifu wake ki-uongozi na pia hana huruma kwa wananchi ndio sababu anasafiri nje ya nchi kila wakati,nitamweleza pia safari za nje siku moja atajulishwa abakie nje

Mualike bar ya jirani kwanza...
Kisha mueleze maelezo yako..
 
Ntamwambia siasa na uongozi ni maisha hivyo utani, uzembe na bahati mbaya kwenye hayo moja kwa moja yana uhusiano na maisha yetu. Pili, ntamuuliza je ni kweli uongozi ni ulevi? mbona jamaa serikalini wanaonekana kama wamelewa? Ni hayo tu.
Utamlinda
Utamfanyia kweli
Utampa salamu zake
Utamlalamikia
Utakimbia
Je kwanini rais analindwa kana kwamba ni mharifu?
Wanangu huenda uzee,
Msifanyie masihara swali langu
Maana najiandaa kuwa rais
 
kilichompata Gadaffi saa za mwisho wa uhai wake mnakikumbuka??
 
nitapiga nae picha halafu nitaupload facebook watu waone, baadae nitaiweka jf kwenye jamii photos halafu nitaweka heading inasema hivi huyu jamaa alie pembeni na jk ni nani? Halafu watu wataanza kuchangia mi nawachora tu!
 
me nikikutatana nae,ntatetemeka hadi atakapopotea machoni pangu..ndio ntaanza kufikiria cha kufanya
 
Eee Mungu niepushe nisije nikakutana na hii kitu.
 
Ntamwambia kuwa huwa ananikera sana anapochekacheka kwenye TV wakati nchi ipo ktk hali mbaya,so ntampa onyo ili asipojirekebisha ,nikikutana naye ni viwiko tu!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom