Ukikuta minyoo kwenye haja kubwa, tatizo ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukikuta minyoo kwenye haja kubwa, tatizo ni nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by baghozed, Oct 10, 2011.

 1. baghozed

  baghozed JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wana JF,ningependa kujua kama ukikuta mnyoo katika haja kubwa ni tatizo gani?na linasabababishwa na nini?na tiba yake ni nini?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 650"]
  [TR]
  [TD]Imeandikwa na: Dr.Henry Mayala Jr Mnamo: Mar 29[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [HR][/HR]
  [​IMG]Mojawapo ya tatizo linaloathiri jamii katika nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ni magonjwa yanayohusiana na minyoo. Duniani kwa ujumla, takribani watu billion moja wameripotiwa kuwa na uvamizi wa minyoo aina ya helminthes kwenye miili yao.
  Minyoo huenezwa kwa njia zipi?
  Minyoo huenezwa pale maji au chakula vinapokuwa vimeathiriwa na mayai au mabuu ya minyoo. Hali kadhalika, uwezekano wa kupata minyoo huchangiwa pia na kutonawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka kujisaidia haja kubwa. Aidha watoto wadogo chini ya miaka mitano ambao hupenda kuchezea mchanga au uchafu kwa ujumla na ambao hupendelea pia kunyonya vidole nao pia huambukizwa kwa urahisi. Mambo mengine yanayochangia katika kupata uvamizi wa minyoo ni pamoja na kuishi katika mazingira machafu, kutembea bila viatu (pekupeku) na kula vyakula ambavyo havijaiva au visivyopikwa vizuri (undercooked foods).
  Aina za minyoo na madhara yake kwa binadamu

  Kuna aina kadhaa za minyoo ambazo, ukiachilia mbali kuwashambulia wanyama wengine kama ngÂ’ombe, nguruwe, mbuzi na kondoo, humshambulia pia binadamu. Aina hizi ni pamoja na
  • Minyoo jamii ya round worms kwa mfano Ascaris lumbricoides ambao husababisha utumbo kuziba (intestinal obstruction) au uambukizi katika kidole tumbo (appendicitis)
  • Minyoo jamii ya hook worms kwa mfano Ancylostoma duodenale ambao huishi kwa kunyonya damu kwenye utumbo mdogo na hivyo kusababisha upungufu wa damu mwilini.
  • Minyoo jamii ya pin worms au thread worm kwa mfano Enterobius vermicularishusababisha kuwashwa hasa sehemu za haja kubwa kwa sababu ya mcharuko mwili unaotokana na minyoo hii kutoa mayai yao eneo hilo hasa kipindi cha usiku.
  • Minyoo jamii ya whip worms kwa mfano Trichuris trichiura husababisha kinyesi kuchanganyika na damu, kupungua uzito, upungufu wa damu na kutoka nje kwa puru (rectal prolapse).
  • Minyoo jamii ya tegu (tape worms) kama vile Taenia solium husababisha kifafa pindi wanapovamia ubongo hasa katika hatua ya ukuaji iitwayo cystercosis
  Dalili za minyoo ni zipi?
  [​IMG]Dalili za kuwepo kwa uvamizi wa minyoo mwilini hutegemea sana aina ya minyoo inayomuathiri mgonjwa. Lakini kwa ujumla, dalili ni pamoja na
  • Maumivu ya tumbo
  • Kupata choo kigumu sana
  • Kuharisha
  • Kujisikia mchovu na mlegevu kutokana na kupungukiwa damu
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Tumbo kuwa na gesi na kuhisi limejaa
  • Kukohoa na kupiga chafya
  • Kwa watoto kusugua meno, kujipinduapindua pamoja na kujikojolea kitandani
  • Kichwa kuuma au kupata kifafa kama minyoo (jamii ya taenia solium) ikitaga mayai yake kwenye ubongo
  • Kuwashwa, na
  • Huathiri ukuaji kwa watoto
  Utatambuaje kama umeathiriwa na minyoo?
  Vipimo vinavyoweza kusaidia kugundua uvamizi wa minyoo, aina zake na hata madhara yaliyosababishwa na minyoo ni pamoja na:
  • Kupima choo kikubwa (Stool examination) kwa ajili ya kuchunguza mayai na mabuu ya minyoo iliyo katika haja kubwa kwa kutumia darubini
  • Kupima damu (Complete blood count) huku mkazo zaidi ukiwa kwenye Eosinophil na kiwango cha damu (Hb). Iwapo kuna uvamizi wa minyoo, kiwango cha Eosinophil huwa juu zaidi kuliko kawaida.
  • X-ray yaweza kusaidia kuchunguza hatua mojawapo ya ukuaji wa minyoo ya Taenia solium iitwayo cystercosis katika ubongo au paja.
  • CT na MRI pia zaweza kurahisisha kugundua na kutambua cyst (vifuko vyenye majimaji) za minyoo aina ya hydatid ambayo huvamia ini, ubongo, figo na sehemu nyingine za mwili.
  • Kipimo cha puru (proctoscopy) husaidia kutambua uvamizi wa minyoo aina ya trichiuris trichiura kwenye puru.
  Minyoo inatibika?
  [​IMG]Bila shaka kabisa, minyoo inatibika. Dawa zifuatazo hutumika katika kutibu minyoo kulingana na aina ya minyoo inayomuathiri mgonjwa
  • Mebendazole hutumika kutibu zaidi uvamizi wa minyoo aina ya round worms
  • Albendazole yaweza kutibu minyoo aina ya tegu (tape worms) pamoja na hydatid
  • Ivermectin hutumika kutibu aina mbalimbali za minyoo
  • Ketrax (levamisole) nayo pia ina uwezo wa kutibu aina kadhaa za minyoo
  • Piperazzine pia ina uwezo wa kutibu aina nyingine nyingi za minyoo.
  Hata hivyo, tunashauri sana matumizi ya dawa hizi hasa kwa watoto, yafanyike mara baada ya kupata ushauri wa daktari na si vinginevyo.

