Ukiitwa mara ya pili for practical interview ni dalili za kuikwaa kazi hiyo?

magessa78

JF-Expert Member
Sep 28, 2009
270
31
wadau,
nimeitwa mahali interview ya pili ambayo wanasema ni practical.je,ni dalili za kuitwaa kazi hiyo?
 
wadau,
nimeitwa mahali interview ya pili ambayo wanasema ni practical.je,ni dalili za kuitwaa kazi hiyo?

Haha..Sasa ulidhani ukiitwa interview ya pili ndo 'chance' ya kupata kazi inapotea? Hapo upo kwenye barabara ya kokoto kuelekea barabara ya lami,ulikotoka kulikua ni barabara ya vumbi.

Jiandae vizuri ukafanje hiyo practical kwa ufanisi upate kazi,.
 
Watu wanafanya hata interview 3 lakini kazi wapi,inauma tu pale unapompotezea muda mtu tena kwa interview tatu kumbe nafasi yenyewe ina mtu
 
Sio guarantee mtu wangu. unaweza piga hata tatu lakini mwisho wa siku wakakupotezea. Ila mwombe Mungu kwa baidii inaweza kua chance yako.
 
Kama ni erolink kazi utapata na maswali yao ya practical marahisi Kama ni erolink lakini
 
hiyo siyo guarantee ya kazi mkuu.....pale utakapoitwa kusaini contract ndo inakuwa guarantee so endelea kukaza hadi mwisho....
 
Mkuu hiyo hatua ni semi final, ukizichanga vizuri karata zako ndio umetusua! Kila la heri!
 
Back
Top Bottom