Mzee wa kusawazisha
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 1,587
- 1,136
Habari za mwamko wakuu humu ndani, nabandika uzi huu ili tulijadili kwa pamoja swala hili.
Binafsi Nina roho ya huruma pale mtu unakuja na shida serious unataka kuzima pesa. Nitolee mfano mzuri ndio ulionifanya niandike uzi huu..
Mwaka 2016 dada yangu mmoja baba na mama mmoja walikua wanacheza vikoba kwa kawaida siku ya kuvunja kama una deni hupati kitu. Sasa yeye alikwama Sana. Nilikua chuoni mwaka wa Kwanza aliniomba nimwazime pesa jumla Laki mbili na 80 ili akivuja tu vikoba atanirudishia.. Walivunja na hakunipigia hata simu nikasamehe,.
Mwaka 2017 alitetereka kidogo kibiashara kiasi hata kodi ya fremu anadaiwa Mwenye fremu alitaka atoe vyombo vyake ndani akanipigia simu nikiwa chuoni tena wiki ya UE Nika risk nikaweka bond simu ili nimuokoe nikamtumia laki 1 japo nilipata baada mwezi m1 na tulipatana baada ya wiki 1.
Mwaka Jana mwezi wa 12 Mwanzoni alinijia tena kuniazima pesa alikwama tena Kuna akaahidi baada ya wiki atanirejeshea Kuna pesa anaisubiri nikampa laki 1 na nusu. Wiki imepita akaomba nimwongezee tena nikampa 20000.
Wiki hii juma 3 anarudisha laki 1 badala ya laki na 70..nikatulia bila kuuliza nikajua Kesho yake angeniambia lolote.
Nami pia kwa Kua niliamini angenirudishia hiyo pesa nikakopa kwa mtu laki na nusu ili niendeleshe biashara yangu kwa bahati biashara hajaenda Sawa jamaa ananidai pesa yake Maana mda umeisha laki nimempa ila bado anataka yote. Na Dada yangu mpaka kufikia Jana nilibidi nifoke kwa Mara ya Kwanza kabisa maana na mimi nadaiwa..
Familia imekaa kikao kwa ajili yangu kisa nadai ela naambiwa Sina utu na sisaidii wenzangu na sisi ni ndugu wa kuzaana Nguvu zote zimeisha hapa sina la kufanya nikikumbuka niliyoyafanya kwa Dada yangu Toka mwaka juzi. Karibuni kwa upembuzi wa kina juu ya jambo hili nadai ili nirudishe deni najibiwa hivyo hapo.
Sent using Jamii Forums mobile app