Ukiishi nchi za wazungu utajua Waafrika tuna laana au tupo kwa bahati mbaya!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Mazingira safi yaliyopangiliwa na ya kuvutia,
Mipangilio ya mitaa na majengo (miji)iko smart,
Taratibu za kazi ziko well defined and disciplined,
kuheshimu ratiba na muda,
Kushughulika na yako ya wenzio hayakuhusu,
kuendena na ratiba na wakati,
kuheshimu haki na hisia za mwingine,
polisi kulinda waandamanaji wanaoikosoa serikali yao,
elimu ya malengo sio mtoto mmoja masomo 12 tena yasiyo ulingano,
Serikali ni za uchaguzi wa wananchi hasa,
Huduma za kijamii sio ombi ni haki ya msingi,
na Mengine mengi...

Sina hakika kama viongozi wa kiafrika huwa wakija huku wanaondoka na lolote la kuiga!
 
Aiseee sisi wa manzese kwa tumbo tuko fresh tu tumekubali hali zetu
Popote ulaya tatizo mkwanja tu
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, ukifika Ulaya, USA au Canada unaweza ukadhania sisi huku Africa tumelaaniwa. Kwa kweli siyo siri, hawa binadamu wenzetu wametuacha kwenye kila kitu.
 
Ongeza,baridi la kufa mtu,bili haziishi kila siku barua za bili zinadondoka kwenye letter box,tv unailipia lesseni kuangalia,bill ya wazoa taka,bili ya gesi msimu wa winter,kama hauna kazi unalipiwa kodi ya nyumba na pesa ndogo ya kusukuma siku mpaka utakapopata kazi,ukimzalisha ke lazima uchangie gharama za mtoto,ukiwa single maza na hauna kazi unapewa nyumba na kulipiwa kodi na pesa ya kutunza watoto mpaka watakapofika miaka kumi na nane,ukiwa mlevi na mpenda msosi mapochopocho kibao.
 
Back
Top Bottom