  Inawezekana kujinga dhidi ya uvamizi wa minyoo?
  Njia za kujikinga na minyoo ni pamoja na
  • Kuishi katika mazingira safi.
  • Kunawa mikono na sabuni baada ya kutoka msalani na kabla ya kula
  • Kukata kucha (kucha ndefu huweza kutunza uchafu)
  • Kuwa muangalifu hasa unapokuwa na wanyama kama paka na mbwa
  • Kutumia dawa za kuzuia uvamizi (deworming) kila baada ya miezi mitatu au sita
  chanzo Fahamu kuhusu Minyoo (Helminthesis) – TanzMED(old) - Afya Kwa Wote
   
 3. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  umekuta minyoo mingapi? Ina pingili pingili au ni ya mviringo aafu mirefu kama kijiti? Hilo tatizo linatokana kula uchafu/chakula chenye vimelea vya minyoo. Mara nyingine huingia mwilini kupitia ngozi kama hao wadudu wapo kwenye udongo. Watoto mara nyingi huathirika zaid kwa sabab ya tabia ya kula kula udongo,hii pia hata wanawake wenye tabia hiyo. Tiba yake inategemea aina ya minyoo iliyopo,maana yake kuna hook worms(and round worms) ambazo hutumika albendazole 400mg single dose na taeniasis(yenye pingili) ambayo ni sensitive kwa niclosamide 2g as single dose kwa mtu mzima.
   
 4. baghozed

  baghozed JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  nilikuta mmoja mweupe na mrefu kama urefu wa kidole kidogo,
   
 5. baghozed

  baghozed JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ahsante sana kwa maelezo na huo ushauri
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana naikubali JF humu ndani tuna kila aina ya msomi. Heko Jamiiforums!
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mzizi naomba unisaidie dawa ya hook worm mkuu
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Zipo Dawa za kizungu za kutibu minyoo ikiwa hazijakusaidia jaribu kutumia Dawa zangu za Asilia kisha unipe Feedback.

  1) Dawa ya minyoo: Ponda tembe 3 za kitunguu thoum, tia ndani ya maziwa na kunywa (bila kutia sukari) usiku kabla ya kulala na asubuhi kunywa mafuta ya mbono. Inshallah dawa hio inaweza kukusaidia.

  2) Dawa za kizungu ni Mebendazole capsules (Vermox--Generic only by prescription in the USA)
  zinapatikana hapo mnapoishi. (kama zikipatikana, Insha Allah; Matumizi: Kwa watoto, chukua kibonge (capsule) moja mara tatu kwa siku) kwa wiki miwili. Kwa watu wazima, chukua kibonge miwili mara tatu kwa siku. Tumia dawa mpaka minyoo hazionikani tena..... Tumia mpaka baada ya wiki 2 ama mwezi moja.

  Alafu kuna Vitaklenz: Ni vidonge (capsules---herbal dietary supplement) zinatumika kuondoa minyoo za aina mbali mbali: (tapeworms, pinworms, hookworms, threadworms, bacteria). Matumizi: Kwa watoto, chukua kibonge (capsule) moja maratatu kwa siku) kwa wiki miwili. Kwa watu wazima, chukua vibonde viwili mara tatu kwa siku. Tumia dawa mpaka minyoo hazionikani tena..... mpaka baada ya wiki 2 ama mwezi moja.


  3) Minyoo:
  Kunywa Habbat-Sawdaa pamoja na siki kuondoa minyoo itwange hiyo habbat sawdaa kisha uchekeche upate unga chemsha maji ya uvuguvugu tiya kijiko kimoja hiyo habbat

  Sawdaa kwenye glasi ya maji ya uvuguvugu na utie kijiko kimoja kidogo cha siki ya zabibu au siki ya apple kunywa kabla ya kula kitu kila asubuhi unapoamka kwa muda wa mwezi mmoja Minyoo yako itakwisha kabisa inshallah tumia dawa kisha unipe Feed back.

  Nb. Habbat Sawdaa kwa lugha ya kiingereza inaitwa Nigella Sativa. Na Siki ni Vinegar. kama upo Dar ,au mji wowote Tanzania kaulize kwenye maduka makubwa ya Super Market au kaulizie Sokoni kariakoo kwenye maduka wanayouza maduka ya kiaarabu ya Wapemba.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  asante sana mzizi.
   
 10. A

  AbdulMwenyeUwezo Member

  #10
  Mar 23, 2013
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Minyoo ni wadudu wadogo lakini ni hatari zaidi ya nyoka.
   
 11. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2013
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MziziMkavu unawasaidia sana watu aisee kila kona upo hata sijui professional yako ni ipi aisee, hongerA sana mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu UKI Proffessional yangu ni hii hapa (Investigator and Research Professionals Herbs) Kwa Lugha ya Kiswahili unaweza kusema hivi ( Mchunguzi na Matafiti Mtalaam wa Dawa za mitishamba) Au kwa kifupi unaweza kusema Mtu Mwenye Kipaji cha kuzaliwa na Mungu.
   
 13. Meljons

  Meljons JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2013
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 2,591
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  glory to God
   
 14. Come27

  Come27 JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2016
  Joined: Dec 1, 2012
  Messages: 3,103
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Katika dawa izi za albendazol na mebendazol ipi ni nzuri sana kutumia. Na ushauri unakula dawa ya minyoo kwa muda gani?
   
 15. Maalim Shewedy

  Maalim Shewedy JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2017
  Joined: Jan 17, 2017
  Messages: 1,952
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Type tahadhali basi Mkuu, tujue madhala ya minyooo

  Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
   
Loading...