Ukiisikiliza Bajeti ya Taifa unahisi umaskini unaisha

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,515
44,565
Toka nianze kufuatilia siasa na kusikilizia hotuba za bajeti kuu ya serikali huwa zinanipa matumaini makubwa Sana kila sekta naona imepata uponyaji maendeleo yatakuwa kwa speed ya gari kwenye mteremko,nakuwa nahisi kbs mwaka huu tunatoboa ila mambo yakianza utekelezaji unakuwa mdogo mwisho tunakuwa pale pale (simaanishi kwamba hatupigi hatua), maendeleo yapo tunapata ila ni kana kwamba NI kwa speed ya baiskeli mlimani.

Tunafeli wapi Kama taifa je sababu kuu NI matumizi mabaya ya pesa za umma au NI ongezeko la watu kila mwaka au Nini hasa kinasababisha bajeti isitekelezwe walau hata kwa asilimia 80%.

Sio Siri wananchi wanalalamika mfano nilimsikia mwananchi wa mkoa wa Lindi akihojiwa na mwanahabari akalalamika Sana toka mwaka 2015 ameanza kusikia mpango wa serikali kujenga chuo kikuu mkoani hapo ili kitoe Ajira lakini mpaka bajeti ya mwaka Jana ikasema pia ingejenga chuo ikawa kimya na Tena ya mwaka huu Imeahidi itajenga chuo.

Amechoka kudanganywa anadai wao Kama wananchi hawataki taa za barabarani kwani hawali taa wanataka chuo kikuu ili kitoe Ajira wapate hela.pia aligusia gharama za matibabu NI kubwa Sana kwenye hospital za rufaa wakati anasikia kwenye bajeti kwamba serikali Imeongeza mabillion kununua dawa.

Shida ni nini mbona bajeti inakuwa na matumaini halafu kwenye real life hali NI tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom