Ukiijua hii Saikolojia na tabia ya Askari Polisi, hawatakusumbua sana

Sema askari Wetu wanavyo penda kujaribu nguvu zao kwa raia ni noma yaani unaweza ukawa mpole nabado ukala kipondo
 
Inaonekana huyu anayewakojolea hawamuoni kwa sababu ya hizo ngao

Wakimtia mbaroni lazima tu atajinyea
 
walimdandia kijana wangu nilimuagiza sehemu ni mizigo haikua na risit lilikua bonge la furushi ila in real life thaman yake ilikua haifik 50k majamaa yakajua apa ulaji dogo akanipigia simu nikaomba kuongea na afande mmoja nilimkoromea akawa mdogo mixa kumuuliza jina lake na number yake nilivoenda sasa kuonana nao nikakuta mnyama kawaalika wenzie waje wampige tough maana ule mkwara ulikua beyond his level walivoniona tu wakaanza kucheka yaan uyu chalii ndio kutia jamba jamba nikatumia mbinu tajwa hapo juu maana jamaa walikua na SMG bullet proofs helmets mabut ma kinga ugoko nikajidai pimbi miksa kucheka cheka kuapologize kila kitu kuwaita bro wakaniachia kiroho safi miksa kuuliza wakitaji hayo mazaga ninayo suply watapataje majamaa yanapenda ukuu
 
walimdandia kijana wangu nilimuagiza sehemu ni mizigo haikua na risit lilikua bonge la furushi ila in real life thaman yake ilikua haifik 50k majamaa yakajua apa ulaji dogo akanipigia simu nikaomba kuongea na afande mmoja nilimkoromea akawa mdogo mixa kumuuliza jina lake na number yake nilivoenda sasa kuonana nao nikakuta mnyama kawaalika wenzie waje wampige tough maana ule mkwara ulikua beyond his level walivoniona tu wakaanza kucheka yaan uyu chalii ndio kutia jamba jamba nikatumia mbinu tajwa hapo juu maana jamaa walikua na SMG bullet proofs helmets mabut ma kinga ugoko nikajidai pimbi miksa kucheka cheka kuapologize kila kitu kuwaita bro wakaniachia kiroho safi miksa kuuliza wakitaji hayo mazaga ninayo suply watapataje majamaa yanapenda ukuu
Jamaa wakipiga kinga ugoko ujue hali si shwari kabisa
 
Kweli inasaidia, lakini kwa Mwanaume kama wao kidogo ni mtihani kuweza kujishusha kiasi hicho.Na hasa ukiwa na akina Mama
ndani ya gari lako.
Pia hii tabia siyo dunia nzima.Kweli nchi kama Marekani mtizamo wako ni sahihi.Lakini mahali kama Uingereza tofauti sana.
 
Hii ni nzuri sana kama wewe ni mtu wa kujishusha, me sio mtu wa aina hiyo ila kuna siku nikiwa na gari ya kuazima natoka Mwanza naenda Igunga pale Usagara mbele kidogo nikasimamishwa na traffic mrembo wa kike, neno la kwanza kuongea " Habari dada mrembo, moyo wangu umepiga paah!
nikidhani nimekutana na malaika kumbe binadamu kama malaika pia wapo' hata leseni sikuombwa. Nilifanya hivyo sababu alikua mwanamke.
 
Yaani hawa jamaa ukikutana nao wewe kuwa Fala tu basi. Nishakutana na ngese zaidi ya 10 lakini jamaa hawachukui hata senti tano.
Kuwa humble, obey their orders jivishe sura ya upole uliopitiliza ==> ufala
Utasikia hebu ondoka !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa askari na unatafuta nguvu...ASKARI WANA INFERIORITY COMPLEX na ndo maana unapowajibu au waelimisha wanakuja juu na kuona umewadharau.hivyo wanataka kutumia nguvu na vitisho. Askari kiakili ni weupe sana. Hawana SUPERIORITY COMPLEX YOYOTE NI SO WEAK AND INFERIOR NDO MAANA INABIDI WAWE WAKALI.
 
Safi sana mkuu! Yaani unawaleta kwenye utengamano wako wa kiraia ili uwaachie Superiority yao uondoke na amani yako. Polisi wako simple sana ukiwajua wanavyocheza kwenye zone yao ya kazi na weakness na strength zao.

Kwa hizo phrase zako hawachomoi maana tayari unakuwa umeingia more willingly and smoothly kwenye conversation nao... They all need that.

Mimi kuna mmoja alishawai hadi kunisukuma baada ya kamkebe(kagari) kangu kuzima ghafla barabarani... Nilimuwin kirahisi sana na akawa mwanangu nikawa naenda hadi kupiga soka barracks kwao.

Easy as that!

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna mmoja tupo nae mtaani yupo poa sana hana mambo ya kipuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawahi kukamatwa askari nikiwa chuo huko DSM (nilikuwa na vijana wenzangu pale mtaani, kama watano hivi)
Walikuwa askari kama wanne wa kawaida, FFU wawili wakiwa full covered pamoja na mabaunsa watatu.

Hiyo siku, majira ya saa 3 asubuhi baada ya kupata chai, nikaamua kwenda kucheza pool table aisee!

Basi, game ya kwanza, ya pili, tatu... Muda unaenda tu, sasa nikawa nahisi kuna communication kichwani ikiniasa kuondoka eneo lile (hapa wakuu huwa nashindwa kujitambua nina kitu gani kichwani, hatari nyingi zinazonitokea huwa kuna nguvu inayonipa habari mda mchache kabla, nyingi huwa napuuzia, nyingine chache naziitikia na kujiokoa) lakini nikapuuzia!

Sasa ghafla aisee, nikajikuta naning'ining'ia juu pasipo kujielewa, kutazama nakutana na jitu refu sana lenye mwili uliojengeka haswa, mweusi ti!

Kuja kutahamaki najikuta ndani ya defender....Dah! Stori ndefu nisiwachoshe!

Baada ya kuswekwa humo na wenzangu, mimi nilijua hapa nikijifanya najua, mara.naongea sana, ntakufa kwa vipigo! Nikawa kiiimya, sikutaka hata kuwaangalia usoni wale jamaa!

Wale wenzangu wakaanza ubabe wa kiaina kama mnavyowajua wagogo na visu vyao! Aisee walikutana na kipondo kikali sana huku nashuhudia! Nikazidi kuwa mpole!

Askari mmoja akanigusa begani
"We dogo, mbona umejikunja hapo, huongei, unaumwa"?

...siumwi afande

" kwanini unacheza pool siku ya kazi"?

...afande Jmosi ni siku yetu ya kuwa free

(Afande akakaa kimya) hapo gari.lishaanza mwendo kuelekea kituoni, shekilango! Kichwani nikiwa nachakata mipango ya kujinasua na hili tatizo! Dah hatari sana

Tukafika Shekilango, nikaruka na.kuwa wa kwanza kutoka, nikasoma mazingira chap chap mle na kuona kuna selo 2. Moja ina watu kama 30, wako gizani hatari, kelele sana halafu vifua wazi! Nikaona humo ntakufa!

Ya pili iko na mzee mmoja, kijana mwingine halafu dirisha kubwa tu inaangalia barabarani.. Nikajisemea.hapa ndo naingia!!

(Nitarudi kumalizia)
Askari ni ndugu yako akiwa kitaa, akifika kituoni anakupita na kukuacha kwa wenzie wakuangamize
 
Maelezo marefu kweli kweli safi sana.

Askari shupavu anakamilisha cycle ya W? Siyo kweli. Hii iko kwenye muvi zaidi na maandiko ya mitandaoni.

Kwamba Mabeyo na Siro wanapiga ulabu kushinda Jibapa?

Sababu pekee sinywi pombe ni kwasababu katika familia nilikosa wa kuchagiza hata kuionja pombe.
Baba ni mwanajeshi mstaafu, hajawahi kunywa pombe wala kuvuta sigara tangu napata akili mpaka leo. Wanawake siwezi kumsemea, ubabe najua hana ni civil sana.

Psychologically askari anaact shit siyo kwasababu ya superiority ila ni kwa sababu ubongo wa binadamu uko programmed hivyo. Yaani hata leo Humble African ukikabidhiwa mamlaka ya kuamua hatma ya mustakabali wa mtu una chance nzuri ya kua sadist soon.

Hiyo iko proved na experiment hii
Stanford prison experiment - Wikipedia

Au kwenye muvi ya Forest Whitaker inaitwa The Experiment.
Mkuu msemee na hao wanawake uliokataa kumsemea ili tumpe marks zake.

Maana kimoja ulichokitaja katika mtungo wa 3w's na kugoma kutaja hicho kingine muhimu, unamkosesha marks za majaji wadau.

Maana hilo moja tu ulilolitaja halimuondoi kwenye sifa zao hizo za jadi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu msemee na hao wanawake uliokataa kumsemea ili tumpe marks zake.

Maana kimoja ulichokitaja katika mtungo wa 3w's na kugoma kutaja hicho kingine muhimu, unamkosesha marks za majaji wadau.

Maana hilo moja tu ulilolitaja halimuondoi kwenye sifa zao hizo za jadi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba unijibu.

Unaweza jua wanawake anaotembea nao baba yako?
 
Maisha haya bhana!

Nilipokuwaga mdogo nilikuwa na akili finyu sana nadhani kuliko watoto wote wa mtaani kwetu.. Niliamini kirahisi sana mambo bila hata kufikiri kwa kina yaani zile akili teketeke za kitoto..yaani nikitaka kuamini jambo basi naamini mwenyewe tu bila hata kuuliza mtu wala kujisumbua kulichambua na kuingia ndani zaidi kifikra, mfano niliamini polisi wote wanajua kufanya kila kitu kuanzia kuendesha gari, pikipiki, ndege, kupiga risasi, hadi kuwa na akili kubwa kuliko wote...maana niliwahi kuwa na rafiki yangu mmoja baba yake alikuwa anaendesha lile pikipiki a kuongozea misafara ya viongozi wa serikali,

Sasa Mimi kwa akili yangu ya kitoto baada ya kuona hata Rais wa nchi anaongozwa njia na traffic nikaamini watakuwa super human hawa yaani hata Rais wa nchi haijui njia vizuri hadi hawa wamwongoze? Watakuwa na akili kubwa sana hawa mapolisi. Ahahaha!! Utoto una mengi sana ya kustaajabisha na kufurahisha.

Sikuishia hapo kuna siku niliona ajali imetokea na umati mkubwa sana uliwasubiri polisi waje wapime pale ile ajali ilipotokea..ilizidi kuchochea Mimi kuhisi polisi Wenda ndio binadamu wenye akili na ujasiri sana Duniani maana wamesubiriwa waje waamue hatma ya ile ajali. Sikujua, I was kid and Naïve.

Mattet of fact, Kuishi na mjomba aliekuwa Kamanda wa Polisi na Kukulia pia kuishi karibu na kambi ya polisi kwa zaidi ya miaka 20 kulinifanya niwe karibu na askari wengi sana kuanzia utoto wangu hadi ukubwani nina marafiki wengi tu mapolisi, hii ilinisogeza na kunifanya niwe karibu na maisha yao ya kila siku, ambao baadhi wamekuwa ni rafiki zangu wa kutupwa hadi kesho maana kuna walio wema na wazuri sana tofauti na wengi tulivyowakariri kwa picha mbaya ya umoja wao kama watu makatili, wanyang'anyi, waonevu e.t.c but trust me! wapo ambao ni wema, waungwana, waelewa na wenye huruma zaidi yetu sisi Raia wa kawaida.

Anyways, Baada ya kwenda chuoni na kusoma masomo yangu ambayo yalijumuisha na pure psychology kama minor discipline ambamo humo nilikuja kugundua Polisi almost wote wana kitu kitaalamu kinaitwa "Superiority complex" hii ni ile hali ya kuona wao wako juu yako wewe Raia kimamlaka na kimabavu hivyo wengi wanategemea kukuona ukikubali na kutekeleza maagizo, maelekezo na amri kutoka kwao bila majadiliano yeyote, afande yeyote Duniani anachukia sana kukuona ukijadili kichwani mwako kutekeleza amri aliyotoa. Hii ndio iliwafanya wakaja na msemo wao "Utii wa Sheria bila shuruti" msemo huu huko wazi kabisa wanataka wewe uwape nafasi yao ya "superiority" sababu hicho ndicho wanachofeel na kutaka kukiona kutoka kwako na ndicho kinachowaplease na kuwapa raha rohoni.

Ufanyeje sasa ili umuwin vizuri huyu kaka Polisi na aione hii superiority yake? Wewe hakikisha una adjust wewe mwenye psychologically hadi uhakikishe Afande anapata nafasi yake ya kuiona ile superiority complex, akikupa amri halali hakikisha unaitii kwa heshima na unyenyekevu huku ukimuonesha kwamba wewe huna shida wala maneno nae na mara zote epuka majibizano nae yasiyo na tija kwako hayakusaidii zaidi unamprovoke tu kaka Polisi, jitahidi kukaa kimya panapotakiwa lakini si saana maana sometimes wanatafsiri ukimya kama dharau na ngebe lakini dhumuni lako ni kuiwin trust yake zaidi ili akuamini na akupe hata mwanya wa wewe kumuachia manyoya na kumtoroka ikibidi kwa yeye kukuover trust.

Maana tayari kakuamini na kukuona wewe sio combatant zaidi kwake. Kamwe usibishane nae na kutaka kumnyang'anya superiority yake atakumwaga mavi hadharani na kwa mara ya kwanza utajua ni kwanini IDD Amini Dada aliitwa Dada wakati alikuwa wa kiume ....

Kuwa mwelevu, makini na mtulivu wakati wote ukiwa unampanga kimkakati Mwela hata kama kakukalisha chini ya sakafu ukipanic na kujifanya unazijua haki zako zaidi ya mwenyekiti wa wanasheria Tanganyika utapigwa vibao, virungu vya kila rangi ili akili ikukae sawa utambue kwamba bado huko Umatumbini kwa akina Nyani Shambuku na sio majuu kwa waliostaharabika kitambo tangu mwaka 1058 B.C ambapo tangu zamani wana askari wa doria maalumu ya magari na helicopter kila siku kwa ajili ya kuokota walevi wanaomangamanga usiku kila mtaa ili wasifunikwe na barafu na kufa kwa kuwalaza kituoni hadi kunapopambazuka wanawaachia huru bila mashtaka yeyote then ikifika tena usiku njemba zinarudi tena Bar kupiga vyombo zinaokotwa na kupelekwa kituoni kwenye mablanketi na vitanda special vya kupumzika walevi kwenye kituo cha Polisi kwa usalama wao.

Hii ni Africa ambayo ni hatari zaidi Raia kuwa sahihi huku serikali ikiwa imekosea ni hatari sana..... Ukiwa mbele ya kaka polisi kama kuna kitu kinamchefua na kumpandisha hasira ni kujua wewe unajua haki zako na unataka kuzidefend hata aggressively ikibidi...its very risk..!

Na nakusisitiza utafia mikononi mwa polisi ukiendekeza tabia ya kusisititizia haki zako ukiwa mikononi mwao labda kama huko na Barrister/ lawyer wako on spot. Wewe zijue haki zako ila unatakiwa ujue namna ya kuzipresent humbly and smoothly kwa kaka polisi ili aendelee kukafeel kale ka superiority kake unless ukikabutua ka superiority unamfanya apate inferiority complex na Daima huwa hawana uvumilivu wa kukumbatia inferiority complex mbele ya Raia huwa hawana namna nyingine zaidi watakuchakata sana mkuu hadi ujiadjust kulingana na uhalisia wao wenyewe.

Jitahidi uijue hii psychological mind battle kati yako na bwana Afande wa kiafrika once ukiimaster hata yule RPC wa Dodoma hawezi kukuadhiri kwenye Press conference zake maana ukikutana nae kwenye preliminary interrogation nae wewe Fanya kazi ndogo ya yeye kuiona superiority yake once akiikosa ataenda kuisaka mbele ya waandishi wa habari akiwa anakushika bega na kukuadhiri bongo nzima kama Nabii Tito vile .... Uzembe kama huu ulimgharimu hata marehemu Mwangosi, alichukua superiority yao akina Afande then wakaitafuta kwa nguvu at last ikagharimu maisha ya huyu innocent journalist, Mwandishi wa habari aliefirigiswa na mamwela majuzi kati kwenye simba Day nae alishindwa kuendana na hii rhythm ya superiority e.t.c

Ukijifanya kuzijua zaidi haki zako utasikia Afande hili linajifanya ni "Libush lawyer" means wewe unajifanya mwanasheria wa kijijini anaejifanya anajua Sheria kumbe hujui... Hapo ndio kwa wale mamwela wa zamani... Linafuata swali kwa sauti ya ukali huku akiwa kashika kitambulisho chako utasikia wewe unaitwa nani? Unajibu naitwa Maiko, unamsikia Afande anang'aka kwa ukali kwa wenzake mnaona maafande limetudanganya linaitwa maiko wakati kitambulisho chake kimeandikwa "Michaeli".... Anakunawa zinga la Kofi usoni pwaaaaaaaaaa... Yaani ni visa tu na mikasa ili aipate superiority yake ilhali ni makosa yake ya kiusomaji tu lakini yeye lengo lake kubwa ni kuisaka superiority yake hata kwa mlango wa nyuma anasahau wakati wewe unasoma yeye alikuwa Muheza - Tanga anauza machungwa then Anko wake akampa kimemo akawa Mwela unfortunately sasa yupo kazini kusoma tu jina anascratch kama CD iliyochubuka vile afu anakuangushia wewe Raia kama ndio kosa lako vile kutaja Maiko.

Then wana kitu kingine kitaalamu kinaitwa "conspiracy of silence" yaani wana mambo yao ambayo wanafeel pleasant sana kuongea wao wenyewe Kama wenyewe nilikuwa na washkaji zangu Mamwela kipindi nikiwa wadogo unasikia redio zao zinaongea mara November... Mara India mara Lima... Yaani upo karibu lakini ung'amui hata moja wakiamua kuongea kwa yale malugha yao ya kipolisi ndio unatoka kapa zaidi. Ila hata mkoloni alilijua hili akawatengenezea Barracks zao au kotazi huko wao wana maisha tao wenyewe na lifestyle yao wenyewe tofauti na wengine.

Hivyo hata wakikaa mtaani watalazimisha waipate hii haki yao ya faragha na kuwa wao sasa kama Raia ni vyema ukiwa nao kama washkaji au mtuhumiwa uwape hii space ya wao kuwa na muda wao wa kuongea lugha yao wanayaoelewana wao tu. Hata wakikukamata give them space ya wao kuishi hii Dunia yao adhimu kidogo. Ukiwa mtumhumiwa pia wape hii nafasi sio unaona kaka polisi anataka kuongea na polisi mwenzie lugha yao unaleta pua yako. Watakupukusa na rungu ushindwe kutembea ili uwape hii nafasi ya kufanya their own conspiracy of silence, Mimi huwa naiita Police to police heart to heart talks.

Wana triple "W" woman, war and whisky, askari kamili alieiva anazunguka katika hivi vitu vitatu, askari alieiva anapenda sana mademu kwa maana ya woman, then anapenda sana ubabe usio na msingi ili adominate na kuwa superior na pia anapenda mtungi ndio maana wamewekewa na canteen zao za kulewa kwa bei chee kabisa ili watimize cycle yao ya W... Askari alieiva ni yule anaemiliki hizo "W" kikamilifu.

Kimsimgi sikumbuki ni lini nimeingia kwenye 18 za askari nikashindwa kumuwin psychologically maana physically simuwezi naanzia deep down his mental processing then mwilini najua patafuata tu yale niliyopandikiza akilini mwake during my first impression kwake. Make sure you Don't cross his line, ukimprovokes negatively utageuka nzi atakutega kwa mavi na sio Mchele kama ukiwa mpole, makini na mwelevu mwenye Pendo fake kama njiwa manga.

Nina mengi zaidi ya kushare na kudiscuss na nyie wakuu ila kwa leo tutembee na haya ya fasta fasta niliyoandika hapo juu, nikisettle vizuri nitaandika deeply and precisely kuhusu police psychology.

Lastly, tuwaheshimu na kuwasamehe ndugu zetu polisi kwa mengi mabaya wanayotufanyia inaweza kuwa sababu ya stress na solid depression wanayopitia kulingana na nature ya kazi yao pia niwape heko kwa kuwa miongoni mwa champion wa kuhandle stress wanazokutana nazo kila siku kazini na niwaase wanasiasa kutowatumia polisi vibaya kwa interest zao ili social harmony and peace itawale milele taifa la Bongo. Amen!

Imekaa vibaya kama Kally P. View attachment 841866View attachment 841867View attachment 841868View attachment 841869View attachment 841870View attachment 841871
mkuu tuwekee na audio mm nimejitahidi but nimeshindwa kabisa kumalizia kusoma, hakuna vituo kabisa
 
Back
Top Bottom