Ukihitimu chuo hasa kijana wa kiume, kubaki nyumbani ni uoga au akili?

kofia ya plastiki

JF-Expert Member
Jun 9, 2019
416
404
Kuna mjadala kwamba vipi waliohitimu elimu ya juu hasa wanaume, kwa situation ya sasa ya kukosa ajira za kudumu kuendelea kubaki nyumbani ni uoga au akili ya kuwa ukitoka nyumbani usalama wako unakuwa mdogo?

Aither kuna utafiti kuwa vijana wengi hawawezi kuishi maeneo ya nyumbani, yaani mazingira yale aliyokulia, kwa hofu kuwa baadhi ya raia hasa wale waliofeli form 4 na primary standard 7 Watamuuliza maswali ya hapa na pale, hivyo wanaona bora watimkie mbali kidogo na pale.

Vipi, wewe una maoni gani juu ya jambo hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya wahitimu waachieni wahitimu, kazi hamwezi kuwapa mnawasimanga utafikiri mlilazimishwa msisome. Historia inaonesha wanajamii wengi tuna asili ya UJIMA, kusoma ni kuongeza maarifa na haimaanishi ujitenge na familia yako ata kama utapata mali au kazi nzuri.

Mh Rais pamoja na kazi yake ngumu yeye mwenyewe akipata likizo anafurahia kwenda kwao na pengine anafurahia chakula cha asili wanapopika ndugu zake.

Si lazima tuishi mifumo ya mabeberu.

Nawapa moyo wahitimu msiogope kukaa nyumbani kama ni salama, msije jikuta katika uhuni, madawa na biashara haramu ya kununua na kuuza penzi. Kitu cha msingi kama upo nyumbani shirikiana na wanafamilia katika kazi za kila siku.

Amen
 
Back
Top Bottom