Ukiijua hii Saikolojia na tabia ya Askari Polisi, hawatakusumbua sana

Hiyo saikolojia ya kumruhusu ajione mwamba kwangu huwa inafanya kazi hata kwa traffic mnoko vipi..

Mfano kuna siku nimepigwa mkono ile napack gari jamaa akagundua indicator yangu ya mbele chenga,inawaka ya nyuma na ile ya kwenye side mirror lakini bahati nzuri nilikuwa nalijua hilo tatizo basi ile kafika tu nikamchangamkia kwa salamu ya heshima kabisa akaniambia ebu washa indicator ya kushoto..hahaa sikumkawiza nikampa ukweli mzima kuwa sitaki kumpotezea muda bure na kwamba hiyo indicator ni mbovu na nimeagiza mpya so nakili kosa.Alifurahi sana kaka afande akaniambia hongera kwa kuwa muungwana endelea na safari.

Mwingine alinipiga mkono kisa nimeoverspeed kiasi tu basi nikamuona anakuja kasi,nikafungua mlango nikatoka natabasamu kama vile nafahamiana nae.Nikampa mkono akaleta wake pia,salamu huku namtania kuwa ndo nini kunivizia wakati vyuma vimekaza..
Mpaka hapo akawa mshikaji na akasahau kabisa kilichomleta mwishowe nikamwambia nawahi kidogo nitamcheki akaniambia safari njema.

Mifano ni mingi na hiyo ni baadhi tu.

Hawa wengine wapiga virungu sijawahi ingia anga zao hivyo sina mifano halisi.
 
Ogopa sana kuleta ujeuri au kuhojihoji na kujibizana na polisi, utapata tabu sana na hakuna atakaye kusaidia kwa muda huo. Hii kitu usije ukaifanya mahala penye watu wengi au anakabiliana na pressure ya mfano ya kutuliza wa upande huu au anazuia hili na wewe una leta mudomo. Muda wa kukusikiliza hana, atakachofanya ni kukushughulikia.
Nakubaliana na wewe mtoa mada kwa kiasi kikubwa sana lakini nakupinga kwenye W3. Sio askari wote ni walevi au wapenda K. Mambo yamebadilika mkuu. Askari wengi ni wasomi na waelewa sana tofauti na baadhi ya watu wanavyowachukulia. Zunguka vyuo vikuu vingi, nakuapia hutokosa kuwaona askari wasasoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hii mkuu ni kila Kitu! Shule! Lecture! Kifupi ni classic lesson! Ahsante sana.
I binafsi napenda sana kucheza na akili zao! Na Mara zote huwa nawin!

Kuna siku nlikuwa namrudisha Bi Mkubwa Ar na chombo chake, basi zile road block na chemli, nikifika tu, nasimamisha gari, nashuka fasta kabla hata kuambiwa, fasta nasalimia kabla hawajaanza! Huwa nawaambia: WAKUU WA KAZI HESHIMA ZENU!

Wanaitikia afu siwapi gap! POLENI SANA NA KAZI HII NYETI! Wanazidi kutabasamu!

Wakati wanazunguuka kuichungulia gari... Nawapa nyingine WAKUU MUNGU AWABARIKI SANA, BILA YA NYINYI SAA HIZI TUSINGEWEZA KUENDESHA!

Yaani Hapo tuna kuwa marafiki!

Sent using Jamii Forums mobile app
Neurolinguistic mind contol

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Morogoro Rd, baada ya Maboresho ya MWENDOKASI, kuna siku nikakunja pale Magomeni Usalama kuelekea Kwa Sheikh Yahya pasi kuzungunka zile taa zao! Hamad! Hawa hapa....! Mi fasta nikapaki pembeni, fasta nikashuka na kuwasalimia: WAKUU SHIKAMOO ZENU, NA POLENI KWA MAJUKUMU YA UJENZI WA TAIFA.... (waliitikia ile shikamoo yangu na huku nina uhakika wale walikuwa sawa nami kiumri ama nimewazidi!) Wakaniuliza wewe mbona unavunja sheria kwa kupita pasiporuhusiwa? Ni kawajibu ni kweli kabisa na naomba radhi ka hilo, na nawashukuru kwa kunielemisha, bila ya nyinyi humu kungekuwa na ajali nyingi sana, kiukweli mnatusaidia sana! Kiukweli sikutoa hata 100 na wakaniruhusu niende!
 
Hiyo saikolojia ya kumruhusu ajione mwamba kwangu huwa inafanya kazi hata kwa traffic mnoko vipi..

Mfano kuna siku nimepigwa mkono ile napack gari jamaa akagundua indicator yangu ya mbele chenga,inawaka ya nyuma na ile ya kwenye side mirror lakini bahati nzuri nilikuwa nalijua hilo tatizo basi ile kafika tu nikamchangamkia kwa salamu ya heshima kabisa akaniambia ebu washa indicator ya kushoto..hahaa siku mkawiza nikampa ukweli mzima kuwa sitaki kumpotezea muda bure na kwamba hiyo indicator ni mbovu na nimeagiza mpya so nakili kosa.Alifurahi sana kaka afande akaniambia hongera kwa kuwa muungwana endelea na safari.

Mwingine alinipiga mkono kisa nimeoverspeed kiasi tu basi nikamuona anakuja kasi,nikafungua mlango nikatoka natabasamu kama vile nafahamiana nae.Nikampa mkono akaleta wake pia,salamu huku namtania kuwa ndo nini kunivizia wakati vyuma vimekaza..
Mpaka hapo akawa mshikaji na akasahau kabisa kilichomleta mwishowe nikamwambia nawahi kidogo nitamcheki akaniambia safari njema.

Mifano ni mingi na hiyo ni baadhi tu.

Hawa wengine wapiga virungu sijawahi ingia anga zao hivyo sina mifano halisi.
HIYO UKIMFANYIA LAZIMA AWE MPOLE!
 
Mjomba hana neno yeye anakula vyombo tu huku wajomba wanapanga mikakati waanze kuwatoa watu machozi kwa moshi.

Sometimes, Don't complicate your mind in life! Relax kama jamaa hapa. Mambo yakienda kombo yaache yaende yenyewe usiende nayo.

Kaa chini barabarani, kula vyombo.View attachment 841877

Sent using Jamii Forums mobile app
ILA HYU JAMAA CHAPOMBE ana guts za hali ya juu sana!
 
Uko vizuri mkuu.
Vipi nasikia hao jamaa hawana urafiki wa kudumu na mtu. Kukugeuka ni sekunde tu hata kama mnaaminiana kiasi Gani. Kuna kamsemo "hakuna urafiki na polisi" . Kuna ukweli wowote?
Kuhusu superiority naunga mkono hoja pia maana tuliwahi kwnda kuripoti kitu cha kawaida sana kituo cha polisi. Pale counter tukapewa maelekezo tukaja mida waliotuelekeza tukaja mkuu wao yupo, alianza mikwara mingi vitisho tukaamua kuondoka kuachana naye tupoondoka ndio akatuita akawaambia wale jamaa watuhudumua. Sikuona sababu ya Yale yote nadhani hoja ya superiority complex nimeielewa vzr.
 
Mimi nmekua katika mazingira ya kuona wazazi wanakamatwa mara kwa mara...
pia nmekulia mazingira ya jeshini.

unachokisema bwana Mleta uzi ni kweli japo sijasoma yote.
lakini mm mapolisi nawachukia sana hasa walio wabaya , lakini wakija na purukushani zao maviatu mpaka ndani, nawakaribisha vizuri karibuni sana ndugu zangu yani nawasalimia watanichachafya weeh na maneno ya karaha nawajibu taratibu ,tutakutia pingu nawaambia nisawa kwakua nmekosa.

yani ukijifanya mjinga inasaidia sana japo laiti kama wangejua hasira inayonifukuta wasingenisogelea.
ila naamua kuikopa furaha na calmness kwa manufaa yangu binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom