Ukikaa na mwanamke muda gani ndo sheria inatambua kama ni mke wako?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
16,359
2,000
Waungwana JF ni uwanja unaoheshimika kwa mawazo na michango yenye kujenga na kuelimisha........

Jamiiforums imekuwa darasa huru kwa wadau mbali mbali kujipatia maarifa mbali mbali kutokana na michango na mawazo ya wadau mbali mbali

Maswali yanayokuja humu ni uwakilisho wa jamii nzima kwa kuwa majibu yake yanawalenga au kuwanufaisha wengi......

Hivyo basi kiungwana kama unahisi huna jawabu au jawabu yakinifu juu ya kile kinachoulizwa ni vyema kubakia kimya kuliko kutoa majibu yanayozalishwa ambayo wewe hupo tayari kuyajibu........

Na wadau ambao kwa namna moja au nyingine wana majibu yaliyoshiba juu swali husika ni vyema kuwasilisha majibu kinaga ubaga ili iwe rahisi kwa wadau kutoa gizani.......

JF
HOME OF GREAT THINKERS.....
 

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,333
2,000
Niulize wanasheria ukikaa na mwanamke muda gani ndo sheria inatambua kama ni mke wako?
Kwa mujibu wa kifungu cha 160(1) cha Sheria ya Ndoa, Sura nambari 29 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2019, inasema kwamba ukikaa na mwanamke ndani ya miaka miwili au zaidi kutakuwa na dhanio la ndoa( presumption of marriage).

Hilo dhanio la ndoa( presumption of marriage) kama inavyotajwa na kufafanuliwa katika kifungu cha 160(1) katika Sheria ya Ndoa ni dhana inayopingika pale ambapo anayedai kwamba kulikuwa na dhanio la ndoa atashindwa kuithibitishia mahakama kuhusu hilo dhanio la ndoa.

Kifunngu cha 160(2) kinaeleza mazingira au vigenzo ambavyo mahakama hutumia katika kuamua kwamba kulikuwa na dhaanio la ndoa au la.

Imetolewa na mtaalamu wa Sheria za ndoa, mirathi, jinai na madai.

Karibuni sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom