Ukiijua hii Saikolojia na tabia ya Askari Polisi, hawatakusumbua sana

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,779
14,302
Maisha haya bhana!

Nilipokuwaga mdogo nilikuwa na akili finyu sana nadhani kuliko watoto wote wa mtaani kwetu.. Niliamini kirahisi sana mambo bila hata kufikiri kwa kina yaani zile akili teketeke za kitoto..yaani nikitaka kuamini jambo basi naamini mwenyewe tu bila hata kuuliza mtu wala kujisumbua kulichambua na kuingia ndani zaidi kifikra, mfano niliamini polisi wote wanajua kufanya kila kitu kuanzia kuendesha gari, pikipiki, ndege, kupiga risasi, hadi kuwa na akili kubwa kuliko wote...maana niliwahi kuwa na rafiki yangu mmoja baba yake alikuwa anaendesha lile pikipiki a kuongozea misafara ya viongozi wa serikali,

Sasa Mimi kwa akili yangu ya kitoto baada ya kuona hata Rais wa nchi anaongozwa njia na traffic nikaamini watakuwa super human hawa yaani hata Rais wa nchi haijui njia vizuri hadi hawa wamwongoze? Watakuwa na akili kubwa sana hawa mapolisi. Ahahaha!! Utoto una mengi sana ya kustaajabisha na kufurahisha.

Sikuishia hapo kuna siku niliona ajali imetokea na umati mkubwa sana uliwasubiri polisi waje wapime pale ile ajali ilipotokea..ilizidi kuchochea Mimi kuhisi polisi Wenda ndio binadamu wenye akili na ujasiri sana Duniani maana wamesubiriwa waje waamue hatma ya ile ajali. Sikujua, I was kid and Naïve.

Mattet of fact, Kuishi na mjomba aliekuwa Kamanda wa Polisi na Kukulia pia kuishi karibu na kambi ya polisi kwa zaidi ya miaka 20 kulinifanya niwe karibu na askari wengi sana kuanzia utoto wangu hadi ukubwani nina marafiki wengi tu mapolisi, hii ilinisogeza na kunifanya niwe karibu na maisha yao ya kila siku, ambao baadhi wamekuwa ni rafiki zangu wa kutupwa hadi kesho maana kuna walio wema na wazuri sana tofauti na wengi tulivyowakariri kwa picha mbaya ya umoja wao kama watu makatili, wanyang'anyi, waonevu e.t.c but trust me! wapo ambao ni wema, waungwana, waelewa na wenye huruma zaidi yetu sisi Raia wa kawaida.

Anyways, Baada ya kwenda chuoni na kusoma masomo yangu ambayo yalijumuisha na pure psychology kama minor discipline ambamo humo nilikuja kugundua Polisi almost wote wana kitu kitaalamu kinaitwa "Superiority complex" hii ni ile hali ya kuona wao wako juu yako wewe Raia kimamlaka na kimabavu hivyo wengi wanategemea kukuona ukikubali na kutekeleza maagizo, maelekezo na amri kutoka kwao bila majadiliano yeyote, afande yeyote Duniani anachukia sana kukuona ukijadili kichwani mwako kutekeleza amri aliyotoa. Hii ndio iliwafanya wakaja na msemo wao "Utii wa Sheria bila shuruti" msemo huu huko wazi kabisa wanataka wewe uwape nafasi yao ya "superiority" sababu hicho ndicho wanachofeel na kutaka kukiona kutoka kwako na ndicho kinachowaplease na kuwapa raha rohoni.

Ufanyeje sasa ili umuwin vizuri huyu kaka Polisi na aione hii superiority yake? Wewe hakikisha una adjust wewe mwenye psychologically hadi uhakikishe Afande anapata nafasi yake ya kuiona ile superiority complex, akikupa amri halali hakikisha unaitii kwa heshima na unyenyekevu huku ukimuonesha kwamba wewe huna shida wala maneno nae na mara zote epuka majibizano nae yasiyo na tija kwako hayakusaidii zaidi unamprovoke tu kaka Polisi, jitahidi kukaa kimya panapotakiwa lakini si saana maana sometimes wanatafsiri ukimya kama dharau na ngebe lakini dhumuni lako ni kuiwin trust yake zaidi ili akuamini na akupe hata mwanya wa wewe kumuachia manyoya na kumtoroka ikibidi kwa yeye kukuover trust.

Maana tayari kakuamini na kukuona wewe sio combatant zaidi kwake. Kamwe usibishane nae na kutaka kumnyang'anya superiority yake atakumwaga mavi hadharani na kwa mara ya kwanza utajua ni kwanini IDD Amini Dada aliitwa Dada wakati alikuwa wa kiume ....

Kuwa mwelevu, makini na mtulivu wakati wote ukiwa unampanga kimkakati Mwela hata kama kakukalisha chini ya sakafu ukipanic na kujifanya unazijua haki zako zaidi ya mwenyekiti wa wanasheria Tanganyika utapigwa vibao, virungu vya kila rangi ili akili ikukae sawa utambue kwamba bado huko Umatumbini kwa akina Nyani Shambuku na sio majuu kwa waliostaharabika kitambo tangu mwaka 1058 B.C ambapo tangu zamani wana askari wa doria maalumu ya magari na helicopter kila siku kwa ajili ya kuokota walevi wanaomangamanga usiku kila mtaa ili wasifunikwe na barafu na kufa kwa kuwalaza kituoni hadi kunapopambazuka wanawaachia huru bila mashtaka yeyote then ikifika tena usiku njemba zinarudi tena Bar kupiga vyombo zinaokotwa na kupelekwa kituoni kwenye mablanketi na vitanda special vya kupumzika walevi kwenye kituo cha Polisi kwa usalama wao.

Hii ni Africa ambayo ni hatari zaidi Raia kuwa sahihi huku serikali ikiwa imekosea ni hatari sana..... Ukiwa mbele ya kaka polisi kama kuna kitu kinamchefua na kumpandisha hasira ni kujua wewe unajua haki zako na unataka kuzidefend hata aggressively ikibidi...its very risk..!

Na nakusisitiza utafia mikononi mwa polisi ukiendekeza tabia ya kusisititizia haki zako ukiwa mikononi mwao labda kama huko na Barrister/ lawyer wako on spot. Wewe zijue haki zako ila unatakiwa ujue namna ya kuzipresent humbly and smoothly kwa kaka polisi ili aendelee kukafeel kale ka superiority kake unless ukikabutua ka superiority unamfanya apate inferiority complex na Daima huwa hawana uvumilivu wa kukumbatia inferiority complex mbele ya Raia huwa hawana namna nyingine zaidi watakuchakata sana mkuu hadi ujiadjust kulingana na uhalisia wao wenyewe.

Jitahidi uijue hii psychological mind battle kati yako na bwana Afande wa kiafrika once ukiimaster hata yule RPC wa Dodoma hawezi kukuadhiri kwenye Press conference zake maana ukikutana nae kwenye preliminary interrogation nae wewe Fanya kazi ndogo ya yeye kuiona superiority yake once akiikosa ataenda kuisaka mbele ya waandishi wa habari akiwa anakushika bega na kukuadhiri bongo nzima kama Nabii Tito vile .... Uzembe kama huu ulimgharimu hata marehemu Mwangosi, alichukua superiority yao akina Afande then wakaitafuta kwa nguvu at last ikagharimu maisha ya huyu innocent journalist, Mwandishi wa habari aliefirigiswa na mamwela majuzi kati kwenye simba Day nae alishindwa kuendana na hii rhythm ya superiority e.t.c

Ukijifanya kuzijua zaidi haki zako utasikia Afande hili linajifanya ni "Libush lawyer" means wewe unajifanya mwanasheria wa kijijini anaejifanya anajua Sheria kumbe hujui... Hapo ndio kwa wale mamwela wa zamani... Linafuata swali kwa sauti ya ukali huku akiwa kashika kitambulisho chako utasikia wewe unaitwa nani? Unajibu naitwa Maiko, unamsikia Afande anang'aka kwa ukali kwa wenzake mnaona maafande limetudanganya linaitwa maiko wakati kitambulisho chake kimeandikwa "Michaeli".... Anakunawa zinga la Kofi usoni pwaaaaaaaaaa... Yaani ni visa tu na mikasa ili aipate superiority yake ilhali ni makosa yake ya kiusomaji tu lakini yeye lengo lake kubwa ni kuisaka superiority yake hata kwa mlango wa nyuma anasahau wakati wewe unasoma yeye alikuwa Muheza - Tanga anauza machungwa then Anko wake akampa kimemo akawa Mwela unfortunately sasa yupo kazini kusoma tu jina anascratch kama CD iliyochubuka vile afu anakuangushia wewe Raia kama ndio kosa lako vile kutaja Maiko.

Then wana kitu kingine kitaalamu kinaitwa "conspiracy of silence" yaani wana mambo yao ambayo wanafeel pleasant sana kuongea wao wenyewe Kama wenyewe nilikuwa na washkaji zangu Mamwela kipindi nikiwa wadogo unasikia redio zao zinaongea mara November... Mara India mara Lima... Yaani upo karibu lakini ung'amui hata moja wakiamua kuongea kwa yale malugha yao ya kipolisi ndio unatoka kapa zaidi. Ila hata mkoloni alilijua hili akawatengenezea Barracks zao au kotazi huko wao wana maisha tao wenyewe na lifestyle yao wenyewe tofauti na wengine.

Hivyo hata wakikaa mtaani watalazimisha waipate hii haki yao ya faragha na kuwa wao sasa kama Raia ni vyema ukiwa nao kama washkaji au mtuhumiwa uwape hii space ya wao kuwa na muda wao wa kuongea lugha yao wanayaoelewana wao tu. Hata wakikukamata give them space ya wao kuishi hii Dunia yao adhimu kidogo. Ukiwa mtumhumiwa pia wape hii nafasi sio unaona kaka polisi anataka kuongea na polisi mwenzie lugha yao unaleta pua yako. Watakupukusa na rungu ushindwe kutembea ili uwape hii nafasi ya kufanya their own conspiracy of silence, Mimi huwa naiita Police to police heart to heart talks.

Wana triple "W" woman, war and whisky, askari kamili alieiva anazunguka katika hivi vitu vitatu, askari alieiva anapenda sana mademu kwa maana ya woman, then anapenda sana ubabe usio na msingi ili adominate na kuwa superior na pia anapenda mtungi ndio maana wamewekewa na canteen zao za kulewa kwa bei chee kabisa ili watimize cycle yao ya W... Askari alieiva ni yule anaemiliki hizo "W" kikamilifu.

Kimsimgi sikumbuki ni lini nimeingia kwenye 18 za askari nikashindwa kumuwin psychologically maana physically simuwezi naanzia deep down his mental processing then mwilini najua patafuata tu yale niliyopandikiza akilini mwake during my first impression kwake. Make sure you Don't cross his line, ukimprovokes negatively utageuka nzi atakutega kwa mavi na sio Mchele kama ukiwa mpole, makini na mwelevu mwenye Pendo fake kama njiwa manga.

Nina mengi zaidi ya kushare na kudiscuss na nyie wakuu ila kwa leo tutembee na haya ya fasta fasta niliyoandika hapo juu, nikisettle vizuri nitaandika deeply and precisely kuhusu police psychology.

Lastly, tuwaheshimu na kuwasamehe ndugu zetu polisi kwa mengi mabaya wanayotufanyia inaweza kuwa sababu ya stress na solid depression wanayopitia kulingana na nature ya kazi yao pia niwape heko kwa kuwa miongoni mwa champion wa kuhandle stress wanazokutana nazo kila siku kazini na niwaase wanasiasa kutowatumia polisi vibaya kwa interest zao ili social harmony and peace itawale milele taifa la Bongo. Amen!

Imekaa vibaya kama Kally P.
images-71.jpg
images-74.jpg
images-73.jpg
images-69.jpg
image-20160805-484-37093z.jpg
images-70.jpg
 
Hiyo picha namba mbili huyo mjomba nimemuelewa ghafla

Sent using Jamii Forums mobile app
Mjomba hana neno yeye anakula vyombo tu huku wajomba wanapanga mikakati waanze kuwatoa watu machozi kwa moshi.

Sometimes, Don't complicate your mind in life! Relax kama jamaa hapa. Mambo yakienda kombo yaache yaende yenyewe usiende nayo.

Kaa chini barabarani, kula vyombo.
images-74.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hii mkuu ni kila Kitu! Shule! Lecture! Kifupi ni classic lesson! Ahsante sana.
I binafsi napenda sana kucheza na akili zao! Na Mara zote huwa nawin!

Kuna siku nlikuwa namrudisha Bi Mkubwa Ar na chombo chake, basi zile road block na chemli, nikifika tu, nasimamisha gari, nashuka fasta kabla hata kuambiwa, fasta nasalimia kabla hawajaanza! Huwa nawaambia: WAKUU WA KAZI HESHIMA ZENU!

Wanaitikia afu siwapi gap! POLENI SANA NA KAZI HII NYETI! Wanazidi kutabasamu!

Wakati wanazunguuka kuichungulia gari... Nawapa nyingine WAKUU MUNGU AWABARIKI SANA, BILA YA NYINYI SAA HIZI TUSINGEWEZA KUENDESHA!

Yaani Hapo tuna kuwa marafiki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom