Ukikataa ya musa utapata ya kaisari ''egypt mapinduzi yanaanza kuwatokea puani" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukikataa ya musa utapata ya kaisari ''egypt mapinduzi yanaanza kuwatokea puani"

Discussion in 'International Forum' started by PascalFlx, Mar 25, 2011.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mara baada ya kumtoa Rais kwa maandamano ya nchi nzima nchin Egypt mambo yanaanza kuwatokea puani wananchi wa nchi hiyo baada ya Wanajeshi kuchukua nchi,
  Wameanza kujiuliza maswali mengi baada ya kuona hali inabadilika kutoka ilivyokuwa na kuwa mbaya zaidi kwani
  1. wameweka sheria Ngumu MPYA kwa waandamanaji kwa kiingereza Sheria inasema "conflict with the productivity of the country." - ukikutwa na hatia utatozwa Faini isiyopungua 500,000 Egyptian pounds,(Sawa na milioni 126 za Kitanzania)
  2. Kingine wame-introduce what is called "virginity test." , mwanamke ukikamatwa na kosa lolote kama hujaolewa unafanyiwa test ya ubikira kama huna bikra unashtakiwa kwa Umalaya.

  Mambo mbalimbali yanayakiuka haki za kibinadamu yamezidi kupamba moto nchini humo kwa kuongozwa na serikali mpya ya kijeshi kwa habari zaidi kongoli hapo chini

  Egypt's revolutionaries say abusive treatment persists - CNN.com

  Wamenifanya nikumbuke Usemi "Unaruka majivu unakanyaga Moto" kabla ya Mapinduzi yeyote inabidi kujipanga simo mapinduzi tu.
   
 2. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wameuza fimbo wakanunua rungu!
   
 3. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  waliosoma Qur'an na hadith za Mtume wana-enjoy sana katika dunia hii (1) Mwenyezimungu hatoindoa neema, mpaka wanadamu waikatae wenyewe! (2) wanapoambiwa wanafanya uharibifu katika ardhi so wasifanye-wanasema wao ndo wanatengeneza (3) Wanapoambiwa waishi kwa kuangalia walio chini yao wasiishi kwa kuangalia walio juu yao, wanasema ni hekaya tu hizo, (4) wanapoambiwa wasimfanye mlinzi mwingine asiye mwenyezi mungu wanadhani Marekani na jamaa zake ndo walinzi, (5) Wanapoambiwa hamtaiondoa arshi ya mwenyemungu katika uso wa duniya wanasema tutaifuta kwa maandamano, yaani mengi tu wanaenjoy! Infact mi sijaona kinachowatokea puani hapo-hayo yote ni ya msingi au wee unapenda zinaa?
   
 4. Selwa

  Selwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  kumbuka hiyo ni nchi ya kiislam...hayo mambo ya kawaida
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ni kawaida msipofanya mapinduzi yanayotokana na nguvu ya umma....kama yananguvu toka nje lazima dhambi itawala...........
   
 6. P

  Percival JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,568
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Wenzako wanasonga mbele wameisha muondoa dikteta.
  Hii habari ya CNN ina ulakini mkubwa sana. Wamisri wameisha piga kura ya maoni na kuikubali katiba mpya inakayo wachukua kwenye demokrasia ya ukweli ya vyama vingi. Sio demokrasia ya Mubarak ambayo ni yeye tu anashinda kwa miaka 30 !!.

  Pia kitu muhimu sana ni kua jeshi la Misri lilivyo chukua msimamo wa kutowadhuru waandamaji na pia baada ya Mubarak kuondoka kutoa taarifa kuwa hawana nia ya kukaaa madarakani zaidi ya miezi sita kwani kusudi lao ni kuwapa wananchi fursa ya kuchagua serikali yao na jeshi kujitoa madarakani.
   
 7. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kama ndio hivi wananikumbusha wana wa Israel walivyotaka mfalme, Mungu akawainulia Sauli!!!

  asomaye na afahamu!!!
   
Loading...