{ukikatazwa kuoa nawe ukaoa utapata chamtemakuni}

Asee...
Una roho ngumu sana ........
Ila ulikashawahi kukatazwa kuoa?
 
Hivi unataka mpaka ufe ndo ujue kwamba huyo ni ......?!...
 
A%20S-devil1.gif
jihadhari kabla ya hatari...
 
Unataka tukushaur nini sasa....... Oa si umependa :spy:
 
Kumbu ile slogan ya "Hiv free generation begins with You" utapata maradhi yasiyotibika kula kona
 
Huyo achana naye kabisa. Hata kama unampenda vipi, tulia, utampata mwingine atakayekufaa zaidi. Halafu usikubali mimba, make unajua wenye pesa hawalei mimba watamtolea nje fasta. Atakuja kwako akishatemwa na kujifanya ametulia kama kondoo. Kitakachofuata: 'mpenzi nikwambie kitu? Nina mimba yako'. Usikubali mpaka kipimo cha DNA kithibitishe. Halafu 'title' yako inaoyesha umekatazwa kuoa lakini habari inaonyesha 'umeshauriwa' kuachana na huyo malaya na unaweza kuoa mwingine.
 
Hivi kweli wewe mzima kweli?? Unaomba ushauri gani wakati mama yako mdogo humsikilizi?? sasa hiyo mimba ni yako?? pole sana ila utajuta very soon....
 
sikulaumu hata kidogo. Labda binti anajua mambo ndo maana hukutaka kumusiliza mama yako mdogo. Penzi la kicheche lilikuchanganya.
Kubali mimba ndo garama za uzembe wako.
 
duh!ww unaroho ngumu kama ya paka!!!ikatae mimba mpaka vipimo vya DNA vionyeshe ukweli,nenda kacheki afya yako then tafuta mwingine.
 
Pole sana mkuu! Ila hata mimi sikushauri uwe na huyo kicheche kwani kama ameshindikana sasa hivi usitegemee aje kubadilika ndani ya ndoa. Mbwage fasta, hakufai huyo hata kama anayajua vizuri kunako 6x6!!!

Usisahau kwenda kupima kama hajakuachia AIDS mana ake!!!

Wanawake wazuri wapo wengi sana, kaa chini chunguze yule ambaye unamuona anafaa pia usimsahau kumuomba Mungu wako!
Nakutakia kila la kheri mkuu!
 
Kuna rafiki yangu alikatazwa kuoa mwanamke mwenye tabia kama hiyo, jamaa alipenda kufa ikabidi ajibebe mzima mzima na akaoa kwa nguvu. Mwaka mmoja wakapata mtoto, baada ya siku chache akagundua kuwa kuna jamaa mwingine naye anadai huyo mtoto ni wake. Jamaa akavumilia. Siku nyingi hazikupita demu katembea na rafiki wa mumewe na hata mume alipogundua huyo demu hakuacha na tayari wana ndoa ya kanisani, HADI KIFO! It's true and not a joke, na hadi leo wanaishi wote lakini ndoa imekuwa ndoano hivi sasa
 
Back
Top Bottom